TAFUTA HAPA

HADITHI:Utamu wa Sukari Guru- 6

Kibua yupo tayari mjini akifanyakazi katika nyumba ya mjeda mmoja anayekwenda kwa jina la Richard. Tuliachana wiki iliyopita kwa Richard kukutana na msichana ambaye wamepotezana miaka 20 iliyopita.Wamekutana ulevini. Je kitatokea nini kwa Kibua?

"Nikoboadi Richard, niko likizo na jamaa ameondoka kwenye advansi pati."
"Wanatakiwa kurudi leo."
"Umejuaje?"
"Idara yangu ndiyo inayowalipa."
"Yaani Richard, nimekukosea nini kumbe unajua kwanini hata kunitafuta?"
"Mke wa mtu wewe na sipendi masikhara na mashapushuta."
"Angeelewa nini?"
"Yeye si mjinga hivyo, nilikuwa naye Mbweni nilimtangulia miaka miwili."
"Unataka kunambia hata wakati ule tunakutana wewe ulikuwa unafanya kazi hii."
"Naam kwani tatizo lilikuwa lipi?"
"Mimi nilijua unafanyakazi ya kufahaulisha mizigo bandarini."
"Ndio na ndio kazi niliyosomea."
"Mbona ofisi yenu ilikuwa NIC."
"Wakati ule nilikuwa kwenye idara ambayo ofisi yake ilikuwa kitegauchumi."
"Kwa hiyo ulikuwa kaunta."
"Naam!"
"Imekuaje sasa unamlipa mume wangu?"
"Baada ya kazi ya Kongo nilibadilishwa kazi. Nikajifunza uhasibu.Nikafanya kazi za uhasibu. Mtu mmoja akauza jina langu. Nikajulikana. Nikarejeshwa kuwa peimasta."
"Pole. Sasa nambie... " akaenda kumnong'oneza sikioni.
"siwezi."
"Nisaidie Richard."
"Mbona siwezi."
"Angalau mara hii moja tu."
Akamkazia macho, akamlegezea, Richard akapatikana.
Saa saba na nusu usiku, wakati wanaingia sebuleni, wakati wako tayari kwa kile kilichowapeleka pale, wakati Mariana anataka kukumbuka miaka 20 iliyopita, akisema maneno ambayo hajawahi kuyasema kwa mume wake, wakiwa watupu, Land Rover yenye namba za jeshi ilikuwa inamshusha mume wa Mariana katika yadi. Mariana aliona, Richard aliona wakatazamana.
Mume wa Mariana alikuwa anachukua hatua ndefu zenye kuonesha uaskari na yumkini hakuwa na mashaka na nyumba yake. Richard alimtazama mtu Yule akijua rekodi yake kwamba huwa haachi mateka wake hai, aliangalia  suruali ilipo akakumbuka kuwa ipo chumbani, lakini kwenye kochi kulikuwa na  kitenge akakikwapua kitenge kile na kutokomea.
Uani alikutana na ukuta wenye umeme, akauangalia, akakumbuka mafunzo yake ya ukomando, hakuna cha kufanya mume wa Mariana ana machale si kawaida. Alifunga vizuri kitenge kile, akachupa juu kama anapiga teke farasi akazunguka na kuangukia kwenye kichochoro cha nje, akatulia.
Kulikuwa shwari akaondoka na kuvuta hatua akiwa amejifunga lubega kuelekea nyumbani huku akiwa katika maumivu makali, mishipa yake  nyeti haikuwa ya kawaida ilikuwa  katika mazingira magumu sana.
Alivuta hatua na kufikia teksi akachukua na kuelekea nyumbani.
Ilikuwa salama kwa Richard, lakini hakuwa na uhakika ni salama kiasi gani.
Mariana baada ya kuona kwamba, Richard  ameshachomoka, alimfungulia mumewe akiwa kama alivyozaliwa.
“Mbona taa zinawaka” alisema mume mtu  baada ya kukumbatiana na kusalimiana.
“Nimekosa usingizi mpenzi nakuwaza tu”
“Haya nimerejea salama, tumewahi kidogo kwa sababu ya utaratibu wa safari”
“Welcome home dear”
“Thanks”
Akalianzisha hapo hapo sebule, nia ni kumchosha ili wakati akipumzika aende akafiche nguo za Richard zilizokuwa zimezagaa kule chumbani walikoanzia matatizo yao ya miaka 20 iliyopita na hasa bangi waliyoivuta pamoja.
Mume wa Mariana alichukua muda mfupi sana kutulia kwani alikuwa amechoshwa na usafiri wa saa 12, akaomba mapumziko akaambiwa asubiri atengenezewe juisi, wakati akisubiri alilala palepale.Mama akanyata na kwenda kuweka kila kitu sawa.
Richard alifika nyumbani na kuingia moja kwa moja chumbani kwake kukawa hakukaliki. Alishakuwa stoni ile mbaya na maungo yake mateke hayakuwa rafiki tena, ashukuru tu lubega aliyoipiga.
Alipowasha taa sebule alikutana na Kibua ambaye naye alikuwa ametoka chumbani kwake baada ya kusikia mngurumo wa gari nje na kuja kutoa huduma.
Alimwangalia baba yake alivyo akashuku kwamba ana matatizo makubwa sana.
“Shikamoo”
“Marhaba”
Kibua alimuona baba yake katika hali ambazo wanaume wote huwa nazo.Akadharau si tatizo lake, akaenda akamwekea chakula chake na juisi, akamkaribisha. Alipomaliza kula tatizo likawa lipo palepale.
“Naweza kukusaidia mzee una tatizo gani”
“Halikuhusu”
“Najua halinihusu lakini naona katika mazingira ya kawaida una shida kubwa na hasa wakati huu ambapo mama hayupo.Naweza kukusaidia”
“We bado msichana mdogo”
“Najua lakini mimi ni mwanamke na najua shida za wanaume, sema nitakusaidia”
Richard alimtazama mtoto Yule ambaye alikuwa anadhani anafaa sana kuwa mkwewe kwa jicho la huruma.
“Huwezi chochote hapa Kibua nenda kapumzike”
“Mimi siko mzima”
Mzee alisikia kizunguzungu, alipoamka na akili zake, alimuona Kibua akimuogesha.
“Kumetokea nini?”
“Nikuulize wewe”
“ Ndumu kitu mbaya sana”
“Unazokumbukumbu?”
“Zimerudi zote.Usiseme kwa mtu”
“Siri zako zote zipo kifuani mwangu, kwa sharti moja tu hutarudia kuomba ulichoomba jana huku unalia”
“Haiwezekani, ilikuwa furaha”
“Kwako.”
“Ndio kusema?”
“Hutanigusa kwa namna yoyote, kunidharau au chochote kile na hutajifaragua”
“Mbona masharti makubwa”
“Nipe fedha zangu nirejee kwetu.Msaada isiwe utumwa”
“Mimi nitakuwa nyumbani muda mwingi, sitasahau”
“Nilipie shule nitakuwa nyumbani mama atakapokuwa anakaribia kurejea”
Alikaa muda mwingi kisha alikubali, alisogezewa karatasi akaandika kiapo, akaandika na kuahidi kumpeleka shule mpaka amalize.
itaendelea