Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mw/Mtunzi: SEID BIN SALIM.
SEHEMU YA 17
Alishangaa sana kuona mtoto wa kike anampatia funguo akimanisha aendeshe yeye, aliichukua akaingia kwenye gari huku raya nae akizunguka upande wa pili, aliwasha gari akageuza na kuanza kuelekea chuoni huku wakipiga stori za hapa na pale.
Walipofika katika geti la chuo, Hamad nae alifika muda huo huo, walionana kupitia vioo vya mbele, kila mmoja alikuwa amemkumbuka mwenzake kutokana na kuwa mbali kipindi cha wiki nzima, ilibidi washuke wote seid na hamad, wakakutana kati kati ya magari yao na kukumbatiana, huku Raya nae akitoka kwenye gari na kumkumbatia Hamad.
"I think ni mapenzi ya Mungu tumeonana tena. ,,aliongea hamad akiwa na furaha za kumuona rafiki yake kipenzi.
"Yah, Bila yeye tusingekutana, Hawajambo huko?.
"Kiukweli tunamshukuru Mungu mamangu vipi hali yake.
"Anakusalimia sana, unang'aaa tu rafiki yangu
" Acha mambo yako bhana hayo hihihiiiii
Walikumbatiana tena kwa furaha, wakasogea pembeni wakasimama na kuongea ndani ya dakika tano na zaid, Seid alitumia muda huo kumueleza mausiano yake na Raya, Hamad alifurahi sana kusikia kuwa ni wapenzi, huku akimtania kwa kumwambia chunga sana baba yake sii mtu mzuri, maneno yaliyopelekea kuachia kicheko wote watatu kisha wakaingia ndani ya magari, wakapita na kwenda chuoni.
*******
Ticha alijiandaa muda huo huo ili aende kazini, alivalia kila kitu Rahma bado alikuwa amelala, baada ya kumaliza alisogea kitandani akamkiss mkewe kwenye paji la uso, kiss lililopelekea Rahma kushtuka usingizini.
"Morning my Wife ,, alimsalimia mke wake
"Morning too ,,aliitikia kwa sauti ya usingizi.
"Mke wangu nishakuandalia kila kitu kuhusu chai, utaamka na kupata kifungua kinywa, mimi naenda kazini.
Rahma alishtuka aliposikia habari za kwenda kazini.
"Unaenda kazini!?
"Yah beib si unajua leo jumaa tatu.
"Um! tunaenda wote ,, alisema rahma kumwambia mmewe.
Mungu wangu kaanza ,,,,,, alisema moyoni mwake ticha, aliposikia maneno ya mkewe.
"Mke wangu acha masiara basi jamani, twende wote wapi na hali yako hiyo!?
"Mawili, twende wote huko kazini kwako au ubaki hapa nyumbani, maana leo nataka kukaa nakuangalia tu ndo furaha yangu, tena tukienda wote si unaingia darasani kufundisha mimi unaniacha nje, tunaingia wote darasan na mimi nasoma.
Ticha alijikuta anacheka kwa uchungu aliousikia ghafla, alimjua vizuri mkewe akishaamua kitu ndo kaamua, ilikuwa ni ngumu sana kuacha kwenda kazini siku hiyo kutokana na prosses alizokuwa nazo.
"Ok sawa jiandae basi twende ,, aliongea ticha kwa unyonge.
"Wao! gud husband ndo maana nakupenda mme wangu.
"Eti ee
"ndio.
Wee ni tese tu zamu yako itafika ,, alisema moyoni baada ya kumwangalia mkewe anavyoinuka kitandani.
Rahma aliingia bafuni kuswaki, akavalia dela na kujitanda kichwani.
"Nshamaliza twende.
"Na Chai je.
"Wewe!!! ,,alimnyooshe kidole alipoambiwaa habari za chai ,,,,, Naomba usinitibue, ningekuwa nataka si ningekunywa kwani sikioni!? twende huko.
walitoka nje ticha akabonyeza funguo ya gari ili kuiwasha, Rahma aliomba apewe funguo ili aendeshe yeye, Ticha hakuweza kumkatalia kwa sababu kasheshe yake tayari alishaijua.
Rahma alikanyaga mafuta mpaka katika paking za magari zilizopo pembezoni mwa shule ya sekondary Green, iliyokuwa karibu sana na chuo kikuu cha Zanzibar, walipaki gari wakatembea mpaka Shuleni.
Walimu wenzake walishangaa kuona Ticha anakuja na mkewe, wengi wao walishiriki katika siku ya ndoa yake hivyo walikuwa wanamfahamu vizuri.
"Heeee profesa mbona anakuja na mkewe vipi ,,alisikika mwalimu mmoja aliejulikana kwa jina la Bi Husna akisema kwa mshangao.
"sijui ila nna wasi wasi itakuwa mimba hiyo, si unaona tumbo lile.
" Mimba? ,,, bi husna aliuliza tena kwa mshangao.
"Um bi husna!, hujabeba mimba nini weye?
"nimebeba ila nashangaa kunambia mimba.
"basi haijakupelekesha, ngoja umuulize akifika, nakumbuka kipindi nna mimba ya makame mme wangu nliitaji niongozane nae hadi kazini kwake, alipokataa namfungia milango yote analale nje.
Ticha alifika akasalimia ,,, Rahma nae aliwasalimia, akapatiwa kiti akae, Ticha alimuomba mke wake aende kuripot ofisini mara moja kisha anakuja.
"Ok sawa ila nna njaa.
Alimkubalia na kumwambia njaa inamsumbua, ticha alichoka baada ha kusikia hivyo, aliachia pumzi kubwa akashika kiuno.
"Mke wangu jamani mbona unataka nilie mbele za watu mimi!,si nimekuwekea chai tena nzuri ukakataa kunywa wewe au sio wewe.
Rahma alimwangalia akionekana kukasirika, aliinuka kwenye kiti akasimama na kumnyooshea kidole.
"Wewe!! ,, Wewe Rajabu wewe!,,,,, Naomba usitake kunichefua sasa hivi, naitaji kula.
"Lakini mke! .....
"Lakini nini staki nataka kula! we vipi?.
Ticha hakuwa na namna zaid ya kukubali, alitamani kulia mbele ya walimu wenzake, walimu wote walichoka kwa kitendo alichokifanya Rahma, alitoka taratibu Ticha mpaka restaurant, akaagiza Supu na chapati mbili kisha akarudi.
"Mbona mikono tupu?
Rahma alimuuliza baada ya kufika akiwa hajabeba kitu mikononi.
"Vinakuja nimeagiza.
"umeagiza nini?
"Supu na Chapati.
Rahma aliinuka kwa ajili ya kwenda kujisaidia akimuangalia mmewe, Ticha alibaki akiwa amesimama akionekana kama mtu aliedata na maisha, Baada ya kutoka walimu walimuuliza kuhusu mkewe.
"Kiukweli nyie acheni tu, kwa hali hii najikuta nkijuta kuoa, Yani tokea mimba ifikishe miezi mitano kila siku nalia mimi tuuuuu akyamungu sionewi hata huruma mwenzenu, hiyo miezi miwili ilobakia naiona kama mwaka kwangu.
walimu walimpa pole baada ya kuambiwa hali halisi, baadhi yao walizijua mimba za aina hiyo zinavyosumbua, Supu ilifika ikawekwa mezani, Rahma alipokuja alionekana kufurahi sana, ticha alienda ofisini kwa ajili ya kuripot huku Rahma akiendelea kula.
Muda wa Ticha kuingia darasani kufundisha ulifika, Ilibidi aingie na mkewe darasani, Wanafunzi wote walitoa macho, alimkalisha mkewe kwenye kiti wanachokalia walimu wakiingia class, alisimama akawaangalia wanafunzi na kuachia tabasam, wengi walikuwa wamemzoea Ticha wao kuwa mtu wa mashairi pamoja na misemo, Methali mafumbo na maandiko ya wandishi wa vitabu kama william, Christopha, Rose na wengine.
" Nadhani mnamkumbuka Hollywoma mfaransa nliewai kuwapeni kisa chake siku moja ,, alisema kuwaambia wanafunzi.
Wanafunzi wote waliitikia ndio ,, mkewe nae akasema ndio ili tu kumkera. .. Ticha aligeuka akamuangalia.
" usintolee macho fundisha huko... ,, Rahma alisema akitabasam.
Yani ungekuwa unajua unavyokera wewe mwanamke, basi tu ,, alisema moyoni ticha, kisha akawageukia wanafunzi.
"Anasema katika kitabu chake cha misemo "Woman, ,, Mwanamke, ,, ni mfano wa kitambaa kizuri cheupe kinachobadilika rangi kutokana na tone la rangi litaloanguka kwenye kitambaa hicho, Bora kinyonga kinachobadilika rangi kila siku, Kuliko mwanadam anaebadilika siku na siku.
Rahma alikuwa yuko anaangalia cm yake aina ya samsung, Ticha alimwangalia kisha akawaangalia wanafunzi, alitikisa kichwa na kusema "Bure hamna kitu kisa!!! ,,,,,, akipiga mfano wa mimba.
Wanafunzi wote walitabasam huku wengine wakicheka kabisa.
Rahma alishtuka akainua paji lake la uso, ticha alipomuona akawaambia wanafunzi ,, " fungueni vitabu tusome huku akiwa tayari amempiga fumbo mkewe bila kujua.
*******
Mausiano mazuri yaliendelea kuwepo kati ya Seid Raya pamoja na Hamad, huku wakiendeleza mwendo wao ule ule wa kuhakikisha wanakuwa bora zaid darasani mbele ya wanafunzi wenzao.
Kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo raya kwa seid, aliamua kumpatia zawad ya cm aina ya LG Tach, Seid alifurahi sana baada ya kupatiwa zawad hiyo, waliyaweka karibu mausiano yao kuliko kitu chochote kile, wanafunzi wote waliokuwa wanasoma nao waligundua kuwa wao ni wapenzi kutokana na jinsi walivyokuwa wakiyanika mapenzi yao...
Baada ya miezi miwili Rahma alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume, Ticha alifurahi sana kwa sababu alijua zile tabu zote alizokuwa anazipata zimemuishia, aliinua mikono juu akamshukuru Mungu kwanza kwa kuamini Tabu zimeisha, Pili kwa kumsaidia mkewe kujifungua salama.
Rahma baada ya kujifungua alimkalisha chini mmewe na kumuomba msamaha kwa yote aliyomfanyia, Ticha nae alikubali kumsamehe kwa sababu alijua wazi haikuwa akili yake.
"Nimekusamehe mke wangu japo ulinitesa sana, naamini haikuwa akili yako, Ila siitaji tuzae tena huyu anatosha, kwa mateso nliyoyapata sitaki tena.
" hee mme wangu tusizae tena ,, aliuliza rahma.
" Ndio.
" aka staki nataka tuzae wa pili.
" ili uje unitese tena sio! ,,
" sikutesi bhna mme wangu ile si ilikuwa ya kwanza tu?
Furaha iliyokuwa imepotea ndani ya miezi mitano hatimae ilirudi ndani ya nyumba, mwili wa Ticha ulishaanza kuporomoka lakini sasa taratibu ukaanza kujirudi, kutokana na kuanza kupata maanjumati mazuri kutoka kwa mke wake.
"Siamini kama mke wangu ameanza kunijali kama zamani, Nlisha hadi konda kwa kunyanyapaliwa ndani ya nyumba, sasa hivi nang'aa tu, nkirudi kazini napokelewa vizuri kama hivi, mambo ya msosi yako shwari, Toto linajua kuvaa vizuri ukimuona mwenyewe unanenepa si wake wengine mme unarudi nyumbani kakuvalia nguo chafu chafu ukimuona hata humtamani, ukiuliza eti za nyumbani, Kitandani shuguli ile ile imerudi kwa nini nsinenepe mie?, lakini wakati ule eeee! mara saa tisa usiku mtu una usingizi kibao mwanamke anataka dudu, mara lala nje mara pika, usikonde mchezo!.
Alijikuta akiongea maneno tofauti ticha, jioni moja baada ya kutoka kazini na kupokelewa vizuri na mkewe huku akiwa amebeba mtoto wake alie mpatia jina la Sudays.
Maisha ya vicheko, furaha , ,,,yaliendelea upande wa Ticha pamoja na mkewe, Huku upande wa Seid, Hamad pamoja na raya, wakikazana kuhakikisha wanatumia umoja wao kufaulu masomo yao yote, na kupata hundrend pasent %z za kila mtihani unaokuja mbele yao.
Baada ya kumaliza kufanya mitihani ya miezi sita wakiwa chuo, walipata rikizo nyingine ya wiki mbili.
Hamad aliwaita wote wawili kwa ajili ya maongezi mara tu walipofunga chuo, akawaomba wazitumie wiki mbili hizo kwenda kutalii katika mlima kilimanjaro, ambao kila siku wanausoma kwenye history bila kuuona hali ya kuwa uko Tanzania hii hii na uwezo upo.
"Nadhani hilo ni wazo zuri sana my friend ila umelifikiria hilo bila kufikiria hali yangu ya kipesa.
Aliongea Seid baada ya kusikia mawazo ya rafiki yake.
"Kuhusu pesa hilo ni juu yangu, nimefikiria hilo kwa sababu, haiwezekani kila siku tunasikia Kilimanjaro, Kilimanjaro kilimanjaro hali ya kuwa hatujawai fika na iko Tanzania hii hii na ni arusha tu hapo.
"Basi mimi niko tayari kwani hiyo itakuwa ni nafasi nzuri sana kufika hata bungeni si unajua kipindi cha bunge hiki?
"Heiwaaaaaaaaa!!!! ,,aliitikia kwa kukumbuka hamad ,, Yes! tunaenda Udm then Kilimanjaro.
"Ila mimi sijui kama ntakubaliwa nyumbani ,, Raya aliongea kwa upole.
"Nyumbani kwani uko na nani? ,,aliuliza Hamad.
"niko na Mama, tena wa kambo.
"Ina maana hauishi na mama yako mzazi!?
"Um kiukweli mamaangu alifariki mimi nkiwa na miaka kumi na tano.
"Oooooh Pole sana Raya mbona ulikuwa hujatueleza sasa na aliugua au?
" nshapoa, ni mambo ya kifamilia tu hayo so! siwez yaeleza kwa kila mtu.
Waliongea, wakakubaliana wote watatu kuwa wataenda, huku Raya akisema atafanya juu chini ili waende pamoja huko Kilimanjaro kwani nae anapatamani sana.
"Nimemmis sana mama, itabidi tuongozane pamoja Seid mpaka nyumbani kisha mi jioni ntarudi mjini ,, aliongea Hamad kumwambia Seid, walipomaliza kuzungumzia habari za kwenda kuuona mlima wa kilimanjaro na mingine ya kihistoria.
"Basi itabidi twende wote watatu kwa sababu hata raya anaitaji kwenda kumuona mama.
"Wao, ni vizuri mno tukienda wote, najua wakati wa kurudi tayari ntakuwa na kampani.
Raya alikuwa ana gari lake, ilibidi aliache pale pale paking, waliingia kwenye gari la hamad wote, wakaanza safari ya kwenda shamba alikokuwa akiishi Bi najma.
Walitumia muda wa Saa zima kufika huko, walimkuta bi najma akiwa amekaa chini ya mti wa mzaituni, walikumbatiana kwa furaha huku wakimsalimia, Bi najma aliwakaribisha kwenye mkeka aliokuwa amekalia, kisha akawaomba wamungoje kidogo anaenda kuchukua kisturi ndani.
"Raya huyu ndo mamaangu, kipenzi changu, Roho yangu, bila yeye nisingekuja duniani.
Seid aliongea kumwambia Raya, Raya nae aliitikia kwa furaha, huku akisema amefurahi kumuona.
Bi najma alitoka ndani akiwa na kisturi kwa furaha, aliwakaribisha kwa mara ya pili, walifungua maongezi yaliyokuwa yameambatana na kutambulishana hasa seid kumtambulisha Raya kwa mama yake.
"Nimefurahi sana kukufaham mamaangu, mkwe wangu, nimefurahii kiukweli, karibu sana nyumbani , aliongea bi najma akipiga piga mikono yake.
"Asante sana Mama, hata mimi nimefutahi sana kukufaham.
Kwa kuwa siku nyingi walikuwa hawajaonana, walijikuta wakiwa na mengi sana ya kuongea. Hamad alizidi kufurahisha maongezi kwa mafumbo na methali kutoka katika vitabu tofauti, pia hawakusahau kumweleza bi najma uamuzi wao wa kwenda kutembelea kilimanjaro, Bi najma alifuruhi na kuwapa baraka zote pindi watapoanza safari yao.
"Binti nyumbani hawajambo? ,, alimgeukia raya akamuuliza hali ya nyumbani.
"Hawajambo wote mama!. ,, raya alimjibu akiwa ameangalia chini.
" Unaitwa Raya Bint nani!?
" Raya bint Soudy!.
" jina zuri sana mwanangu na mama anaitwa nani? ,, alipoambiwa raya bint soudy alishtuka kidogo akajua ndo yule yule bint ambae mwanae aliwai kumwambia kuhusu yeye, ndipo akaamua kumuuliza swali la mtego la kuitaji jina la mama, kwani aliyakumbuka vizuri maneno ya mwanae alipomuambia, " nimeongea na msichana mmoja anaitwa Raya ila jina la baba yake limenishtua, anaitwa soudy, soudy na masoudy si ni sawa?
" Mama yangu anaitwa Yula'ina Bint Qasim ila alifariki kipindi mimi nna miaka kumi na tano, ,,,,,,,Raya alijibu na kumuacha bi najma katika wakati mgumu wa mshangao.
Tukutane Sehemu ya 18