TAFUTA HAPA

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 27)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA 27

Hakuweza kuvumilia macho yalianza kumwaga machozi ya furaha, moyo wote ulimwagika, alitoa kitambaa kujifuta futa lakini hayakuzuilika, ukawa mshangao mkubwa kwa mr mtikira pamoja na Sasha waliokuwa pembeni yake.

" Bosi vipi!? ,, aliuliza sasha kwa mshangao.

Seid hakujibu swali hilo, hatimae alitoa cm mfukoni, akampigia mama yake, cm ilifanikiwa kuita, sekunde kadhaa mama yake akawa amepotea.

" Mama ,, alimuita, akiwa anavuta mafua ya kilio kwa ndani.
" Mwanangu, umefika salama baba ,,, aliuliza bi najma.
" Ndio mama nimefika.
" mbona kama unalia ?
" nimekukumbuka mamaangu, nimekupigia cm kukuambia Asante kwa kufanya juu chini mpaka hapa nlipo, nakushukuru sana mama naitaji zaid dua zako ,, alisema akiwa bado katika sura ya kulia.
" mwanangu mimi nakuombea kila dakika kila sekunde, uko wapi sasa hivi?
" ndo nimeingia ofisini ntapokuwa nafanya kazi, nkaona siwezi kufanya chochote kwanza kabla sijasikia sauti yako mama angu.
" Mungu akusaidie na nshallah amina Mungu yu pamoja nawe.
" Asante sana mama.

alikata cm kisha akaiweka mfukoni, mtikira alimuangalia seid bila kummaliza, alishangaa sana kuona namna anavyokubali machozi yake yatoke wakati ni kipindi cha furaha cha kuwa kwenye ofisi kubwa, kiti kizuri.
" umenishangaza sana kijana, hakuna anaepata nafasi kama hii akalia ndo kwanza nakushuhudia wewe! , kwa nini imekuwa hivi! ,, aliuliza mr mtikira.

Seid alisogea mpaka ilipokuwa meza, aliishika shika kuiangalia namna ilivyotengenezwa vizuri, aligeuka akaiegamia, akakunja mikono yake akiwa anaangalia chini, huku akifinya finya macho.
" Kuna vilio vya aina tano tofauti, menega!, na kilio changu bahati mbaya kimekosekana kati ya hivyo vitano,, mimi ni miongoni mwa vijana wachache sana ambao hawawezi kusahau walikotoka katika maisha yao ,,, alipoongea hivyo akainua uso wake kumwangalia mtikira na sasha ,, nimeishi maisha ya tabu sana menega wangu, nimelala na njaa, nimeamka na njaa, nimeshinda na njaa mimi unaeniona hapa, ilifika muda nlitamani kufa kuliko mateso nnayoyapata ya kuchekwa, kunyanyapaliwa na baadhi ya watoto enzi za utoto wangu, pia na wanafunzi wenzangu ,,, Maisha yangu yalikuwa mfano wa sahani, inachafuka kwa kuwekwa chakula na kuoshwa, lakini pia inachafuka bila kuwekwa chakula kwa vumbi au uchafu utaokuwa karibu nayo.
Namshukuru sana mamaangu, ambae ,, alikuwa yuko tayari kumvulia hata mwanaume nguo, kuudhalilisha mwili wake, ili apate pesa za kunisomesha, ,, lakini namshukuru Mungu haikutokea hivyo japo aliwai kuntamkia, ,, Napata uchungu mkubwa sana nkikumbuka mambo aliyofanyiwa mama na mzee wangu, ,,, Menega usione watu tunakuja kukalia viti vizuri hakika tumetoka mbali, ,, wakati mwingine mtu ana haki ya kuringa anapopata chansi ya kupata mali japo si vizuri, kwa sababu watu tunatoka mbali sana menega wangu,, mtu mpaka kuwa tajiri anakuwa ashahangaika sana ndo maana unaweza kumuomba mtu mwenye pesa akusaidie akakukatalia hata kama anacho kwa sababu ya hasira ya mambo mengi mabaya, yakunyanyapaliwa aliyopitia japo si wote, , but, zaid ya kumshukuru  Mungu wangu sina lengine, mamaangu ,, pia rafiki yangu kipenzi Hamad walionifanya mimi kuwa na Elim hii hapa,, ,, ofisi nshaiona tunaweza kwenda tu menega.

Mtikira aliachia pumzi aliposikia maneno ya kijana, walitoka ofisini vitu vyake kadhaa akawa ameviacha, akijua kesho atavikuta, walitoka sasha akafunga mlango, akakabidhiwa rasmi funguo za ofisi pamoja na funguo nyingine tofauti zilizokuwa zikiifadhiwa na Sasha, Sasha alikaa kwenye kiti chake, Seid na mr mtikira wakatoka huku sasha akimuambia seid karibu....

walishuka taratibu kutumia ngazi za kawaida, njiani walikutana na baadhi ya wafanya kazi, walipofika nje, seid aliombwa aingie kwenye gari, wakaanza safari ya kwenda kwenye nyumba yake seid ambayo amepangiwa kuishi.

" Bosi hii nyumba unayoenda kuishi, ni ya kifahari sana, pia ni kama ya kupanga, kwa sababu kwenye mkataba wake kuna kifungo cha kuinunua kabisa endapo utaridhishwa na manufaa ya kampuni ili hata likija kutokea la kutokea uwe tayari una nyumba ambayo iko nje na nyumba  za kampuni ,, alisema mr mtikira kipindi wako kwenye gari, kutoka posta kuitafuta bara bara ya masaki sehemu ambayo kulikuwa na nyumba hiyo.

" Aisseee! ,, ina maana unaruhusiwa kununua nyumba ya kampuni ? ,,aliuliza seid.
" Na wafanyazi wengi wa vitengo vya juu wamefanya hivyo nkiwemo mimi hapa ,, mwanzo nlipoanza, nlikaa miaka miwili nkiwa naweka asilimia kumi ya pesa zangu nnazopokea kama mshahara ili zitimie za nyumba niinunue, nlifanikiwa hilo, sasa hivi siko kwenye nyumba ya kampuni tena.

" Waaao! si ni pesa nyingi sana hasa kwa hii pesa yetu isokuwa na thamani duniani ,, aliuliza tena seid kuhusu pesa.
" Kwa nlivyoangalia mkataba wa nyumba kama ile yako, ni kuwa ukiitaka, mshahara wako unakuwa unakatwa juu kwa juu robo yake ndani ya miaka mitatu, ina maana hapo kwa hesabu za haraka ni milioni 480.

Seid ilibidi ageuke alipotajiwa hizo pesa.
" ndugu yangu mbona tunatiana presha, milion mia 480 za kitanzania.
" ndio, tena hapo kakuuzia mzungu sasa, mtanzania mwenzako alikuwa anapiga hadi mia tano.....

Daaaah basi maisha nshayafaulu ,, kama nkiitaji nyumba inakatwa robo tu ndani ya miaka mitatu milion 480 zinakuwa tayari, ina maana hapo kwa mwezi malipo yangu ni zaid ya milion kumi sasa

.... ,, alipouliza kwa mshangao na kujibiwa, aligeuka akaangalia kwa nje huku akiwaza.

" Mbona umeshtuka nyingi au kidogo? ,, mr mtikira aliuliza, seid ni kama hakusikia swali lenyewe, bado mawazo mazito yaliyoambatana na tabasam la furaha yalikuwa yamemchukua ,, mtikira alimuangalia jamaa yake, aliekuwa amegeukia kwa nje muda huo, akamshtua kwa kumuita.
" Nimeuliza mbona umeshtuka, nyingi au kidogo ? ,, alimuuliza tena baada ya kumshtua akashtuka.
" Ndugu yangu pesa ya kununua nchi useme ndogo? ,, kwa wenzetu ndo ndogo huko, ,, kwani hiyo nyumba yenyewe ikoje? ,, aliuliza seid akiwa bado yuko kwenye mshangao.
" ngoja tunafika muda si mrefu, ukisikia majengo ya masakiii beach ndo huko, nyumba nyumba kweli, imefungwa kila kitu na magari mawili ya kutembele si mchezo tena yote ya bei mbaya.

alipotajiwa magari kidogo akawa ameshawishika, moyo wake ulitakata, bado alikuwa anadhani labda magari anatakiwa anunue mwenyewe.
" ina maana hiyo nyumba ukiinunua na gari zake kwa hiyo pesa.
" Aah wapi ,, hapana, magari mawili yote milioni Tisini na tano mbali na pesa za nyumba.

Seid hakujibu kitu zaid ya kuguna, alijikuta anadata baada ya kuambiwa magari mawili milion tisini, milion moja ilikuwa ni pesa nyingi sana kwake, kwa sababu bado hakuzikamata, alivyotajiwa milion 480, mara 95 ni kama alikuwa anadatishwa ghafla.

Walifika maeneo ya masaki beach, seid muda wote alikuwa katika mshangao wa kuangalia majengo namna yalivyo ya kifahari.
" Mr mtikira huku hakuna masikini nini? ,, aliuliza baada ya kuona kila nyumba anayoiangalia ya majuu.
" wapo ila si wengi ndugu yangu, sana sana huku wanaishi wabunge, watu wanaofanya kazi kwenye makampuni makubwa,  viongozi na wengine.

walifika katika geti la nyumba ambayo atakuwa akiishi seid, waliingia ndani wakapaki gari lao sehemu iliyokuwa na paking nzuri pembeni yake kuna magari mawili ya kisasa, walishuka seid hakuweza kuamini alipoiona nyumba anayotakiwa kuishi yeye ilivyo nzuri, imejengwa kitaalam zaid, alipeleka macho kila kona na kuiona inavyovutua.
" hii ndo nyumba yenyewe sio ,, aliuliza
" yes! , hii ndo yenyewe unaionaje.
" kweli hapa hata milion 480 wana haki ya kukutoza, nimeamini.

waliongea ongea baada ya kushuka, funguo zote za nyumba alikuwa nazo mtikira, akamkakabidhi funguo, kisha wakaanza kuzunguka eneo kwa eneo nje ya nyumba mpaka ndani...
usiku tayari ulishaanza kuingia, alioneshwa maeneo yote ya nyumba, walipoingia ndani alipelekwa kila chumba kila sehemu akaijua, walipomaliza waliingia seble ndogo iliyokuwa mwanzo kabisa ukiingia ndani, wakaongea tena mawili matatu, mtikira akaitaji kuondoka, alimuomba watoke wote ili akamuoneshe restaurant iliyopo karibu kwa ajili ya mambo ya misosi.

Waliongozana wote mpaka restautant kwa kutumia gari la mtikira, jirani yake kabla ya restaurant kulikuwa na sheri, alioneshwa kama akiitaji mafuta, kisha  wakaenda mpaka kwenyewe ambako hakukuwa mbali sana huku wakitaniana ndani ya gari....
njaa ilikuwa tayari imekamata, walipofika waliagiza chakula moja kwa moja, wakapiga kisha ndo wakarudi, walipofika kwenye nyumba ya seid, seid alishushwa kwa nje, mtikira akamuaga na kuondoka..

alifungua  geti dogo roho ikiwa shwari, alipoingia kwa ndani alisimama dakika mbili nzima, akiangalia mjengo aliopewa kuumiliki namna ulivyo mzuri, aliushusha akaupandisha na kuushusha tena, taa za pande zote zilikuwa zinawaka kuondoa kigiza ambacho kilikuwa tayari kimetanda, aliangalia sehemu za bustanini bila kupapatia jibu namna palivyotengenezwa, kulikuwa na miti mitatu mirefu, alitembea mpaka eneo la gari, akawasha moja baada ya lengine, akayajaribu yote akayakuta yako vizuri, alijikuta anacheka peke yake kijana, kijasho cha furaha kilimtoka, alijua huu ni muda wake wa kutesa baada ya kuteseka miaka mingi, jinsi alivyokuwa akijisikia ni Mungu pekee aliekuwa anajua, alishuka kwenye gari cm yake ghafla ikaita..

Aliweka mkono mfukoni akaitoa na kuangalia nani anapiga, jina lilikuja menenga akajua mr mtikira, alipokea haraka akiambatanisha na neno ,,," Haloo menega.
" Ndugu yangu kuna kitu nimesahau.
" Kitu gani menega ,, Seid aliuliza.
" Kuhusu msichana wa kazi kukutafutia, then mikataba yote ya nyumba iko kwenye droo ya kabati lililoko chumba cha kulala, utaiona utaisoma ili uielewe.
" Kwa hilo nimekuelewa, ila kuhusu msichana wa kazi sijui, achana na hilo ntakaa tu mwenyewe.
" huogopi peke yako ndugu.
" usijali siitaji msichana wa kazi.
" Ok bosi usiku mwema
" Nawe pia.

Menega alikata cm akijiuliza kwa nini bosi wake haitaji msichana wa kazi wakati ni muhimu, seid aliweka cm mfukoni akaanza kutembea kuelekea upande wa pili wa nyumba, cm yake ikaita tena, aliitoa kuangalia nani akakuta Hamad, aliachia tabasam kisha akapokea.

" Rafiki yangu kipenzi ,, alimuita hamad kwa furaha.
" Swahiba vipi hali ? ,, aliuliza hamad.
" Namshukuru Mungu huko vipi ndugu yangu wazima?
" huku pia tunamshukuru Mungu, naamini usingizi wa leo utakuwa ni wa historia kwako.
" Hahahahaaaaaaa!! ,, kwa nini rafiki yangu ,,, alicheka sana seid baada ya kuambiwa hivyo.
" utakuwa kama samaki aliekuwa amezoea maji ya chumvi akaingia ya baridi, japo anaweza kufadhaika ila akifanikiwa kupeta basi huwa hatamani tena kutoka na hata usingizi wake huwa ni wa muda mrefu sana.
" Umeshinda hamad, mimi sikuwezi wewe, ila rafiki yangu mzungu anajenga bhna.
" kwa nini unasema hivyo.
" Hili jengo nlilopatiwa, nimeambiwa limejengwa na wazungu, ndugu yangu limefungwa, si mchezo.
" Mimi nataka kesho unitumie kwenye mtandao, nilishuhudie kwa macho yangu.
" Kuhusu hilo usijli rafiki yangu, ila nakushukuru sana swahiba, yani Rafiki yangu hamad mi mpaka kesho sitokuwa na la kukulipa, Wallah naapia rafiki yangu, yani msaada wako kwangu, ,, ni zaid ya msaada wa mkulima aliekuwa na kidumu chake kidogo cha maji begani pamoja na jembe, akawakuta wasafiri watatu wakiwa wamekwama njiani kwa sababu ya njaa ya kiu, akatoa maji akawapatia wakanywa yote kisha kiu kikaja upande wake baada ya kutembea kwa muda mrefu wakati maji hana tena, nakushukuru sana hamad, yani nakushukuru sana na Mungu akubariki nshallah ,, aliongea kwa kusisitiza...
" we ni rafiki yangu, kwa hilo usijali,  kinachotakiwa ni dua na ibada tu kaka, si unajua yote hayo ni mapito? ,,,, but okey, yote tisa, kumi nlitaka kukutakia usiku mwema kwa sababu leo najikia uchovu sana, nlikuwa kwenye harakati za maandalizi ya ndoa ndugu yangu.
" Sawa nimekuelewa, ila hamad, naomba unambie kitu kidogo mimi kama rafiki yako, kweli mtarajiwa wako hujalala naeee! au ilikuwa changa la macho tu lile? ,, alimuuliza rafiki yake kama utani wa kweli.
" Heheheee Naapia mbele ya mola wangu ndugu, sijalala nae kabbisa kabisa.
" Sema akyamungu ,, alisema katika hali ya siamini.
" Akyamungu nakuambia.
" Ndugu yangu mi ngoja nikutakie usiku mwema umeshinda  ....

wote walicheka sana cm ikakatika, seid aliitumbukiza mfukoni bado akiwa ameachia tabasam, alizunguka nyuma ya nyumba ambako alikutana na mbwa watatu ambao ni kama walinzi, ni mbwa waliofunzwa na harufu ya seid walishaijua, mwanzo walikuwa wamemzoea mtikira lakini baada ya seid kufika mtikira aliwaonesha mwenyeji wao na wakamzoea usiku huo huo, walimwangalia sana akachuchumaa kuwashika shika, alifanya hivyo ndani ya dakika tano akanyanyuka akatembea tena mpaka upande wa pili bustanini kote kisha akarudi ndani.

" Maisha ni theluthi kubwa sana kwa mwanadam, nimejifunza mengi mpaka sasa hivi nlikofikia, baada ya miaka 20 hatimae ndoto zangu zote zimetimia, niko tayari kuinunua hii nyumba ili isiwe ya kiofisi, rizki ni kwa mafungu, fungu langu la kukaa pale linaweza kuisha kisha nyumba ikawa haiko mikononi mwangu nkaazirika, tena ntataka iwe inakatwa nusu kabisa ili nichukue na magari yote mawili, Nakushukuru sana Mungu, Naomba uniongoze katika maisha yangu haya mapya.

Aliwaza akiwa amekaa moja ya masofa yaliyokuwa sebleni baada ya kuingia ndani, alitupa macho ukutani akaona luninga kubwa ya flat, alienda kuiwasha na king'amzi cha dstv kilikuwa hapo hapo pembeni, alianza kuangalia vitu huku akitupa macho yake huku na kule, alicheka na moyo wake ,,, " haya ndo maisha sasa, yani kuangalia vitu vilivyomo tu moyo unafurahi, nimeamini hakuna nafsi inayopenda maisha mabovu bhana basi tu, maisha kama haya alafu ukonde!, wana haki ya kutoka vitambi wenye nazo.

Kipindi amekaa sebleni anaendelea kuwaza, alichukua cm akampigia mama yake, alimuambia kila kitu kinachoendelea, hawakuongea muda mrefu akakata cm, usingizi nao ulikuwa tayari unamuwinda, alitoka sebleni akaingia chumbani kwake kwa ajili ya kulala, hakuitaji kufanya chochote chengine usiku huo zaid ya kulala.....

Bi najma nae alikuwa ashapanda kitandani kulala, alifurahi sana kusikia mwanae amepata nyumba ya kuishi nzuri, aliamini mafanikio ya mtoto wake ndo furaha yake kubwa, alinyoosha mikono juu tena akamuombea mwanae kwa Mungu ili amuongoze katika maisha yake mapya....

Seid alivua nguo akaingia bafuni kuoga, alipomaliza alipanda kitandani kulala, kutokana na uchovu aliokuwa nao hazikupita dakika tano usingizi ulimpitia, kitanda alicholalia kilitosha kumfanya asihisi chochote kile, wala kugeuza ubavu ndani ya usiku mzima mpaka palipopambazuka....

Ilimchukua ugumu kuamka mwenyewe asubuhi, cm ilipoanza kuita ndo akawa ameshtuka, aliichukua kuangalia anaepiga nani, jina lilikuwa menega, alipiga macho pembeni ya cm kuangalia saa ngapi,  ilishakuwa saa tatu na nusu tayari, ,, Alitoa macho akapokea cm, kosa lake alishalijua la kuchelewa, kwani saa mbili alitakiwa awe kazini kutokana na kikao kilichokuwepo cha wafanyakazi wote, hivyo hakuitaji kuongea sana, alikata cm akaingia kuoga, alipomaliza akavaa suti ambayo aliivaa siku ya ndoa ya ticha kabla hata ya kwenda uingereza, hakuivaa tena toka siku hiyo ya ndoa,  alitoka nje akawasha gari akiwa katika muonekano wa kibosi, brifkes mkononi, alipofika nje ya geti akiwa ndani ya gari, aliliona gari dogo likiwa limepaki, ambalo lilikuwa pale kwa ajili ya kumuongoza...

Alisalimiana na vijana wawili waliokuwemo ndani ya gari hilo, kisha wakaanza kumuongoza kwenda katika jengo la kampuni....


Tukutane Sehemu ya 28