TAFUTA HAPA

HADITHI:Utamu wa Sukari Guru-12

Kibua yupo katika duka la chai maarufu kama mgahawa wa Muholo na kijana mmoja ameingia nay eye akashindw akujisititi, Kibua uzalendo ulimshinda je kumetokea nini.

Moyo wa Kibua uliendelea kupiga, wakati yule kijana anamtazama. Akamsoma vizuri akamuona kama ana miaka basi si zaidi ya 35.Wakati supu inafika pale Kibua akajitegeza.
“Kaka kama vile nakujua!”
“Mimi ?”
“Ndio wewe kwani tupo wangapi humu ndani?”
”Tupo watatu hapa pamoja na Berege na namuona anatoka nilidhani unazungumza naye” alisema kwa kutabasamu.
“Ha ha ha” alicheka.
“Naona umefurahi”
“Lazima manake unapoulizwa swali la namna ya kuanzisha mazungumzo nawe ukafurahi kwa sababu ulitaka mzungumze ukasita lazima ufurahi”
Akamwangalia moja kwa moja.
“Naona umemaliza, chai yako naweza kukuitia supu naona inapendeza sana”
“Sitajali kama haitakuwa na masharti”
“Masharti lazima yawepo bibie”
“Kama yapi?”
“Wewe mwanamke na mimi mwanaume unaonaje kwa kuanzia hapo”
“Mhh hili la ajabu zaidi. Mimi najua kwamba ni mwanamke na wewe ni mwanaume. Sasa unachotaka wewe si ukiseme tu”
“Kwani wewe ulianzisha mazungumzo ya kutaka kunijua au?”
“Hapana nimekuona nikakupenda sasa wewe kusema kwamba na mimi umenipenda kuna shida gani?”
“Duhh wewe umetoka mjini nini?”
“Mjini wapi? Morogoro?”
“Sidhani! Tabia za aina yako wanazo wanawake wa Kibaoni ambao wengi wao wapo  kumwani Dasalaam.” Alitabasamu. Tabasamu lile tangu wameanza mazungumzo lilimpeleka eneo baya zaidi Kibua.
“Ni kweli nimetoka kumwani. Lakini kukueleza kwamba mimi nimekudondokea ni tatizo kweli?”
“Si kawaida mwanamke kuanza”
“Sasa nimejiachia unajigonga tu kwanini nisiseme?”
“Haya  mama supu inapoa hiyo na ikipoa hutaila, mbuzi wa leo amenona sana”
“Naona ya kwako ndio kabisa”
“Kuna kipupwe lakini si haba.Nambie unakwenda wapi?”
“Mimi naenda juu Masarawe.”
“We umetoka Lughongo?”
“Swadakta”
“Khaa”
“Mwe shida nini” alisema kwa maringo.
“Marigho (matusi), ugomvi ngumi mkononi mwanaume hakai kwenu pale”
“Ha ha ha, wewe utakaa kama hutajali mapungufu yangu”
“yapi?”
“Napenda vibaya”
“Unajua kutumika lakini”
“Ogopa”
Wakati wanaendelea kuzungumza na sura zao kuonekana zinaelekeana, aliingia mtu mmoja mrefu ambaye alikuwa anamjua vyema kijana yule, lakini alipoingia alipomtazama yeye na kumtazama binti yule akatambua kwamba kuna shida kubwa inaweza kutokea, shida ambayo itatoa haramu katika ukoo huo.
“Hali yako, Silvesta”
“Ohh mjomba, shikamoo.”
“Marhaba. Kibua hujambo”
“Sijambo.”
“Umekuja lini Kibua”
“Ndio nimeingia leo mjomba”
“Unamjua huyo unayezungumza naye”
“Simjui”
“Naona mmekaa vibaya.Sasa sikilizeni nyie baba yenu ni mmoja mama zenu mbalimbali. Mtafanya fujo hapa zinazohitaji kondooo dume jeusi.”
Kibua akapagawa, alishawahi kuhisi kwamba hajui ndugu zake na ipo hatari ya kutembea nao.
“Huyo baba yangu yupo wapi?”
“Muulize kaka yako?”
“Wala simuulizi. Nilishawahi kumwambia mama nitakuja kutembea na ndugu yangu. Unaona sasa namuona mwanamme nampenda kumbe kaka yangu. Kwaheri Silvesta. Nalipa  gharama za supu”
Akamwangalia mjomba wake machozi yakamtoka.
“Mjomba Aksante”
“Kwa lipi mama. Unatoka nilitamani tuzungumze”
“Sina hata hamu ya kuzungumza. Berege fedha yako hii “ akatoa shilingi sita na kumpa.
”Mjomba unaweza kula supu na maandazi”
Alichukua mizigo yake baada ya kupokewa ile fedha na kuondoka.
Njiani aliifikiria sana hali yake. Safari hii aliamua kwamba mama yake atamueleza baba yake yu wapi.
Alifika nyumbani jua limekuchwa kidogo kwani alisimama Mghodo kwa muda kidogo kuongea na rafiki yake ambaye walikuwa hawajaonana kwa muda.
Regina alimpa umbea mpaka wa Severine kwamba mkewe Semie ndio tumbo tayari na kwamba amefurahi kwelikweli kwa kuondoka kwake kwani nusura amwendee kwa mganga kwa jinsi alivyokuwa anahisi anatibuliwa maisha yake. Masimulizi yalikuwa mengi lakini mwishoni walifikia hatima.Akajiondoa na kuelekea nyumbani kwao.
Alifika nyumbani kumekuchwa. Mama yake akamshangilia na kumfikisha chumbani kwake.
“Siku nyingi sana mwanangu”
“Nimerejea mama shikamoo”
Wakakumbatiana na mama akawa analia, mtoto akampangusa machozi mama yake kisha wakaenda kupumzika ndani .
“Nambie Kibua nimeandika barua nyingi nikikuomba urudi, nikawa naambiwa unasoma , sijui nini?”
“Kweli mama nilikuwa nasoma na nimemaliza nimerejea nasubiri matokeo”
“Sasa utakuwa unafanya nini?”
“Nilikuwa na hamu ya kukuona mama na nimeweza kukamilisha nilichotamani, kusoma na wakati nasubiri matokeo natumia fedha zangu za kazi kujenga nyumba nzuri ili nawe uondokane na  nyasi hizi” alisema Kibua ambaye alionekana kutabasamu.
“Kweli mwanangu?”
“Kweli mama lakini usimwambie mtu.”
“Simwambii mtu “
“Haya mama nikuulize swali?”
“Swali gani mama”
“Mama Silvesta ni nani?”
itaendelea