TAFUTA HAPA

JAMANI MIE UKAHABA SASA BASI" PART 3

INAENDELEA HAPA:
Ilipofika kesho yake asubuhi siku ya Ijumaa tatu JENIFER na baba yake Mr. Brown walifunga safari mpaka shule, walipofika shuleni hapo moja kwa moja wakaenda mpaka ofisi ya mwalimu mkuu wa shule hiyo (HEAD MASTER) walipofika ofisini kwa mwalimu mkuu wakamuomba JENIFER atoke nje na aelekee mstarini baada ya hapo aende darasani kusoma. JENIFER akatoka nje na kuelekea mstarini huku ofisini akabakia mwalimu mkuu na Mr. Brown wakizungumza. Mr. Brown alimuelezea kwa kirefu mwalimu mkuu kuwa kuna mwalimu wake hapo shuleni anaitwa MWL. KABAVAKO anamtaka binti yake kama alivyoelezwa na binti yake JENIFER, baada ya mwalimu mkuu kuambiwa vile alichokifanya akamtafuta kiranja wa shule akamtuma aende kumuita JENIFER pamoja na huyo Mwalimu KABAVAKO wafike ofisini hapo kwa mwalimu mkuu. Yule kijana ambae ni kiranja akaenda kuwaita JENIFER na Mwalimu KABAVAKO walipofika ofisini mwalimu mkuu akamuomba JENIFER aelezee ilivyokua kuhusu mwalimu KABAVAKO. JENIFER akaanza kuelezea kama alivyowaelezea wazazi wake kuwa mwalimu KABAVAKO anamtaka kimapenzi lakini yeye hamtaki na amekua anamtesa sana shuleni hapo, na amemuahidi kuwa atafanya kila njia ili amfukuzishe shule pia kuna wanafunzi aliwakamata disco usiku mwalimu KABAVAKO akamuahidi Jenifer kuwa atamuingiza nayeye katika hilo kosa la hao wanafunzi ili wafukuzwe wote shule. Ndivyo JENIFER alivyojitetea kwa kusema haya mbele ya baba yake Mr. Brown, mwalimu mkuu na mwalimu KABAVAKO. Mwalimu kabavako alipigwa na butwaa akabakia anashangaa kutokana na maneno aliyosingiziwa lakini alikua ni mwenye busara na subira akamuacha JENIFER azungumze mpaka alipomaliza ikafika zamu yake mwalimu KABAVAKO ajielezee alichokifanya mwalimu kabavako akamuuliza swali JENIFER "JENIFER WEWE HAPA SHULENI UNA MARAFIKI?" Jenifer akamjibu "NDIO NINAO" mwalimu KABAVAKO akamwambia "UNAWEZA KUNITAJIA MARAFIKI ZAKO WATATU MUHIMU AMBAO NI WAKARIBU SANA?!" Jenifer akaanza kuwataja marafiki zake watatu ambao ndio yupo nao karibu sana na katika hao marafiki watatu aliowataja JENIFER ndio wale ambao mwalimu KABAVAKO aliwakamata wako wote na JENIFER usiku, baada ya hapo mwalimu KABAVAKO akamuuliza baba yake na JENIFER "MZEE SIKU YA IJUMAA MOSI BINTI YAKO JENIFER ALILALA NYUMBANI?!" Baba yake na JENIFER akajibu "MWALIMU MBONA SIKUELEWI TUNAULIZANA MASWALI KAMA TUPO KITUO CHA POLISI?" mwalimu KABAVAKO akamjibu "MZEE PUNGUZA JAZBA MIMI NINAKUULIZA HIVI NINA MAANA YANGU" baba yake na Jenifer ikabidi amjibu mwalimu "KILA SIKU YA IJUMAA MOSI MWANANGU HUWA ANATOKA ANAENDA KUJISOMEA NA WENZAKE USIKU KUCHA ASUBUHI ANARUDI NYUMBANI" baada ya mwalimu KABAVAKO Kumuuliza maswali JENIFER na baba yake kisha akatoka nje na kumtafuta mwanafunzi kisha akamuagiza yule mwanafunzi aende ofisi kuwaita wale wanafunzi watatu aliowakamata wakiwa Club usiku pamoja na JENIFER, yule mwanafunzi akaenda kuwaita wale rafiki zake na JENIFER walikuwa wamevaa mavazi yao ya nyumbani waliyokamatwa nayo wakaelekea mpaka ofisi ya mwalimu mkuu. Walipofika ofisini mwalimu KABAVAKO akawauliza "NYIE WANAFUNZI MNAMJUA HUYU MWANAFUNZI MWENZENU?" wakajibu "NDIO MWALIMU TUNAMJUA ANAITWA JENIFER" akawauliza tena "KWANINI NYIE MMEKUJA SHULENI MKIWA MMEVAA HIZO NGUO ZA NYUMBANI TENA FUPI?" wale wanafunzi wakajibu "MWALIMU WEWE SI ULITUKAMATA SIKU YA IJUMAA MOSI USIKU CLUB UKATUAMBIA TUJE LEO OFISINI KWAKO NA HIZI NGUO PAMOJA NA WAZAZI WETU?" mwalimu KABAVAKO akawauliza tena "NILIPO WAKAMATA HIYO SIKU YA IJUMAA MOSI MLIKUA NYIE NYIE WATATU PEKE YENU AU?" wakajibu "HAPANA MWALIMU TULIKUA PAMOJA NA JENIFER" pale pale JENIFER nguvu zikamuishia akajua tayari kishakamatwa hana jinsi akaanza kulia ofisini kwa mwalimu mkuu. Mwalimu mkuu akamwambia JENIFER "JENIFER TAFADHALI USINIFICHE NIELEZE UKWELI UKINIDANGANYA NAWEZA KUKUCHAPA HAPA MBELE YA BABA YAKO NA NITAKUFUKUZA SHULENI KWANGU, NIELEZE UKWELI SI UNAONA WENZAKO WAMENIELEZA UKWELI? HAYA NAWEWE NIELEZE UKWELI WAKO, MWALIMU KABAVAKO ALIKUKAMATA CLUB KWELI?" JENIFER akajikuta anasema ukweli "NDIO MWALIMU ALINIKAMATA JUZI IJUMAA MOSI USIKU NIKO NA HAWA MARAFIKI ZANGU CLUB" mwalimu mkuu akamuuliza tena "NA JE, NIKWELI MWALIMU KABAVAKO AMEISHAWAHI KUKUTONGOZA?" JENIFER akakosa jibu akakaa kimya, ghafla JENIFER akasema "BABA NAKUOMBA UNISAMEHE NILIKUDANGANYA MWALIMU HAJAWAH KUNITONGOZA ILA NILITAKA NIJITETEE UKWELI NIKWAMBA ALITUKAMATA CLUB USIKU" pale pale Mr. Brown nguvu zilimuishia akamwambia mwalimu KABAVAKO "MWALIMU NISAMEHE MIMI KWA YOTE HAYA, KUMBE HUYU MTOTO NI MUONGO SINA LA KUSEMA NAOMBA MUMPE ADHABU YOYOTE ILE NIKO TAYARI, MSHENZI SANA HUYU MTOTO" mwalimu mkuu akamwambia mwalimu KABAVAKO atoke nje na wale wanafunzi watatu pamoja na JENIFER akawachape fimbo kisha arudi nao ofisini kwake. Mr. Brown akabakia na mwalimu mkuu wanaongea!