JAMANI MIE UKAHABA SASA BASI" PART 3
INAENDELEA HAPA:
Ilipofika kesho yake asubuhi siku ya Ijumaa tatu  JENIFER na baba yake Mr. Brown walifunga safari mpaka shule, walipofika  shuleni hapo moja kwa moja wakaenda mpaka ofisi ya mwalimu mkuu wa shule  hiyo (HEAD MASTER) walipofika ofisini kwa mwalimu mkuu wakamuomba  JENIFER atoke nje na aelekee mstarini baada ya hapo aende darasani  kusoma. JENIFER akatoka nje na kuelekea mstarini huku ofisini akabakia  mwalimu mkuu na Mr. Brown wakizungumza. Mr. Brown alimuelezea kwa kirefu  mwalimu mkuu kuwa kuna mwalimu wake hapo shuleni anaitwa MWL. KABAVAKO  anamtaka binti yake kama alivyoelezwa na binti yake JENIFER, baada ya  mwalimu mkuu kuambiwa vile alichokifanya akamtafuta kiranja wa shule  akamtuma aende kumuita JENIFER pamoja na huyo Mwalimu KABAVAKO wafike  ofisini hapo kwa mwalimu mkuu. Yule kijana ambae ni kiranja akaenda  kuwaita JENIFER na Mwalimu KABAVAKO walipofika ofisini mwalimu mkuu  akamuomba JENIFER aelezee ilivyokua kuhusu mwalimu KABAVAKO. JENIFER  akaanza kuelezea kama alivyowaelezea wazazi wake kuwa mwalimu KABAVAKO  anamtaka kimapenzi lakini yeye hamtaki na amekua anamtesa sana shuleni  hapo, na amemuahidi kuwa atafanya kila njia ili amfukuzishe shule pia  kuna wanafunzi aliwakamata disco usiku mwalimu KABAVAKO akamuahidi  Jenifer kuwa atamuingiza nayeye katika hilo kosa la hao wanafunzi ili  wafukuzwe wote shule. Ndivyo JENIFER alivyojitetea kwa kusema haya mbele  ya baba yake Mr. Brown, mwalimu mkuu na mwalimu KABAVAKO. Mwalimu  kabavako alipigwa na butwaa akabakia anashangaa kutokana na maneno  aliyosingiziwa lakini alikua ni mwenye busara na subira akamuacha  JENIFER azungumze mpaka alipomaliza ikafika zamu yake mwalimu KABAVAKO  ajielezee alichokifanya mwalimu kabavako akamuuliza swali JENIFER  "JENIFER WEWE HAPA SHULENI UNA MARAFIKI?" Jenifer akamjibu "NDIO NINAO"  mwalimu KABAVAKO akamwambia "UNAWEZA KUNITAJIA MARAFIKI ZAKO WATATU  MUHIMU AMBAO NI WAKARIBU SANA?!" Jenifer akaanza kuwataja marafiki zake  watatu ambao ndio yupo nao karibu sana na katika hao marafiki watatu  aliowataja JENIFER ndio wale ambao mwalimu KABAVAKO aliwakamata wako  wote na JENIFER usiku, baada ya hapo mwalimu KABAVAKO akamuuliza baba  yake na JENIFER "MZEE SIKU YA IJUMAA MOSI BINTI YAKO JENIFER ALILALA  NYUMBANI?!" Baba yake na JENIFER akajibu "MWALIMU MBONA SIKUELEWI  TUNAULIZANA MASWALI KAMA TUPO KITUO CHA POLISI?" mwalimu KABAVAKO  akamjibu "MZEE PUNGUZA JAZBA MIMI NINAKUULIZA HIVI NINA MAANA YANGU"  baba yake na Jenifer ikabidi amjibu mwalimu "KILA SIKU YA IJUMAA MOSI  MWANANGU HUWA ANATOKA ANAENDA KUJISOMEA NA WENZAKE USIKU KUCHA ASUBUHI  ANARUDI NYUMBANI" baada ya mwalimu KABAVAKO Kumuuliza maswali JENIFER na  baba yake kisha akatoka nje na kumtafuta mwanafunzi kisha akamuagiza  yule mwanafunzi aende ofisi kuwaita wale wanafunzi watatu aliowakamata  wakiwa Club usiku pamoja na JENIFER, yule mwanafunzi akaenda kuwaita  wale rafiki zake na JENIFER walikuwa wamevaa mavazi yao ya nyumbani  waliyokamatwa nayo wakaelekea mpaka ofisi ya mwalimu mkuu. Walipofika  ofisini mwalimu KABAVAKO akawauliza "NYIE WANAFUNZI MNAMJUA HUYU  MWANAFUNZI MWENZENU?" wakajibu "NDIO MWALIMU TUNAMJUA ANAITWA JENIFER"  akawauliza tena "KWANINI NYIE MMEKUJA SHULENI MKIWA MMEVAA HIZO NGUO ZA  NYUMBANI TENA FUPI?" wale wanafunzi wakajibu "MWALIMU WEWE SI  ULITUKAMATA SIKU YA IJUMAA MOSI USIKU CLUB UKATUAMBIA TUJE LEO OFISINI  KWAKO NA HIZI NGUO PAMOJA NA WAZAZI WETU?" mwalimu KABAVAKO akawauliza  tena "NILIPO WAKAMATA HIYO SIKU YA IJUMAA MOSI MLIKUA NYIE NYIE WATATU  PEKE YENU AU?" wakajibu "HAPANA MWALIMU TULIKUA PAMOJA NA JENIFER" pale  pale JENIFER nguvu zikamuishia akajua tayari kishakamatwa hana jinsi  akaanza kulia ofisini kwa mwalimu mkuu. Mwalimu mkuu akamwambia JENIFER  "JENIFER TAFADHALI USINIFICHE NIELEZE UKWELI UKINIDANGANYA NAWEZA  KUKUCHAPA HAPA MBELE YA BABA YAKO NA NITAKUFUKUZA SHULENI KWANGU,  NIELEZE UKWELI SI UNAONA WENZAKO WAMENIELEZA UKWELI? HAYA NAWEWE NIELEZE  UKWELI WAKO, MWALIMU KABAVAKO ALIKUKAMATA CLUB KWELI?" JENIFER  akajikuta anasema ukweli "NDIO MWALIMU ALINIKAMATA JUZI IJUMAA MOSI  USIKU NIKO NA HAWA MARAFIKI ZANGU CLUB" mwalimu mkuu akamuuliza tena "NA  JE, NIKWELI MWALIMU KABAVAKO AMEISHAWAHI KUKUTONGOZA?" JENIFER akakosa  jibu akakaa kimya, ghafla JENIFER akasema "BABA NAKUOMBA UNISAMEHE  NILIKUDANGANYA MWALIMU HAJAWAH KUNITONGOZA ILA NILITAKA NIJITETEE UKWELI  NIKWAMBA ALITUKAMATA CLUB USIKU" pale pale Mr. Brown nguvu zilimuishia  akamwambia mwalimu KABAVAKO "MWALIMU NISAMEHE MIMI KWA YOTE HAYA, KUMBE  HUYU MTOTO NI MUONGO SINA LA KUSEMA NAOMBA MUMPE ADHABU YOYOTE ILE NIKO  TAYARI, MSHENZI SANA HUYU MTOTO" mwalimu mkuu akamwambia mwalimu  KABAVAKO atoke nje na wale wanafunzi watatu pamoja na JENIFER akawachape  fimbo kisha arudi nao ofisini kwake. Mr. Brown akabakia na mwalimu mkuu  wanaongea!