TAFUTA HAPA

SMS NZURI SANA KUMTUMIA BABY WAKO

Kila unachokifanya natamani niwepo, nikitumainia kila

ndoto yako itimie kila muda na sehemu, niwepo nikikutakia

mafanikio mema kwasababu nakujali.
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*
Kama ungekuwa kidonda kwenye moyo wangu, ningekiacha na

maumivu yake ndani yangu.
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*
Kusumbuliwa na mlio wa simu yako, humaanisha kuwa muda

fulani, mahali fulani, kuna mtu anakufikiria muda huu, na

huyo ni mimi mara zote nakujali.
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*
Nimekuapata! Kama unanichukia, nipige mshale, lakini

tafadhali si moyoni sababu hapo ndipo wewe ulipo.
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*
Naweza kukuazima mabega yangu upande, masikio yangu

usikilizie mikono yangu ushikie, miguu yangu, utembelee,

lakini si moyo wangu kwani tayari unao wewe.
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*
Lazima utakuwa mwizi sababu umeiba moyo wangu, umechoka

sababu unakimbia mara zote akilini mwangu, na labda mimi

sina shabaha sababu mara zote nikikulenga nakukosa.
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*
Mpenzi kwa mara ya kwanza nilipokuana niliogopa kukuambia,

hata nilipokuambia niliogopa kukupenda, nilipokupenda sasa

naogopa mno kukupoteza. Kusema kweli siko tayari kukukosa

katika maisha yangu.
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*
Wanasema mtu huanguka katika mapenzi mara moja, jambo

ambalo mimi naliona si la kweli kwa maana kila

ninapokutazama najikuta nakupenda tena na tena.
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*
Mpenzi wangu kukutana nawe ilikuwa ni bahati, kukuchagua

kuwa rafiki yangu ilikuwa ni maamuzi yangu, lakini

kuanguka kwenye penzi lako haikuwa hiyari yangu. Umeniteka

moyo na akili yangu pia.
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*
Imani hufanya mambo yote yawezekane, Matumaini hufufua

yaliyopoteza uhai, lakini mapenzi hufanya mambo yote

yaonekane mazuri. Sina linalonihuzunisha maishani mwangu

kwa kuwa tunapendana!
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*
Mpenzi wangu T tambua kuwa ulimwengu tunaoishi una mambo

muhimu matatu. Jambo la kwanza ni kumpata umpendaye, la

pili ni kupata atakayekupenda la tatu ambalo ni kubwa

kuliko yote ni kwa jambo la kwanza na la pili kuungana

pamoja.
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*
Ni vigumu kumpata mwenye mapenzi ya kweli na zaidi yule

atakayekuwa tayari kukupenda zaidi, hivyo nafasi

inapopatika si busara kuichezea tudumishe penzi letu

laazizi wangu.
*°·.¸¸.° ♥ °·.¸¸.°*
Nakupenda mpenzi W nafasi uliyotawala moyoni mwangu ni

kubwa, hakuna ambaye anaweza kufikia uhodari wako, wewe ni

mtu muhimu sana maishani mwangu.