TAFUTA HAPA

HADITHI:Utamu wa Sukari guru- 4

Ha ha ha Shemeji,mbona utateseka.Angalia usijiapize  unaweza kufa lazima nije na kuna siku nitakuja bila kualikwa, na ukiona nimefika na mkeo hayupo jua nini nitakachofuata,itakuwa kama leo. Kwaheri . Hayo ndiyo maneno ambayo alisema Kibua wakati akijilamba kwa utamu aliouonja wa shemeji yake kwa Semie, Je kunaendelea nini?

Wakati Severine, amechanganyikiwa kabisa na hali aliyokuwa nayo baada ya kubakwa kwa staili ya aina yake, huku akifikiri kwamba yule binti kama si mchawi atakuwa ni shetani huku akishuka milima kuelekea kwao Kimbinyiko, Kibua alikuwa anatembea taratibu huku moyo wake ukiwa na furaha kubwa. Ametekeleza hamu ya mwili wake.
Tukio hilo lilimjia waziwazi kichwani mwake wakati akimsikiliza Semie akichachawa nyumbani kwao alipokuja kumuuliza alimfanya nini bwana wake.
"We rafiki yangu inakuaje unaingia katika himaya yangu,"
"Naye bwana wako fala kwelikweli, ndio nini kusema tulichokifanya"
"Anasema umemchawia"
"Kweli kabisa Semie?Nimemchawia, mimi Kibua kwa uchawi gani hasa?"
"Unaujua mwenyewe?We utakua lini mbona una mambo ya kizamani sana"
"Mwaka gani hasa, manake huu mwaka 1970?"
"Unajua mwenyewe, kwani umeambiwa dawa zako hizo ndizo umpe kila mtu"
"Ukome mwanahizaya wewe" alisema kwa sauti ya ukali.
"Nimekuzoea. Huo ukali ndio nini?"
"Wanaume zenu dhaifu nikiwatazama tu wenyewe wanakubali"
"We lazima uwe kibwengo"
"Mimi Kibwengo, Semie tutagombana"
"we ulifikiri nimetoka Kimbinyiko mpaka hapa kufanya urafiki?Nimekuja kukuwasha nione utanifanya nini ngedere we"
"Duhh rafiki sasa hii imekuwa kubwa nimegeuka ngedere tena. Kwanza wewe unamchosha tu mtoto wa watu. Dagho umemwacha,Solasolala naye je? Mimi nikimtaka mwanaume niko mbaya ila wewe unawachanganya ndugu unaona si vibaya. Huna haya kwelikweli.?"
"Kwani we hujui kama yuke mchumba wangu"
"Kwa lipi kwanza manake umevaa mangaja na khanga za watu zaidi ya wanne nani mchumba?"
"Huyu ndiye mchumba. Na kesho kutwa wanakuja kutoa mahari"
"Akutolee tu, lakini mie nishapita"
"We mimi nitakupeleka kwa mangalughome"
"Kama na wewe huna dhambi nipeleke tu mwaya"
Wakatazamana, Semie akachoka kabisa kwa jinsi rafiki yake anavyomgeuzageuza kila mara.
"Lakini kwanini kila mara unakuwa adui yangu, unachukua vitu ninavyovipenda."
"Navichukua kwa sababu najua huvipendi"
"Lakini kwa Seve si kweli angalau hili nilikueleza kwamba lazima kabla ya msimu wa kilimo anioe, kwanini unaniingilia kila mahali"
"Kweli mla kunde husau, lakini mtupa maganda hasahau. Niliapa kuwa yoyote atakayekufaa nitatoka naye. Dagho na Sola  wale ukoo wangu nimekataa haramu. Lakini kila ukipotea njia ukatoka nje ya ukoo wangu ha! lazima ulie kiwaziwazi au kikimya kimya"
"Huyu humpati tena"
"Utanikuta naye mno uriri wako (kitanda mwako). Sijui utafanya nini mwaya! Ha! manake hata kupigana huwezi"
"Nitakuua"
"Huwezi, hata kwa uchawi huwezi"
Akamtazama, kweli hamuwezi halafu huwa hajui kwanini huwa kila mara anamshinda. Lakini bado alikuwa kila mara anamshauri vizuri, lakini tangu aliposababisha mwanaume aliyemuingiza ukubwa aondoke jumla,wamekuwa na urafiki wa mashaka.
"Huu urafiki wa mashaka utaisha lini"
"Ukimrudisha yule aliyesema kwamba akirudi yeye ni kigori"
"Mimi nitamrudishaje?"
"Kwani ulimkimbizaje?"
Akamtazama tena, kisha akajua wanakoenda si kuzuri:
"kwaheri Kibua"
"Unaondokaje  bila kunipa jibu?"
"Jibu gani nawe ni mwehu"
"kumbe unajua ehee! umefuata nini hasa?"
"Nilidhani naweza kukuomba uniachie Seve wangu"
"Kwani mimi namchukua, wewe ndiwe umesema namchukua! Kwa utamu gani alionao. Mshamba yule katoka Nyingwa"
"Leo bwana wangu mshamba katoka Nyingwa!"
"Kama hujui ndio nimemtoa ushamba halafu huwa siwamaindi watu wa aina yake, hiyo injini yako mama kaitulize mzuka wake"
"Aksante"
Semei akiwa amechukia kabisa na huku uso umemuiva kwa kushindwa kujua amfanye nini  Kibua, huku akijenga taswira ya hasara katika uchumba wake kwani alitambua kwamba mara zote Kibua hutekeleza tishio lake, alianza taratibu kushuka milima kwa njia ile ile aliyokuwa ameijia.
Kibua kwa upande wake alimtazama kwa nyodo jinsi alivyokuwa akishuka akifurahi jinsi alivyomuweza. Alitabasamu.
Kibua kwa namna fulani alikuwa binti ambaye anapenda kuudhi watu hasa wale ambao wamemfanyia visa vinavyomnyima raha na kwa Semei alikuwa amekamilisha alichotaka, lakini kumuumiza zaidi ni alitaka lazima amfumanie na mchumba wake katika kitanda chake, kukomesha ngebe zake.
Alimfuatilia mpaka alipoingia Dawilo,akiwa mdogo katika macho, aligeuka na kuelekea katika chumba chake.Alikitazama chumba kile kisha akaamua kuanza kupanga nguo zake katika sanduku lake la mbao kwani alijua ima faima safari ya kwenda mjini ilikuwa imeiva.
Hakujua anatakiwa kufanyakazi ya aina gani, lakini alijua kitu kimoja tu kwamba mama yake alikuwa anataka aondoke pale ili aweze kupata raha, manake, hakuwa na raha kutokana na jinsi yeye alivyokuwa akiendesha maisha yake.
Alimfikiria huyo mjomba wake ambaye mara zote hajui kama ni mjomba wake kweli au baba yake. Alikuwa ni mtu ambaye akimwangalia hawezi kumtazama moja kwa moja hadi  siku alipogombezwa na mama yake kwamba si vyema kumwangalia mtu mzima kwa macho ya juu juu.
Alipomaliza kukunja nguo na kuziweka katika sanduku alichukua maji akayainjika na baada ya kuchochea kuni na kupata moto aliipua na kuingia nayo chooni , muda wa kujisafi ulikuwa umefika hakutaka kulala na janaba la mtu.
Itaendelea