TAFUTA HAPA

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 26)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA 26

Akiwa katika mawazo mazito moyoni, Bi najma alimpiga jicho akamuuliza ,,, " Mbona unaniangalia, unawaza nini ? ,, kabla Seid hajajibu ilisikika honi ya gari ghafla kwa nje, walishtuka wote wawili kwani walikuwa hawana taarifa yoyote ya mtu yoyote kuja na gari.....

Ilipiga tena na tena Seid ikabidi afungue mlango aangalie nje kwa kuchungulia, aliachia tabasam baada ya kuona gari la rafiki yake hamad, Hamad alipomuona Seid alishuka akiwa pamoja na Sulaiha, Seid alitoka nje wakakutana wakakumbatiana, walijuliana hali kisha akawakaribisha ndani.

Waliingia bi najma akiwa ndo anamalizia kukunja nguo za mwanae na kuziweka kwenye begi.
aliacha kazi hiyo alipomuona hamad, alimfata taratibu akamkumbatia, huku akimuuliza hali yake, alimuachia akamwangalia Sulaiha nae akamkubatia kisha akawakaribisha na kuwaitaji wakae chini.

"Hawajambo huko nyumbani ,, Bi najma aliuliza baada ya kuwa tayari amesogea kitandani kulikokuwa na baadhi ya nguo ili amalizie kuziweka mahala pake.
" Mama huko hawajambo kabisa wanakusalimia sana ,, Hamad alisema kumwambia bi najma.
" Sulaiha mwanangu ujambo ,, alimwangalia sulaiha, akamuuliza hali yake kwa kiarabu.
" Ndio sijambo mama vipi wewe?
" Kama unavyoniona niko fiti ,, alisema akiachia tabasam.
" Naona uko kwenye usafi.
" Namuandalia kijana wangu huyu kwa ajili ya safari.

Bi najma alimaliza kukunja nguo akiziweka kwenye begi, muda huo chai ilikuwa jikoni inachemka, alimtaka Seid aende kuichukua, akawaomba wasubiri chai wanywe kwanza kabla ya kwendelea na maongezi mengine.

Seid alitoka akaenda mpaka jikoni, alichukua makaratasi, akatoa kisufuria kwenye mafiga kilichokuwa kinachemka, alikiweka pembeni kisha akazima kuni zilizokuwa bado zinawaka, alipomaliza akachukua sufuria akarudi ndani.

Walikunywa chai bila kupiga stori yoyote mpaka walipomaliza, Seid alikusanya vyombo akaviweka pembeni, bi najma aliwaangalia akiwa anafuta futa mdomo wake. ,,, " Aya sasa,, hapa mnaweza kwendelea na Stori ,,alisema, akiinuka chini ili akae kitandani.

Hamad alianzisha mazungumzo kwa kumtania bi najma, walicheka wakafurahi ndani ya dakika kadhaa wakitumia lugha ya kiarabu ili kumfanya Sulaiha nae afurahi, kwani alikuwa hasikii wala haongei lugha yoyote zaid ya kiarabu, kingereza na lugha za kwao.

" Mama tuachane na yote, kwanza kabisa nimekuja kukualika mamaangu, kesho kutwa ufike kwenye shuguli ya harusi yetu mimi na bibie huyu, tunafunga ndoa ,, alisema Hamad kumwambia bi najma.

" Ina maana rafiki yangu naondoka baada ya siku mbili unaoa? ,, Seid aliuliza kudakia maneno ya hamad.
" Yah kwa sababu muda wa kuondoka unakaribia na pale nyumbani ushakuwepo ugeni mkubwa wa ndugu toka huko.
" Na ndoa yenu itakuwa ya kizungu Wallah, maana haiko vile ilivyozoeleka, bibi na bwana bado siku mbili za kuoana na bado mnatembea pamoja hata ile ya kukaa ndani bibi hakuna? ,, aliuliza bi najma.
" Hapana mama ,, alijibu huku akiwa anatabasam kwa swali aliloulizwa ,, " ujue mama, hizo desturi naweza kusema zilikuwa kwenu wazee wetu, hapa unapotuona hatujakaribiana hata siku moja, tunaishi nyumba moja,  chumba chake na mimi changu, kama mtu na dada yake wakati ni wapenzi, hata hivyo kuna baadhi ya watu hawajaweza kukubali kama mimi na sulaiha ni wapenzi kwa tunavyokaa mpaka sasa...

Seid alishangaa kusikia maneno ya rafiki yake, alitamani kumuuliza kama kweli hajalala nae au ameongopa kulinda heshima lakini akamueshim mama yake.
" kweli hamlali chumba kimoja ina maana!? ,, bi najma aliuliza tena.
" Yah, tokea nitoke nae dubai hatujalala pamoja, nlimalizia kila kitu huko nije nae huku ili wazazi wangu wamuone, familia yao imeshiba dini, yeye mwenyewe ameshika dini, mimi pia dini imenikaa, upande wa familia yangu ndo usiseme, hivyo hatukuitaji kufanya tendo ambalo tunajua kabisa tutamkosea Mungu wetu...

" Duh ,, Seid alijikuta akilitoa mayoni mwake neno la Duh, kwani kama kulala na mwanamke yeye tayari tena zaid ya mara moja, ilikuwa ni mshangao mkubwa kwake, akijiuliza uwezo wa rafiki yake kukaa bila kulala na mtarajiwa wake kisa ndoa...

Taarifa aliyopewa bi najma ilikuwa ya ghafla lakini aliichukua kama ilivyo.

" La pili nimekuja kumsindikiza Seid mpaka Bandarini, kwa sababu kuna jamaa yangu nimempigia cm amesema kuna boaty moja tu leo inayoondoka saa saba na nusu, hivyo nkaona ili Seid asije kuchelewa nimfate, nimpeleke mpaka bandarini then!, mambo mengine ndo yafate.

" kiukweli nakushukuru sana mwanangu maana nlishajiuliza kama atawahi au laa,, ,, mwaamnangu unaona mwenzako anavyoonesha upendo juu yako!? ,, sii unafika huko unamsahau rafiki yako, amefanya mengi ambayo huwezi kumlipa, inabidi ukishafanikiwa umuandalie zawad nzuri umpatie kama asante....

Bi najma alimgeukia Seid akamwambia juu ya hamad, waliongea mengi ya furaha, seid alimuaga mara ya mwisho mama yake, Bi najma alitoa kila aina ya baraka kwa seid, rohoni mwake alikuwa na kila aina ya furaha, alimuomba sana Mungu aweze kumtangulia kijana wake, pia amuondoshee misuko suko itayoitaji kujitokeza njiani.

Kama ilivyokawaida ya wazazi hawaachi kutoa maneno ya silaha kwa watoto wao pindi wanapoenda mbali, Bi najma nae alimpa maneno ambayo kama mtoto usipo yasikiliza ndo msemo usemao ,, " asiefunzwa na mamae hufunzwa na ulimwengu,, hufanya kazi hapo.
Ilipofika saa tano na nusu, walimuaga bi najma wote watatu, Hamad alimuomba namba yake akamwambia atampigia cm siku ya shuguli na atafatwa na gari yeye ajiandae tu, alibeba beg  la Seid, huku seid akibeba kimkoba kidogo kilichokuwa na vitu vyake vya muhimu vyote, walitoka ndani wakaenda mpaka lilipokuwa gari, walisimama wakageuka kumwangalia bi najma ambae machozi yalishaanza kumtoka, alinyoosha mkono wa bai wakaingia ndani kwa ajili ya kuanza safari.

" Yaa Rabbi ,, mjaalie mwanangu salama na amani huko aendako ,, mwondoshee kila aina ya balaa la njiani pamoja na macho ya watu ,, Muweke mbali na husda ewe Mungu Wangu , mpe mafanikio ya haraka na umpe moyo wa kuwasaidia wasiokuwa nacho nshallah..

Gari lilipo kuwa limegeuza na kuondoka, Bi najma alinyoosha mikono juu kumuombea mwanae akiwa analia, aliingia ndani akafunga mlango, alisogea mpaka kitandani ambako alilala kuegesha ubavu wake ambao alihisi umechoka...

Speed ya mafuta ilisomeka 80 ndani ya gari kwa mbio walizotoka nazo shamba,  ndani ya gari walipeana maneno ya kufarijiana kuhusiana maisha na kadhalika ,, huku wakimuomba Mungu awakutanishe tena baada ya pale kabla ya kufa kwao....

" Hii ni historia ambayo ntaikumbuka sana Seid, na kama nkimpata mwandishi wa vitabu basi ntaitaji aiandike maana  inatosha kuwa story ya kuhuzunisha ,,  aliongea hamad akionekana kuwa bize na sehemu nzima ya kudrive.
" Kwa nini umesema hivyo ndugu yangu ,, aliuliza seid aliekuwa amekaa nyuma ya city za mbele.
" Kwa sababu, nkikumbuka tulikotoka, kisha leo maisha yanatufanya tutengane kaka, hapo ndo najikuta nkiyakumbuka sana maneno ya mwana kondoo mmoja wa jangwani.
" Ila nadhani Mungu ana makusudio yake, Tuombe tu yawe mazuri, Kwenye harusi tu hapo mi ndo nimechanganyikiwa, yani ifanyike nkiwa sipo mbona ni hatari hii!? ..
" Nna imani hutokuwepo, ila kivuli chako kitakuwepo.

Walicheka wote wawili aliposema hivyo, Sulaiha aligeuka akamuangalia Hamad.

" Mnaniteta ee! ,,
" Hapana mke wangu hatukuteti, nkutete mkalia nyonga yangu jamani!  ,, hamad aligeuka akamuangalia mtarajiwa wake na kumuondoa wasi wasi.
" Kwani Switty huyu rafiki yako mmetoka mbali sana ee! maana inaonekana mmeshibana ,, aliuliza sulaiha.
" Tena zaid ya sana, yani mimi na huyu ni sawa na mapacha wawili wa baba tofauti na mama tofauti.

Alikunja kona ya round ya bauti ya mjini, tayari walishafika bandarini, walisogea hadi sehemu zilipokuwa ticket wakakata ya kesh moja kwa moja, Walisonga mbele mpaka getini, ambako walishuka wote watatu hamad akamuaga swahiba yake mara ya mwisho kwa kumkumbatia, Sulaiha nae alimkumbatia akamtakia safari njema..

Baada ya kuwa tayari wamemaliza kuagana alipenya kwenye geti lililotumiwa na abiria wote waendao dar au pemba akiwa na kitambulisho chake mkononi, aligeuka akamuangalia rafiki yake, wakapeana bai ya mbali kisha akageuka tena na kuondoka.
Hamad na mwenzake waliingia kwenye gari wakaanza kurudi, alivumilia lakini machozi yalimtoka, kila picha ya siamini kama rafiki yangu anaenda sehemu ambayo ngumu kuonana tena ilipomujia usoni, Sulaiha alitoa kitambaa cheupe akamfuta machozi ya kiume mtarajiwa wake na kumliwaza kwa maneno mazuri....

" Eh Mungu muongoze huyu jamaa,, siamini kama umeniweka mbali nae aisee, nlitokea kumkubali kuliko mtu yoyote yule, kama isingekuwa nafasi nliopangwa na chuki binafsi nlizonazo juu ya nchi hii ya Tanzania, hakika ningeenda kufanya kazi dar na mimi,, Mungu akusaidie jamaa yangu....

Hamad aliongea macho yakiwa bado na machozi, alikanyaga mafuta mpaka sehemu za town akamnunulia baadhi ya vitu mpenzi wake kisha wakageuza kurudi nyumbani....

*******
Boaty ya Royal ambayo ilikuwa imembeba seid, baada ya saa moja na nusu ilikuwa inatia nanga katika bandari ya dar, abiria wote walianza kujiandaa kushuka wakiinuka katika viti vyao kuwahi mlangoni, seid nae alipoona watu wanaanza kuinuka, alibeba begi lake kubwa na kimkoba chake nae akainuka akasogea mlangoni, boaty iliweka nanga yake mawimbi ya taratibu yakiwa yanaipiga piga, wahusika walifungua milango abiria wakaanza kushuka wengi wao wakisema ,, " Al hamdulillah" ,, kwa kufika salama bila tatizo lolote.

kipindi seid yuko kwenye kingazi cha kutokea ndani alisimama kidogo akaangaza macho yake huku na kule, alitikisa kichwa akaendelea kushuka huku akiwaza moyoni mwake akisema,,, " Maisha ni mfano wa jiwe manga linalong'aa kama dhahabu, linawaongopea watu wenye akili zao kuwa ni dhahabu, lenyewe likiwa limekaa mahala pake likiwacheka, ukijifanya mjuaji ukalichukua umefeli, ukituliza tamaa zako umefaulu......

Alipiga hatua tano baada ya kuwa amemaliza kushuka akasimama,, alitoa cm yake akapiga namba za mwenyeji wake kuja kumchukua, aliombwa atembee mpaka nje atakuta gari leusi.
alipofika nje aliliona gari leusi pembeni yake akiwepo jamaa amevalia suti nyeusi, moja kwa moja alijua ndo hilo akapiga hatua mpaka kwenye gari lenyewe.

" Hello mr! ,, alimshtua jamaa jina mr jamson aliekuwa amesimama pembeni ya gari akikazana na cm.

Mr Jamson aligeuza uso mbio kwa kushtuka akamuangalia Seid, kabla hajaongea chochote.
" my name's seid ,, seid alijitambulisha.
" my name's jamson, jamson nae alijitambulisha, ,, zunguka uingie ndani ya gari ,, alisema huku nae akifungua mlango kuingia ndani.
" vipi hali yako boss ,, jamsoni alimuuliza hali seid ambae alikuwa anaenda kuwa bos wake ofisini baada ya kuwa tayari wamo ndani ya gari ,, Seid alishangaa kidogo kuitwa bosi, bila kufika hata ofisini.
" namshukuru sana Mungu ila bado sijapata hicho cheo ulichonipa ndugu yangu ,,
" Tayari bos kwa sababu bado kukalia kiti tu. ,, alisema jamson.

" James anasema usijipe cheo hali ya kuwa hujui kitachotokea dakika moja mbele yako, hivyo nifikishe ofisini kwanza, na hilo jina halitakiwi kuitwa mzarendo kama mimi.....

Walitoka eneo la bandari wakiwa wanapiga stori za hapa na pale kujuana, mpaka walipofika maeneo ya posta ndani kulikokuwa na jengo kubwa la ghorofa nane ambalo ndo kampuni ya kufanya kazi seid...
alipofika waliingia upande wa ndani wakapaingia kwenye lift kuelekea ghorofani.

" Thnk you god ,, baada ya kusota muda mrefu hatimae naenda kuwa bosi wa jengo lote hili, Dah

aliwaza kipindi anapanda ngazi baada ya kutoka kwenye lift akiongozwa na jamsoni njiani akiwa anakutana na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na kuwapa hi ya mbali mbali huku nao wakimkaribisha.

" Sarah, bosi wetu mpya umemuona? , aliuliza dada mmoja aliekuwa na mwenzake wakishuka chini baada ya kupishana na seid.
" ndo bosi wetu mpya huyu !? ,, sarah aliuliza kwa mshangao.
" ndio nlisikia data za chini chini kamaliza elim ya mastaz uingereza.
" na alivyo mzuri sasa mbona kesi hizi jamani.

haaloo dadi ,, waliachia kicheko cha pamoja, seid alifika kwa mtu ambae amepewa umeneja wa kampuni hiyo aliekuwa anatakiwa kumtambulisha, wafanyakazi wote waliitwa ndani ya muda mfupi, wakaingia katika ukumbi maalum wa kufanyia vikao, wake kwa waume walifika ukumbini na kukaa kwenye viti vyao, huku seid nae akikaa pembeni ya mwenyeji wake ambae ni meneja wa kampuni mr mtikira.

" Ndugu zangu hiki ni kikao cha ghafla hapa ofisini, kampuni yetu imekaa muda mrefu kidogo tokea kuanzishwa kwake, bila kuwa na msimamizi maalum na ikawa kampuni ya kuwa katika hali ya mterereko, ila sasa nadhani mambo yote yataenda sawa baada ya wamiliki wa kampuni ambao wanaishi Uingereza kumkabidhi kijana huyu kampuni ambae ni mpya katika macho yetu anaitwa Seid, nadhani  tulimuona kupitia mitandao ya intarnet katika Email zetu na website ya kampuni alipokuwa anakabidhiwa mikataba yote ya kampuni huko Uingereza. ,, Bosi wetu karibu sana, hii ndo kampuni yetu, tumejaribu kuiendesha vizuri tukishirikiana na wamiliki, ila sasa nadhani tutegemee mambo mazuri zaid toka kwa bosi wetu, mkurugenzi wetu, kijana wetu, ndugu yetu, karibu uwasalimie wafanyakazi ikiwezekana wakusikie sauti yako, baada ya hapo kila mmoja ataendelea na kazi yake kisha nikupeleke ofisini.

mr mtikira alisema akiwa amesimama kuwaambia wafanyakazi waliokuwa wamemuangalia kumsikiliza kwa makini, baadhi ya wafanyakazi wakitupa jicho mara moja kumwangalia seid. ,, alipomaliza alifungua chupa ya maji kwa ajili ya kunywa, alikaa kwenye kiti seid nae akasimama akionekana kuwa na uoga flan ndani ya moyo wake.

" Sina mengi ya kuongea zaidi ya kuwasalimia ndugu zangu wote ntaokuwa nao hapa, ,, Namshukuru Mungu ambae kwa uwezo wake nimefika hapa ,, pia ntakuwa mkosefu wa adabu, kama sitomshukuru mamaangu, aliehakikisha kijana wake napata elim iliyonifanya leo nakuwa hapa, Nashkuruni sana kwa kunipokea, ntakuwa nanyi katika hali zote za kikampuni.. mimi ni mpenzi wa kusoma vitabu vya watakatifu waliokuwa wanajua kuyatunga maneno yakatungika,,, Ulihangaika kwa ajili ya kazi, umepata kazi piga kazi, na usije kuichezea kazi ukaachishwa kazi ,,, hiyo ndo kauli mbiu yangu kubwa, tueshimiane tukiwa kazini, kujuana tuweke pembeni tupige kazi, tukiwa nje ya kampuni mambo yote yanaweza kufanyika, Asanteni sana.

alikaa chini baada ya kumaliza kuongea, wafanyakazi walipiga makofi kwa maneno yake ya hekma, wengi waliamini sasa mambo shwari kutokana na kijana mwenyewe kuwa msomi, akionekana kuwa mstaarabu na mwenye kiu ya kuongoza kampuni.

kila kitu kilipokuwa kiko tayari, wafanyakazi nao wakipewa nafasi ya kujitambulisha kwa seid, wote walisimama katika viti vyao, wakapeana mikono, wengine wakimkumbatia kabisa seid, mtu wa mwisho alikuwa msichana mrembo ambae alitambulishwa kuwa ndie Secretal wake, moyo wa seid ulicheka kuona atakuwa karibu na bint mzuri, alichukuliwa na meneja wakaanza kutembea tembea kuoneshwa mazingira yote ya jengo la kampuni, huku wafanyakazi wote wakienda kwendelea na majukumu yao makundi kwa makundi wakimdiskasi seid.

" Estar mbali na ubosi huyu kaka mzuri ee! ,, alisema dada mmoja aliejulikana kwa jina la rightness kumwambia mwenzake.
" Yani hii mi naona tumeletewa shida, mbali na uzuri lile body umeliona kwanza? ,, yani mimi nlikuwa pale lakini mawazo yangu yote yakimuwaza mwanamke anaekuwa na huyu kijana kwenye mambo flan anajisikiaje, kifua kule, mkono mkono, sura yenyewe Heee!!
......

" Mage naona wazungu wameamua kutuletea hand some boy ,, dada mwengine akimwambia rafiki yake mage.
" Akyaaamungu yani kaka anavutia hadi raha, alafu anaonekana katulia.
" Um,, kutulia,, hivi uliwai kusikia kijana mwenye pesa anatulia wewe? ,, si unamuona vile kwa kuwa hajazoea, ngoja akizoea aanze kuvua vua vichupi kampuni nzima?
" Na hivi alivyo hand some mwenzangu akiamua anavivua vya wengi humu maana duh,  Ila ukweli yuko vizuri, yani hata ukiwa umetoka nae lanch ukiongozana nae unasikia raha na kujihisi uko na kidume kweli.
.........

" ndugu yangu bosi umemuona !? ,, kundi lengine la vijana wakiambiana.
" nimemuona kaka.
" kijana mbichiiiii, ndo anakuja kuwa bosi  wakati watu na vitambi vyao na ndevu zao nyeupe wapo hapa ofisini, Elim haina adabu kaka, yani mtu ana ndevu zake kitambi kule anaenda kuchukua mshahara kwa kijana anaeweza hata kumzaa.
" Ndo hivyo ndugu, kama uliingia chuo ukapita shot kat ulitegemea nini? lazima ukubali,  sisi wengine tulioishia form six tutaishia kushika visukani vidogo dogo tu huku.

Yalikuwa maneno tofauti yakizungumzwa na watu tofauti tofauti kumwongelea seid, meneja alimzungusha eneo lote la kampuni, mshangao mkubwa ulikuwa kwa seid kwa namna kampuni ilivyokuwa kubwa, moyoni mwake akiwa na swali la ,, " yote hii itakuwa chini yangu ?.....

" Ina maana meneja wafanyakazi wale tu ndo wanafanya kazi kwenye jengo hili lote? ,, aliuliza huku wakiingia kwenye lift kurudi juu baada ya kuzunguka kwa muda mrefu hadi chini.
" Hapana,, wanaingia kwa shift, hawa ndo walioko kwa jioni hii, nadhani kesho asubuhi ndo utaanza kazi rasmi ukiwa tayari umepatiwa kila kitu, kesho hiyo hiyo wafanyakazi wote wataingia asubuhi kwa ajili ya kikao, ni wengi sana bosi.

Hakujibu kitu, walipanda kwa lift mpaka ghorofa ya sita, walienda moja kwa moja mpaka kwenye room ambayo ndo kuna ofisi yake, nje room yake alimkuta bint ambae ndo secretal wake aitwae Sasha, walisalimiana akafungua droo akatoa funguo, aliwakaribisha huku akifungua  mlango wa ofisi ya Seid, wote watatu waliingia ndani, Seid alishangaa kuiona ofisi ilivyo nzuri ya aina yake, aliiangalia bila kuamini kama muda mchache ujao ataimiliki yeye, atakalia kiti kilichoko katikati ya meza ya kifahari iliyokuwa na kila kitu, hakuweza kuvumilia macho yalianza kumwaga machozi ya furaha, moyo wote ulimwagika, alitoa kitambaa kujifuta futa lakini hayakuzuilika, ukawa mshangao mkubwa kwa mr mtikira pamoja na Sasha waliokuwa pembeni yake.


Tukutane Sehemu ya 27