Kibua baada ya kumaliza kazi zake na kuraiwa sana na Chioma anaenda zake kujipumzisha. Tulimaliza kwa kuona kwamba anagongewa hodi chumbani kwake usiku. Je ni nani aliyekuwa anagonga hodi ni mtoto Chioma akiendeleza hoja zake au baba mwenye nyumba.
Pamoja na kwamba alikuwa usingizini, Kibua aliweza kupambanua ugongaji ule, akanyanyuka bila kujivika shuka akiwa kama vile alivyozaliwa na kwenda kufungua mlango.
"Karibu baba Chioma"
"Aksante" alipitiliza hadi kitandani.
"Nini tena baba Chioma"
"Unaondoka, nimeona tuagane"
"Mimi naenda nyumbani tu baba Chioma, nitarejea"
"Nitakumisi sana."
"Yaani kwa miezi mitatu tu"
"Unaiona midogo"
"Unaendekeza baba Chioma una mke wewe"
"Anajua au asijue, lakini nadhani anajua kwamba huwa unanisaidia"
"Unaweza kuwa umemsikia vibaya, wakati tunaagana"
"Sijawasikia vibaya, kuna siku nilitoboa siri"
"Tangu umetoboa siri ni miaka mingapi"
"Miwili sasa"
"Nini kilikufanya unitafutie mtoto wa watu kifo?"
"Kifo?"
"Ndio!"
"Hapana, sijui ilikuwaje lakini nakumbuka alicha kuzungusha akasema wewe unatembea na
Kibua,nikakanusha, akaniambia ana ushahidi wa kutosha kwa sababu hata namna ya ufanyaji mapenzi
nimebadilisha sana, nina spidi na ninamjali"
"Hilo tu!" akakumbuka jinsi baba mwenye nyumba huyo siku za kwanza alivyokuwa na haraka, mpaka akamfundisha kutulia akimtafadhalisha kwamba kama kaamua kula haramu basi ale kwa kujinafasi na si kwa wizi. Akamfundisha namna ya kufanya mapenzi, namna inavyotakiwa kuwa wawili wanapotaka kustarehe kwelikweli na kwa namna ilivyokuwa aliweza kumbadili kwelikweli kutoka katika kungonoana hadi kufikia kufanya mapenzi.
"Si hilo tu aliniambia anadhani anaweza kuishi na wewe, ila suala ni nini kitatokea kama wewe utapata mimba na shule hujamaliza."
"Na wewe ukasema"
"Nilikaa kimya, utapataje mimba na mimi sitembei nawe?"
"Ehee baba Chioma nambie kweli"
"Nakwambia "
"Richard!" kwa mara ya kwanza alimuita kwa ukali kwa kumtaja jina lake.
"Basi mama nitakuambia ukweli"
"Wala sitaki ukweli wako nipatie tiketi yangu."
"Utaenda na basi la reli"
"Wewe nipe tiketi kwanza."
Alitoa tiketi ile ya daraja la kwanza katika basi la shirika la reli kutoka katika mifuko ya pajama aliyoivaa na kumpatia.Akaipokea na kuipiga busu.
"Aksante"
"Mbona unaenda mlangoni"
"Nikufungulie mlango tutaonana asubuhi"
"Sio hivyo Kibua"
"Nikianza kuwaita watu kwa majina yao halisi, huwa sina tabia njema. Maana yake Baba Chioma ukalale kwako"
"Na hapa kwangu"
"Kweli kabisa na kitanda chako, lakini mwili huu si wako hujaulipia mahari. Umewaona wazazi wangu
Wewe?"
Alimshushua.
"Mbona leo umekuwa hivyo?"
"Hatujaandaana kwa siku ya leo"
"Unataka kwenda kazini baba Chioma kesho au hutaki" alimuuliza swali ambalo huwa analiogopa.
"Ninataka kwenda kazini"
"Basi we nenda ukalale"
"Unaniona sina nguvu nini?"
"Hapana leo nina nguvu sana, tutaumizana"
"Tuone"
"Karibu." akaenda kufunga mlango.Akarejea kitandani.Wakavuta shuka, kulala. haikupita muda shuka ile ilionekana kuleta ghasia, feni ndio iliyohitajika.Richard alikuwa Richard Kweli na Kibua alikuwa kibua kweli.Richard alitamani ardhi ipasuke immeze jinsi alivyopelekwa dunia nyingine.
Saa kumi na moja Chioma pombe ilikuwa imemtoka, akaamua kwenda kumgongea msaidizi wao wazungumze na safari hii akifanya masikhara , alijisemea moyoni atambaka.
Kibua alishtuliwa na sauti ya kugongwa kwa mlango kwa vurugu, akamtazama baba Chioma alivyolala akamfunika na kwenda kufungua mlango na khanga moja nyepesi.
"Sema Chioma" alifungua mlango kidogo kwa komeo la mnyororo.
"Nataka kuzungumza nawe"
"Usiku Chioma haiwezekani"
"kwanini?"
"Kwa sababu baba yako amelala utamuamsha"
“Atasikiaje sauti na yeye yuko nyumba kubwa?”
“Hapana mwanangu baba yako amelala ”alisema kwa sauti ya kimama kabisa.Chioma akachoka kabisa.Akachoka sana, akavuta mwayo akasema:
"Baba yangu? Haiwezekani"
"Haya karibu"
Akamfungulia mlango kidogo,akaingia chumbani na kupigwa na butwaa jinsi baba yake alivyolala kwa tabasamu, hakuwa na sura yenye stress ambayo amekuwa na kawaida ya kukutana nayo.Akageuza uso akatoka ndani ya chumba, Kibua akamfuata.
"Mbona umefadhaika?"
"It is not fair"
"Nani alikuambia kwamba dunia ipo fair? Nani alikuambia?"
"Baba anawezaje kutembea nawe"
"Mimi ni mwanamke, si mtoto, Chioma"
"Kwa hiyo?"
"Mimi ni mama yako, je bado una hamu ya kuzuru alipozuru baba yako? Kumbuka sisi si wanyama kwamba kijana ndiye mwenye mamplaka ya kutawala."
"Unanikumbusha ustaarabu ambao baba yangu hana"
"Ndivyo inavyokuwa kama unaweza kufikiri kama mwanaume, lakini ukifikiri kama mke utakuwa na mawazo mabaya dhidi ya baba yako"
"Unampenda au"
"Unataka kujua ukweli?"
"Unadhani sitaki kuujua?"
"Mara nyingi ukimchunguza bata anakula nini huwezi kumla.Siwezi kukujibu kitu chochote kile.Lakini kama unadhani kwamba kumsaidia baba yako nataka urithi wako sahau kabisa, siuhitaji. Mama yako analijua hilo wala usijisumbue" alisema Kibua.
"Mimi nashangaa kabisa"
"Hapa sio feri ambapo meli za tani nyingi zinaelea halafu ukitumbukiza shilingi inapotea."
"Haya Kibua, siungi mkono shauri hilo"
"Usiku mwema"
Waliagana na kila mtu akarejea kwake. Kibua aliingia chumbani na kumwamsha mzee kwani safari ya kwenda nyumbani ilikuwa imetimia.
"Hatuwezi kupata chai kidogo"
"Ukishiba, hutanisindikiza.Ugali uliokula unakutosha kabisa kwani hadi sasa umevimbiwa."
Akacheka akachukua taulo akatoka, akapita mezani akamkuta Chioma anatengeneza juisi kuinywa.
"Karibu baba,mbona usiku sana"
"Nikuulize wewe unayetengeneza juisi saa hizi inakuaje?"
"Nimechoka sana kimawazo"
"Umechoka nini?"
"Kama hivi unavyotoka kwa msaidizi wa ndani"
"Nimeenda kumpa tiketi yake nisije nikasahau"
"Tiketi kwani vipi"
"Alimuomba mama yako akapumzike na mama aliafiki"
"Muda gani?"
"Zaidi ya miezi mitatu"
"Na wewe utakuwa unafanya nini?"
"kwenda kazini si ndio kazi yangu"
"Sikia baba wewe unafanya mapenzi na Kibua, kwanini?"
"Nani amekuambia"
"Nimekukuta ukiwa umelala kitandani"
"Ohh nawewe ulifuata nini?"
"Nilikuwa nataka kumuuliza kama ana nafasi nami"
" Usiku wa manane?"
"Kwani kuna tatizo"
"Hajawahi kukuambia kwamba yeye ni mama yako?"
"Ndio maana nilitaka kwenda kumuuliza?"
"Unampenda?"
"Ndio"
"Nafikiri, bado una nafasi lakini je unaweza kumuoa mama yako?"
"Siwezi!"
"Kwanini unadhani?"
“Kwa sababu ni mama yangu"
"Sawa kabisa. Na mwanamke anayetembea na baba yako ni mama yako.Keep distance son."
Baba aliendelea chumbani kwake akaoga na baada ya kuoga na kuvaa, gari ikawa inapiga honi. Kibua alitoka na begi lake lililosheheni mambo mbalimbali na fedha taslimu zinazotosha kujenga nyumba ya tofali la kuchoma.
Baba Chioma, Richard alitoka na kwenda kusaidia begi na kumfikisha kwenye gari, kabla ya yeye mwenyewe kuingia na kumfikisha relwe tayari kuabiria kwenda mkoani.
Baba Chioma alipohakikisha kwamba Kibua amepanda basi alirejea kwenye gari na kuondoka huku akiwa na mawazo juu ya mtoto shoo, Kibua.
Alikuwa amekua na kufanana kabisa katika kufanya mambo yake na mke wake mtarajiwa Mariana. Walifanana katika kila kitu mpaka urefu wao haikuwa rahisi kumuacha kuondoka.
Akalifikiria wazo la mama Chioma la kumuoa binti Yule, baada ya kuona kwamba yeye hawezi kuzaa tena na kazi zimemzidi kiasi ya kwamba hata akirudi nyumbani hujilalia tu, akaona hawezi kufanya hivyo kwani tayari ana matatizo ya kutosha na mtoto wake ambaye alionekana wazi anataka kuishi na kibua.
Wakati yeye anawaza hilo Kibua yeye mawazo ya kutulia kwa mwanaume halikuwepo alishachagua njia, njia ya kumpekleka kwingine kabisa,njia ya kujilimbikizia maarifa kwa kusoma na kuajiriwa.
itaendelea