TAFUTA HAPA

Hadithi:Penzi La Mpangaji Sehemu Ya #16

Sehemu ya 16…………
“Kwa hiyo akiwa na hela utamkubalia?”.
“Aaah wapi,hata ajenge nyumba ya dhahabu halafu aje kavaa nguo zilizoshoneshwa kwa noti za elfu kumi,hapa ataambulia manyoya”
“Ha ha haaa,kumbe na wewe una maneno. Kwani wewe Stela umewahi kuwa na boy”.Nikamuuliza baada ya kuona huyo Lameck anazingua tu! kwenye soga zetu.
“Tangu nizaliwe,sema wengi sana wananifuata fuata lakini mimi sina muda nao”.
“Haya bwana,we jitunze hivyo hivyo”.
“Ha ha haaa,kwani wewe vipi? Maana sijawahi kukuona ukileta hapa mwanamke”.Aliuliza swali ambalo nilikuwa napenda sana aulize.
Hapo nikakumbuka filamu moja kaigiza JB, sijui hata inaitwaje. JB yeye alisema, ukitaka kumpata mwanamke, usimwambie kuwa hujawahi kuwa na mwanamke, kwa sababu wanawake wengi sana hupenda wanaume waliyowahi kuwa na wanawake hapo zamani au hupenda wanaume wenye wapenzi tayari,hasa hawa chipukizi kama Stela.
“We acha tu!”. Nikaongea huku kama nimeumia moyo.
“Vipi tena?Mbona umeshindwa kuendelea”.Akaniuliza
“Umenikumbusha mbali ujue?”.
“Wapi tena,mbona umenitisha?”.Aliongea huku akiwa tayari kusikia nitakachomwambia.Wakati huo mimi nilikuwa napanga niseme nini ambacho kitamfanya ajisikie kuomba samahani.
“Aaah! Achana na hizo bwana,tupige story zetu”.
“We si uniambie tu!”.Bado alikuwa ana hamasa ya kujua nini kilichonisibu.
Nilikuwa na viujuzi kidogo vya wanawake,vingine nilivipata bongo muvi na vingine mtandaoni.
Ukitaka kumteka hisia mtoto wa kike kuhusu historia yako ya mapenzi ya nyuma,basi muhadithie ya kusikitisha hata kama ni uongo,hivyo kwangu mimi wala sikuwa na tatizo kuhusu hilo.
Nilipopata cha kumuhadithia,nikaanza kwa upole kuufungua mdomo wangu.
“Nilikuwa naye,lakini hadi sasa sinae tena”.
“Ilikuwaje?”.Akauliza.
“Aliniacha wakati nampenda sana”.
“Yaani ilikuwaje kuwaje mpaka mkaachana”.
“Alifariki bwana”.Niliongea huku nikionesha wazi naumia ili asiendelee kuuliza alikufa vipi.
“Heee,pole jamani. Sikujua bwana,kumbe ndiyo hivyo? Samahani sana”.Alikuwa mpole na kuanza kunibembeleza.