TAFUTA HAPA

*HIRIZI YA MAHABA* *SEHEMU YA SABA*


*SEHEMU YA SABA*
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

Jumbe zile za Jacq zilinichanganya sana. Kwanza mara ya mwisho kuwasiliana na mimi alionesha kuua uhusiano wetu, sasa kwanini anarudi ghafla namna hii?.
Pia, itakuwaje kama Mwantumu ni dada yake? Na wameongea nini kuhusu mimi? Hili liliniumiza kichwa zaidi maana Mwantumu alikuwa ameingia moja kwa moja moyoni mwangu, nilianza kujihisi kumpenda kuliko wanawake wengine wote ambao nilikuwa nikitembea nao.
“Baby vipi kwani?” aliniuliza Rahel baada ya kuniona nikiwa nimezubaa baada ya kusoma ujumbe ule kwenye simu yangu.
“Aaaaah! Matatizo tu ya kidunia” nilimjibu kihuni huku nikijirudisha pale kitandani na kujaribu kujichangamsha ili kumfanya aachane na maswali ambayo alitaka kuyaanzisha. Lakini kiukweli nilikuwa nimetoka mchezoni tayari, hata sikuwa na mzuka wa kuendeleza ambacho Rahel alikuwa akikitaka, ila sikutaka kumuumiza, hivyo nikaendelea kuwepo pale nikishirikiana naye kibishi tu.
“Baby una matatizo gani kwani?” Rahel alisita kidogo na kurudia swali lake, nadhani hii ilitokana na kuniona nikicheza chini ya kiwango changu alichokizoea. Maana tayari alikwishanigusa maeneo yangu ambayo anapoyagusaga huwa ninasisimka vibaya. Ila leo hata jogoo wangu hakusimama.
Badala ya kujibu swali lake mimi nilimkamata na kumvutia kwangu kisha nikaanza kutembeza ulimi wangu mwilini mwake, mchezo ambao alikuwa akiupenda sana na mara zote ninapofanya hivyo Rahel hucheka kwa sauti ya juu sana akisisimka vibaya mno. Nilijua nikifanya hivyo hatokuwa na muda wa kuona kama sikuwa sawa na kweli nikafanikiwa.
Michezo ya hapa na pale ikaendelea na hatimaye nikaona kuwa Rahel alikuwa tayari kumalizia sehemu ya mchezo iliyobakia. Hivyo nikaamua kukamilisha. Niliendelea kuwepo juu ya kifua cha Rahel kwa kama dakika 45 bila kushusha wazungu hata mara moja wakati Rahel alikuwa ameshusha kama mara tatu hivi.
Hapa akapata tena nafasi ya kugundua kuwa sikuwa sawa, nikaona akinichomoa kutoka kifuani kwake...
“Hakuna maana ya jambo hili kuendelea kama hauenjoy, mimi sitaki kukutumia kama chombo cha ngono, nataka sote tufurahi” alisema Rahel huku akijifunika shuka kuonesha kuwa mchezo ule ulikuwa umesitishwa.
“Najua unajua kuwa ni wajibu wangu kukuridhisha na siku zote nafanya hivyo, naomba nivumilie kwa leo” niliamua kujisalimisha kwa kumwambia maneno ambayo nilijua lazima yamuingie, na kweli nikafanikiwa.
“Sawa nimekuelewa, lakini ningependa pia kuja tatizo ni nini” alisema Rahel.
“Nina matatizo kidogo ya kifamilia, ila nina uwezo wa kuyamudu, hata usijali”. Rahel akaamua kuwa mpole, tukabaki tukiongea hili na lile kama kwa nusu saa tu kisha akaniaga na kuniachia elfu hamsini kisha akaondoka akinitaka nimtafute nikiwa sawa.
“Hatujamalizana, ukiwa sawa utanitafuta” alisema Rahel akichukua mkoba wake na kutoka.

Mara tu baada ya Rahel kutoka, nikachukua simu yangu haraka na kupiga namba ya Jacq, simu haikuita sana ikawa imepokelewa..
“Hallo mpenzi” ndivyo alivyopokea simu Jacq, lengo la kumpigia nilitaka kujua kuhusu ukweli wa taarifa za Mwantumu kuwa dada yake na kutaka kufahamu kama ni kweli je wameongea nini juu yangu.
“Utanitia matatizoni wewe mtoto, angalau tutulie kidogo hii kesi ipite” nilimwambia Jacq ambae ilionekana kuona kuwa nilikuwa namwambia kitu kigumu mno.
“Mi siwezi bwana, kama vipi tutoroke tukaishi mbali ambapo hatutopata usumbufu wa familia yangu”. Alishauri Jacq bila kujua kuwa tayari nilikuwa nimetosheka naye na nilitaka penzi lile life muda wowote.
“Hapo ndipo ninapogombana na wewe, kila siku nakwambia ujifunze kuwa mwanamke wa kujitegemea, unadhani utawezaje kujitegemea ukiitupa elimu? Siku moja tutaishi kama tunavyotaka ila kwa sasa vumilia” nilijifanya kuleta busara huku nikitumia ile sauti yangu ya ukali kidogo ambayo huwa naitumia kwa mwanamke ambaye najiona kuwa nina uwezo wa kumtawala na sitaki abishane na kauli yangu.
“Sawa, mi nitavumilia ila kuonana na wewe ni lazima, sitoweza kusitisha” aliongea Jacq kwa sauti ya kudeka.
“Mwantumu ni dada yako kivipi? Mbona hukuwahi kuniambia habari zake kabla?” sasa nikauliza swali ambalo ndilo lilikuwa lengo langu hasa la kupiga simu. Nikiwa nimejua kuwa Jacq hakufahamu hata kidogo juu ya jambo nililofanya na Mwantumu kule kituoni maana kutokana na wivu alionao juu yangu tusingeongea vizuri kama angelijua jambo lile.
“Dada Mwantumu ni mtoto wa shangazi yangu yule wa Donge, amenigombeza sana mwenzio akanambia nataka kukusababishia ufungwe miaka 30” alielezea kwa kifupi Jacq.
“halafu?” nikauliza kutaka kujua zaidi.
“Akasema ataongea na mama ili hili jambo lisiende mahakamani ila akasema niachane kabisa na wewe na kama nikiendelea safari hii atanikamata yeye mwenyewe anipeleke kituoni” alielezea vizuri Jacq, nikaona hakuna ambacho kimeharibika.
“Usihofu, Mwantumu ni mtu mzuri tu naamini atanisaidia, hebu nitumie namba yake kwanza tupange mkakati wa kulimaiza hili jambo” nikaamua kumtumia Jacq kupata namba maana sikupata nafasi ya kuichukua wakati natoka kituoni, Jacq akakubali na kunitumia mara baada ya kukata simu.
“Haloo” iliita sauti ya Mwantumu baada kupokea simu.
“Haloo, nambie” nami nikitikia.
“poa, nani mwenzangu?” Mwantumu akajaribu kunifahamu nami nikajitambulisha..
“Jay anaongea”.
“Aisee, nilikuwa nawaza nitakupataje Jay, uko wapi?” aliuliza Mwantumu nikamwambia nilipoa akanitaka tuonane haraka.

Nilifika kwenye bar moja maarufu katikati ya mji ambapo Mwantumu alitaka tukutane hapo. Nikatoa simu na kumpigia kumwambia kuwa nilikuwa nimefika tayari, kumbe yeye alifika kabla yangu. Akanielekeza alipokaa nami nikaenda kujiunga naye, akaniagizia kinywaji na maongezi yakaanza.
“Aisee nimejaribu sana kumsihi mama yake Jacq kutopeleka kesi hii mahakamani ila imekuwa ngumu, sijui tufanyeje?” alinielezea Mwantumu habari ambazo zilinishtua.
“Mimi nategemea wewe unambie tunafanyaje maana mimi hata sijui nifanyeje” nilijibu.
“Cha kufanya itabidi ukimbie mji kwa muda mpaka hapo hali itakapokuwa shwari” alinipa maelezo ambayo sikuwa tayari kuyatekeleza, kabla sijajibu chochote simu yangu ikaita, nikaitoa na kukuta alikuwa ni afande Zassor.
“Haloo, mida ya saa 9 uje kituoni na mama yake Jacq atakuwepo tulizungumze hili jambo liishe” alinielekeza afande Zassor na kukata simu. Nikamjuza Mwantumu juu ya ujumbe ule....
“Hakuna ambacho kitaendelea, hawezi kuelewa kitu mama Jacq, mimi nimeongea nae sana” alisema Mwantumu nami nikamtaka asikate tamaa, tuitikie tu ule wito tuone nini kitatokea.
Saa yangu ilionesha kuwa ilikuwa saa saba na dakika kadhaa, nikaamua kurudi nyumbani kujiweka sawa kwa ajili ya kwenda kituoni saa 9. Nikaamua kumpigia mjomba Mwinyi na kumtaka ahudhurie pia pengine busara zake zingeweza kunitoa kwenye mkwamo ule. mjomba Mwinyi akakubali kuhudhuria.
Saa 9 na dakika 12 nilifika kituoni nikiambatana na mjomba, tukakuta tayari mama Jacq alikuwepo kituoni. Maongezi yakaanza, afande Zassor na Mwantumu wakiwa wasemaji wakuu wakimsihi mama Jacq kupunguza hasira na kunionea huruma kwani tayari nilikuwa nimelijua kosa langu na kuahidi kutorudia.
“Mna uhakika kuwa hatorudia?” aliuliza mama Jacq kwa ukali na wote wakajibu kuwa wana uhakika. Mara akachukua mkoba wake na kutoa simu ambayo niliitambua sana, ilikuwa simu ya Jacq. Akaonesha sms ambazo Jacq alinitumia kisha akaonesha historia ya simu ambayo nilimpigia Jacq tukaongea kwa dakika 8.
“Huyu hajakoma na hawezi kukoma mpaka nimkomeshe” alisema mama Jacq. Macho ya watu wote yakarudi kwangu, ilikuwa ni kama wananilaumu kwa kuyakoroga zaidi.
“Ni kweli nilimpigia Jacq ila ilikuwa ni kwa lengo la kumkanya kunitafuta” nilijitetea.
“Kumkanya kukutafuta sio jambo la kuchukua dakika 8, jamani naombeni huyu mtu afikishwe mahakamani kesho” alihitimisha mama Jacq na kuondoka bila kuaga.

Mara baada ya mama Jacq kuondoka, nikamuomba Mwantumu anipatie namba yake, wote wakataka kujua nikuwa na nia gani, nikawataka waniamini na Mwantumu akanipa namba.
“Haloo samahani mama tunaweza kuonana?” niliuliza baada ya mama Jacq kupokea.

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
*Usikose sehemu ya 8*