TAFUTA HAPA

Hadithi:Penzi La Mpangaji Sehemu Ya #14

Nilikuwa kijana mpole sana tangu wale wapangaji waamie. Sikutaka kabisa kuwaonesha tabia zangu. Upole wangu uliwapelekea walezi wa ile familia ya akina Stela,kuniamini sana na kuwa wananiachia hata funguo pindi wanapokuwa wametoka wote. Tabia zangu za ucheshi na utani,ziliwapelekea Maimuna na Stela wawe wanashinda kwangu,ambapo kulikuwa na kila kitu anachohitaji kijana,hapa nazungumzia luninga,mziki mkubwa sana tu,friji na vitu vingine vingi.
Mara nyingi nilitumia muda wangu kumfundisha yule mtoto wao mdogo aitwaye James masomo ya ziada,jambo lililoongeza mapenzi baina yangu na ile familia. Hawakuwa hao peke yao,hata wale wapangaji wawili ambao wote walikuwa wanaume,niliweza kuishi nao vizuri sana na bila matatizo.Sikuwa na shaka kabisa,kwani niliamini simba mwenda pole ndiye mla nyama na nilijiongezea na misemo mingi mingine ya ajabu ajabu ninayoijua mimi na akili yangu binafsi.
Pale mtaani walikuwa hawajanijua bado tabia zangu, hivyo sifa zilizoenda kwa walezi wa akina Stela hazikuwa mbaya hata kidogo. Kuna kipindi Stela alikuwa anakuja kukaa na mimi hadi mida ya usiku bila wasiwasi, na mimi wala sikuwa na papara naye.Moyoni mwangu niliendelea kujipa matumaini kwa kubadilisha misemo ya wahenga na kuwa ya kihuni,eti kuku wangu mwenyewe kwa nini nimchinjie msumeno?