Sukari Guru ni Kibua.Na haya aliyasema mwenyewe kwamba yeye ni sukari guru haifai kwa chai. Luwanda alipashwa akapashika kwamba hawezi kufaa kwa limao au ndimu.Nyumbani mama naye anasema mwanae mcharuko. je hali inaendeleaje?
"Haya niambie mjomba gani anataka kunisaidia kupata kazi?"
"Baba Nesta"
"Hakuna nia njema kwake mama"
"Ipo dada(alizoea kumuita mwanae vile) suala ni wewe kujua umefuata nini pale"
"Haya mama"
Aliendelea kukishambulia chakula kile na kisha kumaliza akatwaa vyombo
akavipeleka jikoni akamuaga mama yake akaenda kulala, kesho ilikuwa Jumapili alihitaji kudamka mapema kuwahi misa.
kitu cha jaabu kabisa, aliwahi misa na akasali kwa bidii sana lakini alipotoka tu nje na kusalimia watu wawili watatu alimuona mtu ambaye huwa anamkimbiza mbio dhana ya dhambi ikaanza kujijenga kichwani mwake. malaika katika mwili wake walianza kushindana pasi shaka walikuwa malaika wawili mmoja mwenye nidhamu mwingine bule bileshi labda alikuwa ndiye aliyetoka motoni.
Mmmoja alimwambia ulishasema wanaume watu wa hovyo nini kumwangalia kwa jicho la tamaa mwingine akasema huyu akikuuoa atakuwa mume bora hasa kwa kizazi chako, kitakuwa supa.
Severine kijana ambaye aliondokea kumpenda bila kumweleza, alikuwa anatoka katika ukoo ambao watu wake wengi wana rangi ya maji ya kunde iliyokoza, walikuwa na mazoea ya kuitwa wazungu. Walikuwa na kasoro moja walikuwa wanaringa sana.Pamoja na kuringa inaaminika kwamba wao ni wachawi na mara zote wanapooa au kuolewa watu wa huko upande wa pili huharibikiwa kwani mtu huyo hatajali nyumbani kwao. Ilikuwa dhana dhaifu kuifikiria, lakini Kibua alikuwa na kila sababu
ya kutaka kufikiri.
'Ahh, mtoto mzuri Yule hawezi kuwa mchawi' alijisema kibua huku akiwa anauma mdomo wake na kusogeza vyema miguu yake. badala ya kumfikiria kwa neema akawa anamfikiria kijana wa watu katika mambo anayoyapenda yeye.
'Mimi si kawaida nimeupata wapi ugonjwa huu kama si wa DNA. Mbona nateseka hivi ahh nitamvaa' akarejea katika akili akamuona severine akielekea njia ya Kimbinyiko, akavuta hatua kumfuata.
"Sema mvulana wa Kimbinyiko" aliita Kibua kutoka pale alipokuwa amemkaribia, Severine ambaye alikuwa katika mawazo yake aligeuka na kumuona Kibua.
"He leo unatutembelea?" alisema.
"Nimekuona, halafu umekuwa si mtu wa misele tena naona umepita maduka yote peke yako unaondoka"
"Ahh Kibua we nina matatizo kibao kichwani mwangu naona nikae nyumbani nifikiri"
"Semie kafikisha hoja ya kuolewa nini?"
"Ahh"
"Lakini kifaa kile, kwanini usikubali tu"
"Nikuulize swali"
"Uliza"
"Nini kinakufanya uwatake wanaume?"
"Kile kinachokufanya uwatake wanawake, mapenzi tu"
"Wewe ni aina gani ya mapenzi unayataka?"
"Mbona unaenda haraka sana Severine?"
"Asiyekujua wewe lazima awe na wazimu"
"unataka kujua ukweli haraka?"
"Sidhani kama nataka kujua ukweli"
"Mimi sikugandi wewe kama Semie anavyofanya.Mimi nakutaka wewe tu kwa muda nifurahi, mengine historia"
"Ha ha ha ha!"
"Kinachokuchekesha nini?"
" Umekuwa mwanaume unasema tu"
"Cha ajabu nini umependa usiseme nani akusemee"
"Hivi aliyekuambia kwamba unaweza kufanya ujinga na mimi nani?"
"Kichwa changu"
"Mbona siwezi?"
"Si kweli unaweza ila kama hutaki sema tu, mtoto mzuri."
"Mimi sitaki"
"Angalau tuwe marafiki" alimnyoshea mkono, hakumwelewa,pepo wa ngono alishamtawala, walikuwa katika eneo ambalo lina mikataruba mitupu,Severine aliponyoosha mkono hakujua kumetokea nini, akili ilipompata alikuwa dunia nyingine.Alitikisa kichwa kurejesha akili, Kibua alikuwa pembeni mwake anatabasamu.
"Unajisikiaje"
"Wewe ni mwanaharamu"
"Nikuulize swali"
"Swali gani mshenzi wewe"
"Sukari guru tamu au chungu"
"Huna adabu"
"Adabu ninayo, nimekuheshimu sana"
"Kwanini unapenda kutumia nguvu"
"Semei alifichua siri yako, nataka mtoto rangi yako hasa wa kike"
"Semei?"
"Ndio. Anatamba sana kwamba lazima utamuoa uko hoi wala hutapiki"
"Huwa mnazungumza wapi?"
"Rafiki yangu yule kumbuka"
"Nitamweleza ulichofanya"
"Kama unao ubavu huo?"
"Unanitaka nini?"
"Nilichotaka nimekipata. Unakoza wewe!Semei kapata mume"
"naenda kumwambia"
"Sasa naona akili imekurudia.Aksante Severine"
"We mchawi, umeniwangia"
"Wala siwangi wala sichawii, umejiachia sana, imenisaidia sana.Aksante nakualika tena na tena kama utaweza"
Akanyanyuka akatengeneza gauni lake vizuri.
"Kwaheri shemeji"
“Shemeji yako nani?”
"Utakuwa shemeji yangu daima"
"Na sikualiki nyumbani kwangu"
"Utamuoa semei, Semei atanialika."
"Tuone kama utakuja"
"Ha ha ha Shemeji,mbona utateseka.Angalia usijiapize unaweza kufa lazima nije na kuna siku nitakuja bila kualikwa, na ukiona nimefika na mkeo hayupo jua nini nitakachofuata,itakuwa kama leo. Kwaheri" alisema huku akimrushia maneno matamu huku akitabasamu.
Severine, alichanganyikiwa kabisa na hali aliyokuwa nayo. Si bure yule binti ni mchawi, kumetokea nini? Akajikagua, akaguna.
Severine hakurejea barabarani, alishuka milima ile moja kwa moja nyumbani kwao Kimbinyiko akamkuta, mchumba wake akiwa anaandaa ugali kwa konge.
Itaendelea