Chioma amejikuta amempenda kibua. akawa anamsemesha lakini kibua amekuwa akikataa akimwambia kwamba yeye ni mama yake mdogo.Tunajua kulitokea shida fulani na Kibua alisawazisha.Je ana haki kwa hilo kujiita kwamba ni mama yake? Chioma atakoma kwa kauli hizo hasa baada ya kuulizwa maswali na baba yake?
Kibua alikuwa anatengeneza mboga jikoni wakati Chioma alipoingia bila taarifa na kumgusa maungo yake kiuchokozi. Kibua hakuruka na badala yake alimgeukia na kumwangalia kwa pozi.
"Unataka nini Chioma jikoni huku"
"Wazazi hawapo naona tuendelee na mauzngumzo yetu ya siku nyingi zilizopoita"
"Mazungumzo?"
"Ndio mazungumzo unajifanya umesahau?" alisema kwa tabasamu kubwa.
"Mhh sijui kama kuna kipande cha mazungumzo ambacho mimi na wewe tumekiacha mahali?"
"Ndio. Tuna kipande. Umekuwa ukinikimbia muda mwingi sasa leo tumebaki wawili lazima unijibu"
"Kama nisipokujibu utafanya nini?"
"Nitajua wakati huo?"
"Nichukulie kama tishio?"
Alitulia kidogo kwani aliona sauti ya Kibua ilibadilika ghafla na kuachana na ile ya kubembeleza. Haikuwa rahisi, alimtazama akamuona akifinya macho kidogo na kuyaachia.
"Usiwe na mashaka. Nataka tuzungumze tu."
Kibua akashusha pumzi na kubadili mkao wa kisu.
"Unataka nini kwangu Chioma."
"Nataka penzi lako."
"Hujachoka tu?"
"Nichoke kwa sababu gani?"
"Unaniona sikujali, kwanini unanitakia shida?Unataka kuchukua vinavyochukuliwa na baba yako?"
"Hii haiwezekani,"
"Sikia wewe mtoto wa kiume.Ukiambiwa kitu usikilize kwa makini. Sitaki kuyumbisha familia hii. Pili nimelelewa kwetu siwezi kuchanganya watu, hasa mtu na baba yake.Ninachotaka kukuambia kisa cha kutokukubalia ombi lako kwa kuwa baba yako keshapita hapa"
"Hii haiwezekani"
"Mbona neno lako la hii haiwezekani unalirudiarudia sana?Haiwezekani kwa kuwa mimi si mwanamke au unadhani kwamba baba yako ana heshima sana?"
"Moja ni kweli kwamba yeye ana heshima sana, pili wewe si saizi yake"
"Kwani mimi saizi yako?"
"Ndio kijana mwenzako."
"Kwetu ninakotoka na nadhani hata kwenu mtoto wa mwenzako mkubwa mwenzako. na kwetu ukishavunja ungo ukatokea misimu miwili mitatu mingine unaolewa, sasa mimi shida nini au unaona shida kusema shikamoo mama?"
"Wewe unanidanganya?"
"Nikuambie Chioma?Muulize baba yako?"
"Ili nilete ugomvi?"
"Kwanza huleti ugomvi leo si anarudi? Mwambie hivi baba mimi nataka kumuoa Kibua. halafu umuone atakuambia nini"
"We unadhani ni rahisi?"
"Kama si rahisi, basi jua kuwa mimi mama yako, natunza siri za baba yako"
"kwenda zako" aliondoka Chioma akiwa amechanganyikiwa kabisa. baba yake nini anakosa kwa mama yake mpaka anamchukua mtumishi wa ndani? Tena mtumishi ambaye anamsomesha kwa dai kuwa anasaidia sana pale nyumbani?Katika kusaidia haikuwa masikhara binti alikuwa anajua kutia mzigo kuanza bajeti ya nyumba hadi mahitaji yake. Mama yake amemsifia sana, lakini kama hilo silo inakuaje sasa?
Alirejea chumbani kwake akaenda kupumzika.
Kibua pale akaendelea kutengeneza mboga zake kama vile hakukutokea kitu. Akawa anawaza mambo mengine, alikuwa anamwaza mama yake, kipindi kimepita na alikuwa haelewi kama anajua kwamba mwanae alikuwa amebadilika sana.
Alikuwa anajua anachotaka nini, alikuwa anajua wanaume wanataka nini toka kwake, akawa anajua vile vile namna ya kuwakwepa. Mtoto wa baba mwenye nyumba alikuwa kijana mwenzake, anayeweza kabisa kuwa naye lakini ataweka wapi aibu ya kutembea na baba na mwanawe.
Pamoja na ukweli kwamba muonja asali huchonga mzinga, kwa shida yake ya kutaka kuendelea kusoma, alifanya mikataba ya ajabu ambayo imemwezesha kukaa pale kwa muda mwingi, akiwa mpole lakini akiwa anasoma kwa manufaa yake.
Alikuwa na hasira ya kutopelekwa shule, lakini pale alipogundua kwamba anaweza kwenda shule, pamoja na kumjua baba mwenye nyumba kwa bahati mbaya, baadae alikuwa anakwenda naye kila mama mwenye nyumba anapokuwa hayupo japo kwa usiri mkubwa.
Alizitafuta siri za baba mwenye nyumba akazipata, akazitafuta za mke akazipata na kutokana na kuwajua vyema aliweza kuishi nao bila mama mwenye nyumba kupiga kelele.
Alitamani kurejea nyumbani kumuona mama yake alikuwa amechoka na makisha yasiyokuwa na uhuru. Alijua kama atashinda mtihani wake ataingia kidato cha tano na kuanzia hapo atajua nini cha kufanya.
Wakati akisubiri matokeo alikubaliana na nia yake ya kwenda kwa mama yake. Alikuwa tayari ameshazungumza na baba mwenye nyumba ambaye kwanza alikataa na baadae alipomuona mama mwenye nyumba alipata kibali, kwani alisema si vyema kwa yeye kukaa pale miaka mitano bila kumuona mama yake.
Wakati anakaanga mbona mama mwenye nyumba aliingia pale.
"Ha mama sikukuona"
"Una mawazo mengi huwezi kuniona"
"Nimemkumbuka sana mama yangu sijui ana hali gani"
"Nimetoka kukukatia tiketi ya Reli, utaondoka na basi daraja la kwanza kesho, utafikia Morogoro mapema sana sijui huko kwenu sasa utafika saa ngapi"
mabasi ya Reli yanaingia morogoro saa tano, nitawahi tu mama basi la mwisho"
"Hautapotea kweli?"
"Wala mama hakuwezi kuwa na mabadiliko makubwa vile"
"Haya, mimi naondoka jioni hii, utaikuta kwa baba tiketi hiyo nilishamweleza kwamba unastahili kwenda kumuona mama, mwezi Aprili baada ya Pasaka waweza rudi, ukaangalia matokeo halafu ujuwe utafanya nini."
"Mama nawapendeni sana nashukuru kwa kunisaidia"
"Mimi nikushukuru wewe kwa kunitunzia mume wangu.Manake mwenyewe kwa pilikapilika huwa naona simsaidii yoyote humu ndani"
Huku akiwa ameinama, manake hakumwelewa vyema mama yake yule hasa mazungumzo yake kwamba anamtunza mume wake, alijikaza kisabuni. kweli alimtunza mume wake, tena alimtunza kila kitu japo chanzo kilikuwa msaada mdogo.
"Usijali Kibua hapa nyumbani kwako"
"Haya mama"
Aliondoka na kuelekea chumbani kwake.Kama alivyokuwa amemweleza mama Chioma alipomaliza kula cha mchana, akaenda kulala na saa 11 walitoka na mumewe na mtoto wao wa pekee na kuondoka safari, walirejea nyumbani Chioma na baba yake.Baada ya kuhakikisha kwamba amewatengea chakula na yeye akaketi akala pale mezani.
Baba hakuwa na mazungumzo, wakati ananyanyuka Chuioma akaachia mdomo.
"Mzee ninahitaji kuzungumza nawe na hivi mama hayupo"
"Hatuwezi kufanya kesho, nimechoka nahitaji kupumzika, lakini kwanza nataka kusoma sebuleni hapo"
"Sawa baba. Kama hivyo wacha niende klabu kidogo"
"Mbona usiku "
"Si sana baba."
"Lakini siku hizi naona majira ya usiku si salama sana."
"Sawa baba , lakini basi wacha nichukue tusker hapa naenda chumbani kupumzika" akatoka akaenda kwenye jokofu akachukua bia zake nne akaondoka nazo chumbani.Alifikiria sana kauli ya Kibua kule chumbani akaamua kubugia pombe fasta ili alale, na kweli alilala.
Kibua kwa upande wake baada ya kuhakikisha vyombo vimerejeshwa mahali pake vimefanyiwa usafi, akasafisha jiko na kurejea chumbani kwake. alipanga mizigo yake na alipomaliza alikuwa amechoka akajitupa kitandani na usingizi ukampitia.
Alishtushwa na sauti ya kugongwa kwa mlango, ulikuwa unagongwa taratibu.
itaendelea