TAFUTA HAPA

HADITHI: Utamu wa Sukari Guru-15

KATIKA kadhia hii toleo mla mwisho tuliona jinsi Kibua alivyofika nyumbani kwa baba yake kutaka kujijua nakumjua.hakuelewana na baba yake na kumtafadhalisha Silvester kwamba anaweza kuleta posa. Hoja ambayo ilikatyaliwa na Silvester kiasi cha kumlazimisha baba yake kutoa kondoo kw atambiko na kumpeleka kwao na Kibua wakati yeye hayupo. Je Kibua alienda wapi?Na ameenda kufanya nini. Endelea kusoma

Safari ya Kibua ilikuwa ni nyumbani kwa rafiki yake waliyekorofishana, akitamani kwenda kutimiza kiapo chake cha kumvuruga Semei kwa kwenda kutembea na bwana wake tena kitandani mwake.
Ni kitu ambacho alikuwa lazima akifanye ili ajisikie raha. Semei alikuwa amemtoka si kidogo, rafiki ambaye si mwaminifu ni lazima umfanyizie ajue kwamba uaminifu ni kitu muhimu.
Mwendo wake ulikuwa wa kasi hivyo aliufika katika makazi ya akina Semei mapema zaidi . Baada ya kuhakikisha kwamba nyumba ya akina Semei na mume wake ni ile ile aliyowaacha nayo, alijisogeza mlangoni na kukuta nuko wazi na  ndani alikuwapo severine.
“Sema mvulana wa Kimbinyiko" aliita Kibua kutoka pale mlangoni , huku akiendelea kujisogeza mbele kuingia ndani sebuleni.
Severine pamoja na miaka kupita aliijua sauti ile hakuweza kuondoka kutoka pale alipokuwapo, alikuwa amechelewa,Kibua alikuwa tayari sebuleni.
“Ndio nini Severine kukataa kujibu salamu yangu?” alisema huku akimwendea moja kw amoja pale alipokuwa amepumzika katika kiti cha marimba. Akambusu.
“Hujambo laaziz…” wakati akisema aliingia mtoto wa miaka mine hivi akimuita baba yake, ambaye alisita.
“Nini Mlachuma?”
“Mama amesema wende ukamsaidie mimi nikae na mtoto”
“Mlachuma, kamwambie mama kuna mgeni nyumbani, anaitwa Kibua.” Mtoto aligeuka na kukimbia. Mtoto yule alipoondoka tu, Kibua alimpelekea macho yake severine, macho ambayo Seve huwa yanamuogopesha daima.
“Unataka nini Kibua”
“Ukitaka nisikusumbue nataka mkeo akija hapa anikute nimemaliza kazi au namaliza kazi”
“Sifanyi chochote na hunitishi”
“Utafanya mtoto mzuri.Niliapa kwamba nikirejea tena lazima Semie anikute kitandani mwake tena kwenye huba zako.”
“Kwanini unanifanyia haya mimi
“ Kiukweli nataka Semei aumie hata kama kakuzalia watoto wawili. Nataka aumie na leo namuumiza, ukitaka usiwe na matatizo ukubali tu mkeo leo aumie au la na wewe utaumia”
Akamtazama bila kusema kitu.
“Twende chumbani laaziz” akasema. Kama mbwa kwa chatu, alimfuata chumbani.
Uko  ndani kulianzishwa mchakato wa kubaka na Kibua aliumudu, severine baada ya muda akaona ahh ishakuwa taabu mwacha ashirikiane naye kumaliza lile zoigo manake tayari alishaadhibiwa.
Semei alipofika sebule akakosa watu machale yakamcheza, akamwagiza mtoto wake kwa bibi, akapitiliza kwenda chumbani.Alichokuwa akikifanya Kibua nusura kimtoe roho, aliegemea ukuta macho yakawa yamemtoka.
“Kibua, mbona unataka kuniua” alisema kwa kulia, huku akiwa anataka kwenda kiugomvi.
Hakumjibu kwanza, alizungusha mpaka Severine akagumia, gumio ambalo lilimuumiza kwelikweli semei, kwani halikuwa na uchungu lilijaa kila kiwango cha TBS katika kufanya mapenzi.
Kibua, alipoona Seve kamaliza akajiachia taratibu na bila kupepesa alimfuata Semei .
“Mwache mwenzio apumzike wewe. Unamtesa mtoto wa mwanamke mwenzako kwa sababu gani hasa? uzazi ? nicheke Kibua. Kaa hapohapo uone wenzako tunavyojua.”  Akarejea kwa mahaba kifuani mwa Seve ambaye alikuwa muda ule hajitambui.Semei moyo ulipaa, ukaondoka,hakujua hata kumetokea nini na  alipoamka, alimuona mama yake na mumewe na Kibua.
“Afadhali umeamka” alisema mama mtu.
Semei alianza kulia kidogo kidogo kisha kwa nguvu mpaka mama yake akaingilia kati baada ya kugundua alikuwa haoti na wala hayuko kisimani katika usingizi wa mchana ilikuwa kweli na tena nyumbani kwake.
“Mimi nimesimuliwa na mumeo hapa ugomvi wa wewe na Kibua.Amesema ulimfanyia haya aliyokuja kukufanyia. Amekuja kulipiza kisasi kwa kuwa alisema. Ni upuuzi kwelikweli lakini nifanyeje. Alitaka kuondoka lakini, nilimsihi asiondoke mpaka hapo utakapoamka mumalizane manake hamwezi kuwa hivi.”
“Mama sijui Kibua kakueleza nini, mimi nisemeje?”
“Huna chochote  cha kusema Mwanangu. Huna cha kusema”
“Kwanini mama”
“Kwa sababu ulichokifanya wewe ni cha kishenzi na mwenzio alijiapiza kwa miungu na alisema alikuwa na haki ya kulipiza ili ikuume halafu ujuwe ni kwanini hana raha tangu umemrusha ndege wake angani”
“Mama mimi nitaendelea hivi na Kibua mpaka lini”
“Amesema yataisha kama utasema kitakachomfurahisha”
“Mimi nitamfurahisha? Semei mimi, mama humjui Kibua”
“Kwao watu wa milunga, ni shida kidogo lakini hebu mwombe samahani”
“Nishamwomba samahani sana mama”
“Ha ha ha ,hukusema kwa nia ya dhati  hasa kutokana na ulikomchafua sana”
“Mimi sikumchafua mama ni tabia yake”
“Anasema kwa kuwa mlikuwa marafiki alikuambia kila kitu na ukatembea na shemeji zako wote na yeye haoni sababu kwanini asitembee na baba Chuma.”
“Mimi ndio nilikuwa namkosea kwa sababu alikuwa anafanya mzaha na nikaona wala hajali”
“Mwenzako anasemaje, eti Kibua unasemaje”
“Aliniambia mimi mchawi. Unakuaje mchawi mama! Aliniambia mimi nachukua kila kitu kizuri.Nachukuaje kila kitu kizuri.Ahaa nimekuja kumchukua Seve kwa sababu ambazo yeye anazijua si tunachangia mabwana!” alisema kwa bashasha
“Nambie Semei umemsikia mwenzako?”
“Seve anasemaje”
“Hii ni mara ya tatu huwa nashindwa la kufanya ninapokutana na Kibua. Utadhani ana sumaku Fulani nisiyoweza kuirudisha nguvu zake.Kama leo alisema wazi nisipokuwa huru nikamchelewesha kwa namna yoyote kufanikiwa katika haja zake nitarajie kuumia mimi au Semmy sasa nikaona wacha tu.Niliposhindwa kushiriki akajiapiza kwamba hakuna hapa kufanya masikhara ataniumiza. Mama nifanye nini?nimemuuliza mara nyingi Semmy arekebishe mambo yake na Kibua, lakini yeye anasema tunajua wenyewe?Wanajuana nini? Anajua leo Kibua kasema nini kingine? Anataka mtoto ili niwe nafika kwake anitumie anavyotaka”
“Kibua.. “ Semei alinyanyuka ghafla akaenda kupiga magoti kwake:”Nisamehe rafiki , nisamehe, nitaenda wapi mimi na watoto wawili?Akija huko najua hatarudi tena Kimbinyiko.Nimeona ulichofanya ambacho siwezi kukifanya. Una mizuka yako, na kila nilichokuwa naambiwa kipo, mimi nifanyeje ukinichukulia Seve. Mwanamke mwenzangu wewe usinitese nina watoto”
“Sasa Semie nikuulize. Kama leo nimepata mimba unafanyaje?”
“ Haiwezekani ushike mimba. “
“Sasa nikikuambia kwamba mzunguko wa leo ni wa ujauzito utasemaje?”
“Mimi nitakufa Semie,mimi nitakufa Semie” alisema huku machozi yakimmwagika, alikuwa kila mahari anachachawashwa, anawashwa alikosa raha.
 “Sikia Semie.Najua huwezi kumrejesha tena mwali wangu, ameshaoa hawezi kubaki mpweke hakuzoea na sikumzoesha kukaa bila mke. Na siwezi kukutoa wewe kwa Seve, ushazaa najua umuhimu wa baba ingawa ulikuwa unanicheka kila siku. Leo nilienda kuonana na baba yangu kwa mara ya kwanza. Nimefurahi sana. Kwa furaha yangu nakuachia Seve.”
“Ndio kusema unamjua baba yako?”
“Mh na kaka yangu pia.Sikia Semei, nimekusamehe wala sitarudia tena kukuvuruga nilitaka tu uone na uone ubaya wa kuharibu mambo ya watu.Unaweza kukutana na mtu ambaye hajali kitu. Siku hizi najali sana. Usijali ukipata nafasi  njoo nyumbani tuongee, lakini baadae sana.”
“Baadae manake nini?”
“Nitakuwa bize sana . leo nimeshusha kila kitu katika moyo wangu na mwili wangu. Naanza upya. Kwa muda kidogo nataka kumalizana na baba kisha huyooo narejea tena mjini na mahangaiko yangu labda nitampata  mtu mwingine wa kunifanya nitulie”
“Hutamfuata tena Seve?”
“Unataka nimfuate?Muulize kama ana ubavu wa kunizuia?Ninakoza mimi  wewe, hii sukari guru ikitolewa kwa kipimo haikinai na mumeo ana dozi ya kipimo ndio maana  ulipofika hakuwa anaweza kumudu chochote ameduwaa kama balagaja ( mjusi) aliyebanwa kwenye mlango.”
“Unajua kwanini sikupendi? Kwa sababu kuna siku Seve alipiga kelele akikutaja jina lako, ndio siku pekee nilimuona uso wake umechangamka na leo niliukuta vile vile. Nikasema duhh jamaa anatabasamu katika usingizi.Sikumweleza leo niliona tabasamu “nikazimia.
“Usipate munkari mwingine.Hii jua tu imekwisha. Mama naomba maji”
Mama yake Semei alienda katika mtungi akatwaa maji kwenye kata, akatulia akayanywa, kisha akampelekea kata ile yenye maji.
Akachukua maji akasema maneno Fulani, akaita babu zake, akamtemea maji usoni semei, akanywa na kumpa anywe.
“Semei tumemalizana kimila, sina ugomvi nawe, kaa na mumeo bibie”
Akamkabidhi kata mama yake Semei na bila kumwangalia Seve, Kibua akatoka ndani ya nyumba ile kimya kimya,Kibua alitaka Semie amkute anafanya mapenzi aumie na  ndicho kilichotokea hivyo amekamilisha maapizo yake na sasa anastahili kuondoka wala hakuwa na sababu ya kutazama  nyuma.
Itaendelea