TAFUTA HAPA

*HIRIZI YA MAHABA* *SEHEMU YA SITA*


*SEHEMU YA SITA*
Kabla sauti ile haijafika mlango wa chumba tulichokuwepo, niliruka kutoka pale nilipokuwa nimelala. Nikanyanyua shati langu na kuanza kuvaa haraka haraka. Nikawa nimesimama pembeni. Mwantumu alikua amehamaki sana. Akakosa cha kufanya kwa muda huu mchache ambao tulijaaliwa kabla ya kufumwa rasmi.
“Hee Afande vipi tena?! Mbona sielewi??!! Alihamaki afande mmoja baada ya kutukuta pale, ambaye baadae nilimtambua kwa jina la Zassor. Muda huu Mwantumu alikua amesimama, akiwa anaiweka sawa sketi yake, huku ameshikilia shati lake la sare ya askari kwa mkono wa kushoto. Sehemu ya kifuani pakiwa wazi huku maziwa yakiwa yameshikiliwa na sidiria ya rangi ya pink.
Afande Zassor alisogelea hadi pale tulipokuwa, huku akiachia mdomo wake wazi. Haamini anachokiona. Mimi pale nilipokuwa dua zangu zote zilikuwa nimezielekeza kwa Mungu kuomba kitu kimoja tu.. Niliomba Afande Zassor asije akaona chupi ya Mwantumu iliyokuwa pembeni mwa kile kigodoro pale chini.
Lakini nahisi dua zangu hazikupokelewa, kwani katika kupitapita na kutuchunguza vizuri, Afande Zassor alifanikiwa kuikanyaga ile chupi ya Mwantumu.. Akazama na kuiokota na kuanza kuiangalia kwa umakini. Akaigusa sehemu ya mbele, ilionekana kama imelowa ingawa si sana. Mwantumu baada ya kuona hivi, akaruka na kuikwapua ile chupi kutoka kwa Afande Zassor.
“Siwezi kuamini Afande kama wewe ndo umefanya mambo haya” Zassor aliongea kisha akanigeukia mimi. Akanishika mkono na kunivuta kuelekea nje..
“Twende huku wewe falaa...”
Akanikokota mpaka nje kabisa ya kituo. Nilishangazwa na hali ya Afande Zassor baada ya kufika nje ya kile kituo. Ni tofauti na alivyokuwa pale ndani. Aliachia tabasamu huku akinifutafuta vumbi kama vile mtu anayenithamini sana. Tofauti na hapo awali.
Nje kulishapambazuka ingawa bado ilikuwa ni saa 11 kasoro alfajiri. Kama yalivyo maeneo mengi ya mikoa ya Pwani, jua huwahi sana kuchomoza.
“Kaka, hebu nambie, umewezaje kumla yule Mwantumu? Yaani siamini ujue, umewezaje wezaje?” aliniuliza Zassor tukiwa pale nje. Baada ya swali hili, nikaona ndio nafasi pekee ya mimi kutoka pale selo kwa kesi ile iliyonikabili. Cha kufanya ni kumueleza tu Afande Zassor ukweli, nikiamini ni lazima atanisaidia tu.
“Hakuna jipya kaka, ni yeye mwenyewe tu kaka” Nilimjibu jibu jepesi ili kuona kama kweli ni muhitaji wa kiasi kikubwa ama laa.
“Hapana kaka, yule demu mimi nimeshamuhangaikia sana, na bado alinitosa, na tupo wengi.. Yaani anajisikia sana” Aliweka nukta ndogo Afande Zassor kisha akaendelea..
“Sasa huwezi kuniambia eti amekutamani yeye mwenyewe, si kweli!! Maana ana dharau kwa sisi askari wenzake halafu akutake wewe Mhalifu uliye mahabusu? Wewe nambie tu, umetumia nini kumnasa, basi!!” Hapa sasa nikapata kumsoma vizuri Zassor na kumuona kweli alikuwa na shida haswa..
“Afande, sio siri, mimi natumia Ndere, kuwanasa hawa warembo”.
“Ndere?! Ni nini hiyo kaka? Sijakupata”
“Ni uganga flani hivi, unapewa hirizi, ukiwa nayo hiyo hakuna mwanamke anaweza kukukataa..!! Na sio tu kutongoza na kutokataliwa, bali unakua na mvuto kwa kila mwanamke unayepita mbele yake”. Maelezo haya ndiyo yaliyommaliza Zassor, akapata shauku ya kutaka kujua anaipataje Ndere.
“Sasa, mi naipataje kaka, daah maana wewe kwa uliyoyafanya jana usiku, tayari nshakuogopa”.
“Namna pekee ya kuipata ni mimi kukupeleka kwa mganga wangu.. Maana hata nikikuelekeza hatokufanyia hadi twende wote., na hii kesi ilivyo nzito unafikiri nitatoka leo kweli hapa?” Nilichomekea kwenye kesi yangu kuona Zassor atasemaje.
“Kaka, hapa hamna kesi wala nini, tena twende ukachukue mizigo yako uondoke mapema, mimi nitajua nasemaje..”. Sikuongeza neno, tukarudi ndani ya kituo, Afande Zassor akanikabidhi vitu vyangu na kunipa namba yake ya simu kisha akaniruhusu niondoke haraka pale kituoni.
Wakati haya yote yanafanyika sikufanikiwa kumuona Mwantumu tena. Nikahisi atakuwa amebaki kwenye kile kichumba tulipofanyia yetu.
Nikachomoka kwa kasi pale kituoni. Nikaona pikipiki ikitokea upande wangu wa kulia kunifuata. Nikaongeza spidi zaidi kuelekea njia ya nyumbani kwangu nilikopangisha. Nikasikia sauti ikiita “Mjomba unaenda?” Ndipo nikashusha pumzi za uoga na kujibu, “Naenda kaka”. Kisha nikapanda bodaboda ile huku nikimuelekeza wapi pa kumpeleka.
Nikiwa juu ya ile pikipiki ndipo nikakumbuka kumpigia Mjomba Mwinyi.
“Ndo najiandaa kuja huko kituoni mjomba” Alisema Mjomba Mwinyi mara baada ya kupokea simu yangu.
“Usije tena Mjomba, nimeshatoka pale kituoni”.
“Duuuh... Wamekuruhusuje hao jamaa?, kwahiyo unaelekea wapi saa hizi?” aliuliza kwa shauku mjomba.
“Naelekea kwangu, kupumzika” Nilijibu swali lake la pili nikijifanya kama sijasikia lile swali lake la kwanza.
“Ok, nitakuja huko basi kukusalimia nikishakunywa chai”. Aliongea mjomba baada ya kuona hakuna tena umuhimu wa kuwahi kutoka.
“Hapana mjomba, wala usije, pumzika tu.. Kama kutakua na tatizo nitakwambia”. Niliona hakukuwa na haja ya kumsumbua mjomba tena.
“Haya bwana, maisha yako unayajua mwenyewe wewe” aliongea mjomba na kukata simu.
Nilifika nyumbani na kujitupa kitandani nikitafakari mawili matatu. Hazikupita hata dakika tatu simu yangu ikaita. Nikaangalia mpigaji alikuwa Rahel, nikapokea.
“Baby mume wangu kasafiri alfajiri hii, niko njiani nakuja kwako”. Rahel hakutaka hata kunisalimia. Na kabla sijajibu chochote alishakata simu. Nikatoka na kwenda kuoga kisha nikakiweka sawa chumba changu. Nikatoa udi ambao alinipatia mganga wangu, nikachoma na kubadilisha harufu ya kile chumba. Nikakaa na kumsubiri Rahel.
Zilipita dakika chache nikasikia mlio wa sms katika simu yangu. Kabla sijafungua kuisoma mlango uligongwa. Nikainuka na kwenda kufungua mlango, naam alikuwa Rahel, nikamkaribisha na kuingia ndani huku ameshikilia kiuno changu. Tulitembea kama walevi wa gongo.
Baada ya kufika chumbani, Rahel hakuuliza chochote, wala kusema neno lolote, alitoa nguo zake zote na kubaki kama alivyozaliwa. Kisha akajitupa kitandani. Nikajikuta nasimamisha jogoo wangu ghafla sana. Nami nikaanza kuziporomosha pamba zangu kwa kasi.
Wakati naendelea na zoezi hili, mlio wa sms ulisikika katika simu yangu.. Hapa ndo nikakumbuka kuwa kuna sms ambayo sijaisoma. Nikaamua kuzisoma zote. Nikianzia na hii ya pili ambayo ilisomeka 'luv u xn' ilitoka kwa Jacq. Nikaipotezea, nikafungua ile nyingine ya kwanza ambayo ilisomeka *“Baby, pole sana kwa tukio la jana, ila yule askari wa kike uliyekutana nae hapo kituoni ni dadaangu, ameniambia umeshatoka kituoni, ila wazazi hawajui ndo wanajiandaa kuja huko.. Na mimi nasubiri watoke tu nije kwako my baby”*. Nikashusha pumzi ndefu na kuhisi kuishiwa na nguvu.
***********************************
*Usikose sehemu ya Saba*