TAFUTA HAPA

SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

http://www.bellanaija.com/wp-content/uploads/2015/06/Pokello-and-Elikem-pre-wedding-3.jpg


Uzuri wa usiku si giza lifunikalo dunia wala si kimya kinachotawala mazingira bali ni njozi njema zenye maono na matarajio yenye mafanikio. Nakutakia ucku mwema

*°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Kama jicho langu halija kuona basi moyoni daima nakukumbuka na ikiwa dua zangu hazijakulinda basi mungu daima
atakulinda,nami cna budi kukutakia usiku mwema.
*°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*

Upendo ni tiba maradhi hukimbia. Salamu ni shiba biriani yazidiwa. Kukumbukana ni haiba nuru hutuangazia. Kwa furaha na mahaba sichoki kusalimia. Usiku mwema

•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
Salio la macho yako halitoshi kuendelea kuona kwa sasa tafadhali tandika kitanda na ulale,kwa maelezo zaidi subiri usingizi ukolee uote ndoto nzuri. usiku mwema!
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•

ni usiku tulivu wenye hali ya hewa saafi na usingizi  wa amani ukishika hatamu kuzisafirisha fikra za binadamu katika  ndoto! najua umechoka na pilikapilika za mchana ,jua na makelele na kila aina ya mwingiliano wa sauti ,ni wasaa mzuri sasa wakupumzisha mwili na akili yako.amua kumsamehe aliyekuudhi mchana wa leo na pia kumbuka ulipokosea leo ili kesho usirudie,lakini pia jipongeze kwa mafanikio ya mipango yako,fumba macho uikaribie nchi usiyoijua.usiku mwema

•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
lala ulale vyema na upoe moyo wako,lala ulale salama utulie roho yako,lala usingizi mwema upumzishe akili yako,akujalie
karima zitimie njozi  zako.usiku mwema
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•

Mpenzi tambua wewe ndiye sababu ya huu usingizi, najilaza kwa pozi nikiamini tutakutana kwenye njozi, njozi za kulienzi letu penzi, Nakupenda mpenzi, gn mwaaah…!!

•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
Jns navyozd kuongea nawe nataman kuwa krb yako,ni chezee zako lips na mwili wako kuukumbatia.nataman kuwa nawe kwan nna meng ya kukuambia.nilee penzin na moyon unitunze.ucku mwema mpz
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•

Usiku mwema mpenzi wangu, upepo wa khuba ukuliwaze katika wako mnono usingz! nakupenda kutoka kwenye chembe ya kulia ya moyo wangu mkunjufu, ulale unono dia!
Nakupend laaziz

•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
natamani kuona macho yako ukiyafumba,natamani kusikia sauti za chini za ndoto zako za ucku,natamani kukuona ukijigeuzageuza kitandani! Natamani busu lako la kunitakia ucku mwema ,lkn yote hayo hayawezekani kwakuwa 2po mbali! Nakupenda dear.
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•

sasa ni usiku najua utakuwa umechoka kwa kazi kutwa nzima ya leo,pumzika mpenzi wangu,ukipanga mambo ya kesho ,lkn elexa ki2 kimoja ,hakuna mwingine moyoni mwangu zaidi yako!

•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
ulikuwa mwanzo mgumu sana kwangu ,lkn moyo nikajipa na kukuweka wazi kuwa nakupenda!
Sikuamini ulivyonikubalia na kunikaribisha moyoni mwako ,nakupenda sana dear ,usiku mwema laaziz wangu!
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•

ajua kazi za kutwa nzima leo zitakuwa zimekuchosha sana mpenzi wangu,pumzisha akili yako na mwili wako kwa ajili ya kufanya kazi tena kesho.pole sana dear!nakutakia usiku mwema

•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
akili yako imechoka,hata mwili wako pia!huu ni wakati wako wa kupumzika mpenzi,nakutakia usiku mwema,lkn uache moyo wako uwe macho kwa kuwa yupo anayekupenda kwa dhati! Nakupenda sana mpenzi wangu,pokea busu mwanana . . .mwaaaaaa . . . . .
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•

Namini utakuwa umerejea kwenye yako makazi na umechoka na kazi mpenzi, badili yako mavazi, bafuni ingia upate maji kujimwagia, nakupenda la azizi, pole sana na kazi!

•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
Giza limeingia simuoni wakunikumbatia niko kama kinda la njiwa na zaidi ya mshitakiwa mwenye hatiya, sjiui wapi joto kwa kwakulipatia na wajua kipupwe kimewadia, uko wapi my dear?
•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•

Nnahmu! nnahamu, Nnahamu jmani nnahamu, Nnahmu mpka nashindwa kujzuia,Ninhmu ya kkutkia ucku mwemw.

•·.·°¯`·.·•*•·.·°¯`·.·•
usiku huu tulivu nikiwa nimejilaza kitandani natamani nisikie sauti yako ambayo hunikosha na kunikosesha raha nisipoisikia.uwembamba Wa Sauti Yako Hupenya Kwenye Ngoma Ya Masikio Yangu Hunitekenya Na Kuniacha Nikifurahi. Nakupend Wangu Kipenzi
*°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
('.') Mh!
<(   )>
_/  /_
Nmechoka kusimama hapa kusubiri sms yako ya kunitakia usiku
mwema. Naenda zangu kulala miguu isije ingia ndani bure...!GD9T
*°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Usiku Ni "utulivu"
Usiku Ni "mzuri"
Usiku Ni"upole"
Usiku Ni "kimya"
Lakini Usiku
Haujakamilika
Bila..Kukutakia
Wewe..
U
S
I
K
U=m=w=e=m=a.
*°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako, naomba
ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
............................
......................
  , - .(. - .
        '.MOYO.'
   WA ' .
. . 'NGU
 unakusaka popote ulipo ili
 ukudokeze ujumbe usemao;

U~S~I~K~U~ ~M~W~E~M~A~