JAMANI MIE UKAHABA SASA BASI" PART 2
INAENDELEA HAPA:Baada ya JENIFER na wenzake kukamatwa na mwalimu na  kupewa adhabu hiyo ya kwenda na wazazi wao shuleni siku ya Ijumaa tatu  na kupelekea kupoteza mudi ya kuendelea kufurah usiku huo ikawabidi  waondoke kabisa sehemu hiyo ya CLUB usiku huo huo na kwenda kulala  kwenye chumba cha rafiki yao CHRISTINA waliekuwa nae katika kundi lao  usiku huo, ilipofika kesho yake siku ya ijumaa pili asubuhi kila mtu  alirejea nyumbani kwao huku wakiwa na sura za hudhuni na mawazo kibao  kichwani wakijiuliza itakuaje kesho yake ambayo ni siku ya Ijumaa tatu  wanatakiwa waende shule na wazazi wao?!. Jenifer alipofika kwao moja kwa  moja alielekea chumbani kwake na kujilaza kitandani huku akiwa na  mawazo kibao hata chakula hakuweza kula siku hiyo muda wote alikua  kajifungia chumbani analia. Ghafla akasikia mlango wa chumbani kwake  unafunguliwa aliposhtuka akamuona mama yake Mrs. Brown. Mrs. Brown  alimsogelea binti yake Jenifer kuanza kuzungumza nae kama ifuatavyo:-
MRS. BROWN:"Jenifer binti yangu mbona unaonekana leo hauko sawa, nini tatizo mwanangu?! Na mbona unalia?
JENIFER:"Hapana mama, wala usijali hamna kitu chochote naomba uwe na amani mama yangu, niko sawa tu!"
MRS. BROWN:"Jenifer mwanangu lazima kutakuwa kuna kitu ila  unaficha. Mwanangu nakuomba unieleze usinifiche niambie tu mwanangu wala  usiogope"
JENIFER:"Mama wala usijali hakuna kitu chochote kile"
MRS. BROWN:"Sidhani binti yangu kama kweli hakuna tatizo sasa mbona unalia, Au umepata ujauzito?!
JENIFER:"Mama bora ningekua nina ujauzito ila kwa hiki  kilichonipata mama yangu najuta tena najuta hata sijui kwanini  mlinipeleka shule mama yangu"
MRS. BROWN:"Mwanangu mbona unasema hivyo kwani kuna tatizo limetokea shule?!
JENIFER:"Ndio mama, kuna mwalimu shuleni alinitongoza  nikamkatalia sasa kila siku huwa ananichapa fimbo bila makosa na  ananitesa sana shule na kaniahidi kuwa atanitafutia kosa lolote la uongo  ili nifukuzwe shule anikomoe na juzi siku ya Ijumaa kuna wanafunzi  kawakamata usiku CLUB akawaambia kuwa atawafukuza shule sasa kaniambia  namimi ataniingiza katika hilo kosa la hao wanafunzi kesho shuleni ili  nifukuzwe namimi"
MRS. BROWN:"Haiwezekani mwanangu wewe nyamaza acha kulia  tumsubiri baba yako aje nimuelezee ikiwezekana kesho akupeleke shule  akamkomeshe huyo mwalimu, wala usiwaze sana mwanangu Jenifer looooo,  huyo mwalimu hana hata aibu"
Baada ya Jenifer kutumia uongo wa kumdanganya mama  yake Mrs. Brown kwa dhumuni la kujitetea kutokana na kosa alilolifanya  usiku wa jana yake walipokutwa na mwalimu wao wa shule CLUB ikamlazimu  kumpa kesi ya uongo yule mwalimu kwa wazazi wake ili wasimuone yeye  anamakosa. Mama yake na Jenifer Mrs. Brown alihamaki na kuingiwa na  hasira akawa anamsubiria mume wake arudi ili amuelezee kilichotokea.  Ghafla baba yake na Jenifer Mr. Brown akaingia nyumbani kwake na kumkuta  mke wake Mrs. Brown akiwa na binti yao Jenifer, Jenifer alipomuona baba  yake Mr. Brown akaanza kuangua kilio huku akisema "BABA NAJUTA MIMI  MWANAOO, NAJUTA BABA HIVI KWANINI ULINIPELEKA NIKASOME ILE SHULE BABA  YANGUUUUUU" Jenifer alikua analia huku akitoa sauti kubwa ya  kumlalamikia baba yake. Mr. Brown alipigwa na butwaa hakujua nini  kinachoendelea ikabidi akae chini na kumuuliza mke wake "MKE WANGU NINI  KIMEMPATA BINTI YETU JENIFER?" Mrs. Brown akamjibu mume wake "MUME WANGU  NENDA KWANZA KAKOGE KISHA ULE HALAFU NDIO NIKUELEZEE KILICHOTOKEA" Mr.  Brown nae akamjibu "HAPANA MKE WANGU NIELEZEE KWANZA NIJUE TATIZO  NINI?". Mrs. Brown ikabidi aanze kumuhadithia kama alivyohadithiwa na  binti yao Jenifer kuwa kuna mwalimu wa shule alimtongoza binti yao  akamkataa sasa huyo mwalimu anamtesa sana Jenifer shuleni na kamuahidi  atamfanyia njama yoyote ili binti yao afukuzwe shuleni. Pale pale Mr.  Brown nayeye akapandwa na hasira akamnyamazisha binti yake Jenifer na  kumwambia "JENIFER BINTI YANGU NYAMAZA, KESHO IJUMAA TATU ASUBUHI  TUTAKWENDA WOTE MPAKA SHULENI KWENU UKANIONESHE HUYO MWALIMU.  ATANITAMBUA" baada ya hapo wakatawanyika Jenifer akaingia chumbani  akaanza kushangilia peke yake kimya kimya akiwa na imani kuwa  kishamaliza kesi aliyokuwa nayo na akawa na furaha tele akaendelea  kufanya mambo yake kama kawaida.