*SEHEMU YA NANE*
“Nani wewe?” Alijibu Mama Jacq na hapo ndio nikakumbuka kuwa sijajitambulisha wala kumsalimia.
“Mimi Jay” Nilijibu kwa ufupi.
“Unataka kuongea nini na mimi wewe mshenzi?” Ndilo swali lililofuata baada ya Mama Jacq kunitambua.
“Samahani mama, naomba tafaadhali tuonane”. Nilisisitiza, nikiwa najua nikionana nae na tukiangaliana machoni kwa dakika kadhaa, kesi itaisha tu.
“Tukutane hapo Kibarua Restaurant dakika kumi kutoka sasa”. Sikuwa na cha kuongeza, nikakata simu na kuagana na Mwantumu pamoja na Afande Zassor na safari ya kuelekea Stendi ya Zamani ambapo Kibarua Restaurant ilipatikana, ikaanza.
Nikafika ndani ya dakika chache tu kwani nilitumia usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda. Nilijijaza pale Kibarua Restaurant na kuangaza huku na huko. Nikafanikiwa kugundua kuwa Mama Jacq hakuwemo mle ndani. Nikatafuta kiti na kukaa. Mhudumu ambaye alivalia mavazi meupe kuanzia kichwani hadi miguuni, alifika pale nilipokaa haraka sana.
“Tukupe nini kaka?” Aliuliza muhudumu yule wa kiume kwa sauti nzito ya mkwaruzo. Nikanyanya uso kumtazama, kisha nikamjibu..
“Nipe supu kaka”.
“Supu gani? Ya kongoro, utumbo, mbuzi au ya maini?”
“Kaka, saa 10 yote hii masupu ya utumbo ya nini tena?! Namaanisha Pweza kaka, we mgeni nini hapa mjini?” Nilimjibu yule muhudumu kwa kumhisi kuwa hajielewi. Hakuongeza neno, akaondoka eneo lile haraka na kwenda kutekeleza 'oda' yangu.
Nilikua naambaza ambaza macho yangu kulia na kushoto, nikitegemea kumuona Mama Jacq muda wowote akiingia pale. Zikapita dakika kumi zaidi, si mama Jacq aliyeingia, wala muhudumu aliyeleta supu. Nikawa nipo tu pale nikishangaa.
Nikiwa katika mawazo mazito ya mambo mengi yanayonikabili, nikahisi kuguswa begani. Nikainua uso wangu na kukutana na sura ya mwanadada mweupe ambaye kimuonekano alikua ni shombeshombe, yaani mchanganyiko wa aidha muarabu au mhindi na mswahili wa sambaani. Mavazi yake yalitosha kumfahamu kuwa ni mmoja kati ya wahudumu wa hii Restaurant.
“Umeshahudumiwa?” Aliniuliza baada ya macho yetu kugongana.
“Hapana, naomba ukae hapa nikueleze kilichonitokea..” Nilimwambia huku nikimuelekeza kwa mkono akae katika kiti kilichokua mbele yangu. Akatii bila kuongeza neno lolote.
“Nimemwambia tangu mapema yule jamaa pale akuite nikuagize wewe, akakataa.. Matokeo yake nimemwambia alete supu ya pweza mpaka sasa kimya.., sasa hapa nimekaa kama mjinga yani”. Nililalama, lengo likiwa apate kunisikiliza kwa dakika kadhaa, anionee huruma, halafu nipate namba yake. Ndio, kwani hirizi ilikuwa na kazi gani nyingine zaidi ya hiyo?!.
“Ok, ngoja nikakuletee, usijali” Aliongea yule dada na kunyanyuka pale kwenye kiti. Nikamshika mkono na kumrudisha.
“Hapana, mwache tu ataleta, wewe hapa cha kunisaidia ni kitu kimoja muhimu sana..” Nilianza kuitafutia njia sahihi namba yake ya simu.
“Enhee kitu gani hicho?” Aliuliza yule dada..
“Jina lako tu..” Nilimjibu huku nikitabasamu. Nikamfanya na yeye acheke.
“Yaani wewe una vitukooo, mimi nilidhani kitu gaaniii.. Hahahaa... Ok, mi naitwa Ummul-kheir, kwa kifupi niite Ummy”.
“Jina zuri sana Ummy, asante sana kwa kukufahamu, mimi naitwa Jumanne, kwa kifupi Jay” Nikamjibu kama alivyojibu yeye, na kumfanya acheke tena.
“Hhahahah, yani wewe una vituko kweli, sawa basi karibu sana Kibarua Jay” Alionyesha uchangamfu wake.
“Nitakuwa mteja wa hapa wa kila siku endapo nitapata kitu kimoja tu” Nilifikia kuiomba sasa namba yake ya simu.
“Kitu gani tena hicho Jay, maana wewe, unaweza pia ukasema ni supu yako hahahha”.
“Hapana, namba yako ya simu Ummy, hiyo ndio muhimu kwa sasa..”
“Alaa hilo tu, nakuletea, ngoja nikahudumie mteja kwanza.” Aliongea Ummy na kunyanyuka pale alipokua na kwenda meza ya tatu. Nikamfuatilia kwa macho na kugundua kuwa mteja aliyeenda kumhudumia ni Mama Jacq, yawezekana hakuniona hapa nilipokaa. Au anahisi labda sijafika.
Nikaamua kunyanyuka pale nilipokuwa nimekaa na kwenda pale alipokaa yeye.
“Mama, mimi nilishafika muda mrefu sana” Nilimwambia Mama Jacq huku nikimtizama usoni.
“Ooh, pole sana, wakati natoka nikapigiwa simu kuwa jirani yangu mwanawe ni mgonjwa, kwahiyo nikabidi nianzie hospitali kwanza kwenda kumuangalia, kwahiyo umekaa sana hapa?”.
“Hapana, si sana mama”.
“Enhee nakusikiliza, ulikuwa unataka kunambia nini baada ya kuniharibia mwanangu?” Aliniuliza swali lile mama Jacq. Nikatia mfukoni mkono wangu na kuiminya ile Ndere yangu huku moyoni nikitaja Jina la “Mama Jacq” mara tatu.
Nilifanya hivi kwa sekunde tatu haraka haraka na kujifanya kama nimemeza mate.
“Bro, supu yako hii hapa” Ndiyo maneno niliyoyasikia kutoka kwa mhudumu baada ya zoezi langu lile la haraka haraka.
“Asante sana” Nilijibu. Na kabla sijaongea neno jingine lolote kuhusu swali la Mama Jacq, Ummy alikuja na gilasi mbili za Juisi ya parachichi, nadhani hiki ndicho alichoagiza Mama Jacq. Akaziweka pale mezani huku akiziwekea tishu chini yake. Wakati anaondoka alinifinya bega kijanja bila Mama Jacq kuona. Nikahisi katika hizi Juisi zilizoletwa kumeambatanishwa na namba ya simu, kwahiyo nikaongeza umakini.
“Mama, sio siri naomba unisamehe sana, maana sikuwa najua kuwa Jacq ana mama mrembo kama wewe, wala nisingehangaika nae yeye, ningekutafuta wewe mwenyewe” Niliongea wakati nimemaliza kupeleka kijiko kimoja cha supu kinywani kwangu, nikimpiga jicho la wizi Mama Jacq. Hakuongea neno lolote, aliendelea kunitazama tu. Nikaona niendelee.
“Taarifa za kuwa mumeo ni balozi wa nchi hii kule Sweden ninazo, na najua ni jinsi gani uko mpweke sana mwaka mzima. Na najua ni jinsi gani mumeo analazimisha uishi maisha ya kawaida licha ya nafasi uliyokuwa nayo, naomba niwe mfariji wako mama, nimetokea kukupenda sana”. Nikaweka nukta ndogo hapo nikijua sasa Mama Jacq atasema neno lolote.
“Unajua wewe Jay nashindwa kuelewa kwanini hizi dakika chache nilizokaa na wewe hapa nakuona tofauti sana sijui kwanini..?!! Yaani nakuona kama hujanifanyia chochote kibaya, maneno unayosema yanaingia moyoni mwangu kabisaa...” Alianza kuongea kwa hisia mama Jacq, nikajua kazi nimeshaimaliza. Kabla sijaongeza neno nikashtuka na kauli aliyoitoa Mama Jacq.. “Tuondoke hapa, sio sehemu sahihi kwetu kwa sasa”.
Japo nilishangaa sana, lakini sikuwa na cha kufanya zaidi ya kufuata amri yake. Wakati huu ile supu nilishaimaliza. Juisi nilikuwa nimeinywa nusu, nikaondoa ile glasi na kuchukua tishu iliyokuwa chini yake. Nikaikagua vizuri nikakuta imeandikwa namba ya simu, chini yake ikiwa na maneno *Lakini nimeolewa*. Nikatabasamu huku nikijisemea moyoni.. "cha mtu huliwa na mtu bana, chuma ndo huliwa na kutu".
Wakati huu Mama Jacq alishanyanyuka pale alipokuwa amekaa.
Tukatoka, Mama Jacq mbele mimi nyuma. Nikiwa sijui mama Jacq ananipeleka wapi. Tukaingia katika taxi moja pale nje ya Kibarua Restaurant, kisha nikamsikia mama Jacq akimwambia dereva “Regal Naivera”. Sikutia neno lolote, nilijikohoza kidogo tu. 'Jamaa' yangu huko ndani ya boxer nikamsikia akifurukuta kuashiria nafasi haimtoshi ndani ya boxer. Nikajua sasa supu ya pweza inaleta majibu.
“Vyumba vipo?” Aliuliza Mama Jacq pale mapokezi mwa Regal Naivera Hotel.
“Ndio” Alijibu mhudumu wa kike ambaye baada ya kumuangalia mara moja sikuvutiwa naye. Mama Jacq akafuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kujaza katika kitabu cha wageni. Tukazama chumba namba 103. Chumba kilichokuwa na kitanda kikubwa cha 5×6, sofa nzuri, meza ya kioo, kabati, choo safi na AC ilipuliza vizuri sana chumbani mle.
“Jay, nakupa penzi langu kwa lengo moja tu-usimsumbue mwanangu, muache asome” Alisema mama Jacq huku akigeuka na kumuomba nimsaidie kumfungua sidiria yake ya rangi ya bluu bahari. Sketi pamoja na blauzi alishavivua kitambo sana.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
*Usikose sehemu ya 9*