TAFUTA HAPA

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 18)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: Seid Bin Salim.

Sehemu ya 18

Mama yangu anaitwa Yula'ina Bint Qasim ila alifariki kipindi mimi nna miaka kumi na tano, ,,,,,,,Raya alijibu na kumuacha bi najma katika wakati mgumu wa mshangao.
"Mama yako anaitwa nani!? ,, aliuliza tena bi najma akiwa kama bado haamini alichokisikia.
" Anaitwa Yulaina bint Qasim mama.

Bi najma machozi yalianza kumtoka hapo hapo, hakuitaji kuamini kile alichokisia, Hamad alishtuka kuona mama analia baada ya kutajiwa jina, huku seid nae akianza kupata picha nzima, moja kwa moja bila hata kuambiwa akajua Raya ni dada yake.

" Eh Mungu nakushukuru kwa kuniogoza, kuingia kwenye mausiano na raya, sikubahatika kulala nae.

Seid maneno yalimtoka, yaliyowafanya hamad na raya wakae njia panda bila kujua nini kinaendelea, kicheko kilibadilika kuwa huzuni hasa kwa bi najma, alimuangalia sana Raya, akibinya binya macho yake kuzuia kilio ambacho kilikuwa kinamuandama muda huo bila kuzuilika.

" Mama!, Ebu tuambie mbona mmebadilika ghafla mamaangu, Seid vipi?

Hamad aliongea kwa mshangao, alimuangalia mama, machozi yalikuwa tayari yanamtoka uso wake ulishabadilika, kugeuka kwa Seid akamkuta ameinamia chini akitikisa kichwa kumaanisha anasikitika.

" Mbona mnatuchanganya jamani!, tatizo  nini? ,, aliuliza tena Hamad akionekana na yeye kuchanganyikiwa.

" Raya na Seid ni mtu na dadaake.
Aliongea bi najma, hamad alitoa macho ya mshangao , msemo wa "What!?? ulitoka upande wa Raya.

Raya alimuangalia Seid bila kummaliza akiwa amebadilisha sura yake katika muundo wa kulia.
" Mama unachokiongea ni kweli?

Aliuliza huku hamad akiwa  katika hali ya sielewi, ,,, Bi najma alimuangalia Raya akiwa anajifuta futa usoni kwa kanga yake aliyokuwa ameivaa...

" Mama yako mnene ana asili ya kiarabu? ,, alimuuliza.
" Ndio mama! ,, Alijibu Raya.
" We ni mdogo wake Seid ,,, mimi nlikuwa mke wa Soud, na mwanzo kabisa tuliishi kwenye nyumba hii hii kabla ya kupata mali.

" Ooooh My God!  ,, Raya alisema akipeleka mikono yake kichwani.

Huzuni ilitanda kwa muda mfupi, walizidi kufahamishana mpaka wote wakaelewa, Raya kila alivyofahamishwa alizidi kufahamu kweli seid ni kaka yake, mwisho bi najma alimuuliza Raya mama yake kitu gani kilipelekea kufariki.

" Mama angu alifariki kwa presha baada ya fumfumania baba.
" Na sasa hivi unaishi na nani.
" sasa hivi naishi na mama yangu wa kambo anaitwa sauda...

ukimya kidogo ulipita, raya alikuwa analia kama mtoto, huku seid akiwa ameinamia chini. Hamad aliondoa ukimya akawaomba kukabiliana na kila  kilichotokea, Ndoto za seid kuwa na raya kimapenzi zife, huku akiwaomba washirikiane kama ndugu wa pamoja, bi najma awachukulie wote wawili kama watoto wake, Huyo Masoudi wamuache kama alivyo siku yakimkuta ya kumkuta atabadilika.

" Mama ,, Raya alimuita bi najma huku akipiga magoti, ,, Naomba vita uliyonayo juu ya baba usiichanganye na kwangu mimi, mimi ni mtoto sijui nilitendalo, naitaji kuongozwa na wazee wangu lakini baba yangu mwenyewe ndo hivyo hashugulikii juu yangu, Naamini utakuwa na kinyongo juu ya baba, Ila naomba mimi unichukulie kama mwanao, nadhani ntafarijika sana na ntajiona kama mpya kwenye dunia hii, Endapo utaniruhusu nikuite mama.

Raya aliongea kwa huzuni, Bi Najma alinyanyuka kwenye kisturi chake akamnyanyua Raya akamkumbatia, Alimuomba seid nae anyanyuke, walikumbatiana wakaunda familia moja bila kujali mama yake raya alifanya nini kwa bi najma wala bila kujali masoud kamfanyia nini bi najma.

Hamad alifurahi sana kuona namna walivyokumbatiana, aliachia tabasam huku akisema " Inapendeza sana.

"Kuanzia leo heshimianeni kama mtu na dada yake, msije kugombana wala kutofautiana, kama mlivyokuwa mkiishi mwanzo ishini hivyo hivyo ila jueni mmechangia baba.

bi najma alisema baada ya kukaa kwenye kisturi chake Seid na raya wakiwa tayari nao wamekaa chini, Seid alifurahi upande mwengine aliumia kwani raya ndo msichana wa kwanza aliekuwa ametokea kumpenda katika maisha yake, aliamini wataendelea kupendana lakini sii kimapenzi tena.

Baada ya nusu saa mbele hamad na raya ilibidi waage  ili warudi mjini, Seid alibaki na mama yake huku raya akiahidi kuja kila siku kwa ajili ya kutembea.
Safari ya hamad na raya kurudi mjini ilianza, waliongea mengi wakiwa ndani ya gari hasa kuhusu tukio lililotokea, walipofika mjini walienda moja kwa moja mpaka katika paking za magari ya chuo, Raya alishuka akaingia kwenye gari lake wakawa wameachana hapo kila mmoja kwenda na safari yake.

Binti soud alipofika nyumbani alipitiliza moja kwa moja hadi chumbani kwake, alitupa mkoba kitandani kisha nae kujitupa, kichwa chake kilijawa na mawazo mengi akiwaza kilichotokea, ghafla alihisi kumchukia baba yake zaid kwa matendo aliyoyafanya kwa bi najma pamoja na mama yake, japo tokea awali alikuwa akimuogopa kutokana kuwa mkali kwake.

" Mwanangu mimi wakati wowote naweza kupoteza maisha kutokana na mambo anayonifanyia baba yako.

akiwa amelala kitumbo tumbo aliyakumbuka maneno ya mama yake aliyomuambia....

alijikuta anaanza kulia huku akikumbuka baadhi ya mateso aliyoyashuhudia akipatiwa mama yake ikiwemo kupigwa, kubamizwa ukutani, kuletewa mwanawake mbele yake na mengine mengi.

" Nlidhani hayo yalimkuta mama angu tu, kumbe na mamaangu mkubwa pia?, kwani babaangu ni mtu wa aina gani jamani, Eh Mungu nisaidie na nakuomba unijaliie nimalize masomo yangu ikiwezekana niende kuishi mbali.

Ghafla mama yake wa kambo ambae ni mke mpya wa baba yake aliingia chumbani, Raya alijifuta futa machozi, aliulizwa hali wakaongea mawili matatu kisha akamuitaji aende kula sebleni.

" Inabidi umpigie baba cm uniagie nataka kwenda kilimanjaro.

Aliongea Raya kumwambia Swaumu ambae ndo mama yake mdogo baada ya kutoka chumbani na kuwa kwenye meza ya chakula kwa ajili ya kula.

" Kwenda kilimanjaro kufanya nini?
" Jamani mi si mwanafunzi au ? ,, Raya alionekana kukereka na swali aliloulizwa.
" Sawa mwanafunzi lakini kumbuka bado upo kwenye imaya ya wazazi wako, kama mlezi wako nna haki ya kujua unaenda kufanya nini na usalama wako pia.
" Basi naenda kusoma, mpigie baba cm kesho kutwa ndo nataka kuondoka.

Swaumu alimuangalia akashusha pumzi huku akipeleka macho chini " Sawa ntampigia nimueleze.

Alipomaliza kula aliingia ndani kupumzika, alishazoea kumpigia seid cm hivyo hakuona vibaya mda huo akimpigia waongee japo tayari ni kaka yake, waliongea machache baada ya kuipiga ikaita na kupokea, walitaniana kisha wakakata cm wote wawili wakifurahi.

" Damu yangu ilipatana na damu yako siku ya kwanza tu nlipokuona Seid, kumbe ni kakaangu!, Ama Mungu mkubwa, je mfano tungeshavuana nguo? sipati picha hapo ingekuwaje dada na kaka wamefunuana duh.

Raya aliongea peke yake akijitania mwenyewe baada ya kukata cm, aligeuka huku na kule kitandani mpaka usingizi ulipompitia.

Alilala mapema kwa uchovu aliokuwa nao, Seid na mama yake nao walipumzika mara tu baada ya kumaliza kula ,, huku Hamad akipitia baadhi ya vitabu vya methali na misemo nje ya nyumba yao (ubarazani)

" Nakuona mwanangu unapitia mambo ya Nuktas.

Alitokea baba yake mzee shaibu akiwa na grass ya juic mkononi mwake, alikaa kwenye kiti kilichokuwa pembeni ya kiti alichokalia mwanae.
" Yes baba, nawapitia wazee wakubwa hawa maana ndo furaha yangu.

" Ni vizuri ,, nakumbuka ulinipigia cm kipindi uko chuo kuwa umeplan kwenda mlima wa kilimanjaro, ulikuwa sirias au ulitania tu?.
"  Hilo jambo ni kweli baba, na ni kesho kutwa tu kwa sababu naitaji kwenda kuupanda kabisa, kutembelea na bunge pia.
" Good aidia, una kampani yoyote au mwenyewe.
" Niko na Seid pamoja naa rafiki yangu mwingine.
" basi mimi nikutakie safari njema kwa sababu ntakuwa na safari siku mbili hizi.

" Usijali baba.

Mzee shaibu alimuacha mwanae akiendelea kupitia vitabu yeye akaingia ndani kulala, Hamad nae hakuendelea kukaa sana, alipoona muda unaenda alifunga vitabu akaingia chumbani kwake kulala.

Baada ya siku moja mbele asubuhi na mapema ya siku waliyokuwa wameahidiana kukutana ili kuianza safari yao ilifika. Seid kwa kuwa alikuwa anakaa mbali, ilibidi apande dala dala alfajiri ili saa moja awe mjini ambapo atakutana na wenzake. Ilipofika saa moja na nusu wote watatu walikutana darajani wakakodi tex iliyowapeka hadi airpot kwa ajili ya kupanda ndege iliyokuwa inaondoka saa mbili na nusu kuelekea Dar, ili wakishafika dar wapande mabasi ya kuelekea Kilimanjaro.

Seid kwa mara ya kwanza tokea azaliwe akapanda ndege kupitia mikono ya Hamad, aliwaza na kuwazua bila kujua nini amlipe rafiki yake kama shukrani kwa kutumia pesa zake kuhakikisha nae anaonekana mtu katika watu. Pia ilikuwa ni kwa mara ya kwanza anafika dar katika jiji analolisikia kila siku kuwa gumzo Tanzania.  ,,, walifika dar majira ya saa tatu kamili, Hamad alishapasua kidogo pande hizo zote, aliwatoa uanja wa nyerere na kuwaingiza kariakoo ili waone mandhari ya jiji kwanza, Seid alijikuta anaingiwa na uchizi wa wanawake aliokuwa akiwaona kila kona bara barani wakiwa ndani ya nguo fupi huku wakitingisha walivyojaaliwa nyuma...
Walifika kwenye hotel ili  kupata Chai, hotel hiyo ilikuwa imetawaliwa na wazungu wahindi pamoja na wabongo, wengi waliipenda kwa mandhari yake, ilikuwa ni hotel yenye hadhi ya kimataifa namna ilivyokuwa imejengwa, kila mtu mwenye pesa zake alitamani kula katika hotel hiyo,

" Ndugu yangu Seid ukisikia bongo, hii ndo bongo ,, Hamad alimsemesha Seid baada ya kukaa kwenye kiti.
" Hata mimi naona.

Alijibu kwa mkato seid, macho yake yalikuwa yametazama kwa mbele, yalifanikiwa kugongana na mtoto wa kike aliejazia kila sehemu za mwili wake,Huku akiwa amevalia kanguo kepesi kalikoonesha baadhi ya maungo yake, nyuma vitu vikitingishika.

mambo kama hayo hakuwai kuyaona tokea azaliwe ndo kwanza siku hiyo, kitu kilichomfanya atumie muda mrefu kuyashangaa, alizoea kuwaona watoto wa kizanzibar wakiwa ndani ya nguo za stara, zinazowafanya maungo yao yasionekane..

mhudumu alikuja sehemu walipo kwa ajili ya kuwaudumia, Seid alipomuangalia mhudumu mwenyewe nguvu zote zilimuishia, Alipopatiwa maagizo na kuwapa mgongo akielekea sehemu ya mapishi namna makalio yake yalivyokuwa yanapishana ndani ya sketi fupi nyeusi, Seid alibaki ameduwaa kama mtu alopigwa shot, ghafla coment ilipita moyoni mwake " Eh E E E E E E! kweli tembea uyaone, hivi kuna mwanaume anamiliki mzigo kama huu kweli!.....

akiwa hajamaliza kuwaza aliangalia nyuma ya hamad akakutana na sura nne za masistar duh wa mjini, macho yalimtoka kila aliemwangalia nyuma kajazia, alizidi kudata kijana seid, pozi zote za kukaa zilimuishia, alitamani wasiondoke eneo hilo ili asafishe macho kwa kuviangalia vizuri, ambavyo anadhani hakuwai kuviona tokea kuzaliwa kwake.

Wasichana warembo waliokuwa wanatembelea eneo hilo kwa ajili ya kupata chai walizidi kumchanganya sana Seid, macho yake hayakutulia sehemu moja, chai yenyewe imparia, Haikuwa peke yake bali hata Raya mwenyewe japo ni mwanamke lakini alijikuta anapitisha baadhi ya maneno ya kuisifu kazi ya mungu katika uumbaji, huku Hamad akiyaona ni ya kawaida kwa sababu si mara ya kwanza kuyaona mambo hayo, hakuitaji kuyapa nafasi yampagawishe, alipiga chai yake akiwa anaangalia sehemu ya meza, Seid macho yalitanga tanga huku na kule kuangalia kila mashine inayoingia  na kutoka pale.

" Kiukweli Nkimaliza kusoma Tu nakuja kula ujana huku, Huku kunaonekana kuwa na Raha za aina yote,  Lazima ntarudi nkiwa peke yangu tu siku moja ngoja nizipate..  Heeeee!!!! Ona mitoto hiyo utafikiri haijaumbwa Jamani!! ,, au malaika hawa?  ,,, Sipati picha ukiwa na litoto kama hilo kitandani mbona raha!, yani hadi mwili unapata vibrate kumuona tu heee.

Aliwaza moyoni macho yake yakizunguka huku na kule, Hakuwai kufanya mapenzi tokea atoke tumboni mwa mama yake na alikuwa hafikirii kutokana na mazingira ya Zanzibar lakini alijikuta anaingiwa na tamaa za kulala na mwanamke ghafla kutokana na vyombo anavyoviona, Walimaliza kunywa chai na kutoka eneo hilo, Kipindi wanatoka nje bado seid hakuacha kumuangalia kila mwanamke mzuri aliemuona mbele yake, au hata kugeuka alipohisi aliempita mbeleakielekea nyuma uenda kajazia vya kutosha.

Tayari alishaweka nadhiri ya kurudi bongo endapo atapamaliza kusoma na kupata kazi nzuri inayomuingizia pesa, ili kuja kula kwanza ujana kutokana na yale aliyoyashuhudia, imekuwa ni kwa muda mchache sana lakini mambo aliyoyaona ameshindwa kuyapatia majibu.
Walifika sehemu ya kuvukia bara bara, kidogo kulikuwa na magari mengi mengi ikabidi wasimame kwanza, Seid alipotupia macho upande wa pili wa bara bara akamuona msichana mzuri nae anasubiri kuvuka, magari yalipoisha ilibidi wavuke huku na mdada wa upande wa pili akivuka, Seid akiwa katikati ya bara bara alijisahau akajua bara bara za bongo ni sawa na za zanzibar magari si mengi, alimwangalia mdada huyo alivyo mzuri mpaka alipompa mgongo, akageuka na nyuma kumwangalia namna alivyojazia bila kuangalia anakoelekea, "" Jamani! hawa wanafanya makusudi au ndo walivyoumbwa hivi mbona shida? ,,, mawazo yalipita akilini mwake baada ya kumuona dada wa watu alivyofungasha nyuma,  Honi za mfurulizo za gari aina ya fuso  zilipiga gafla, Zilipekea kila raia aliekuwa eneo hilo kugeuka,  kabla ya seid kuonekana kuvuka lilipita alipokuwa amesimama kwa kasi, na kumuacha kila mtu katika swali la kitendawili cha mshangao, huku watu wakishikilia midomo yao wengine " Mungu wangu " kwa  kile wanachokiona.

Tukutane Sehemu ya 19 hapa hapa.