TAFUTA HAPA

Hadithi:Penzi La Mpangaji Sehemu Ya #6

“Mi ndo kinywaji changu hicho”.Alijibu huku anatabasamu.
“Ha ha haaa, na mayai je?”.Swali lingine la kisomi.
“Siyo saana, ila napenda yakiwa yamekaangwa”.Alijibu Nesi.
“Kwa hiyo yakiwa yamechemshwa na yapo tayari kuliwa na wewe, unaweza kuyala?”.Nilizidi kutema mafumbo.
“Mh! Ya kuchemsha mi siyo mpenzi”.Akajibu huku akizidi kutabasamu.
“Kwa hiyo mayai yaliyochemka hata mawili humalizi?”.
“Mawili tu! Hayo fasta,tena naongezea na koka”.
“Aaaah”.Nilihamaki huku nikiwa na furaha baada ya jibu lile.
“Eeee”.Akajibu.
“Basi poa. Nikimaliza nadhani nitalala,au utakuja kupiga stori na mimi?”.
“Mh! Sijui aisee. Ila nitaangalia si wajua vitu vya watu hivi”.Alinijibu wakati huo mimi nilishaanza kutupia kile chakula kinywani mwangu.
“Ok! Poa. Ngoja mimi nile kwanza kwa maana ili tumbo nahisi linanyonga kwa sababu halina kitu”.Nilimjibu yule Nesi na kisha alinikabidhi chenji yangu na kutoka mle wodini.
Sikutaka kumuonesha muda uleule nia yangu, mpango mzima nikaupanga ufanyike saa nne au saa tano kama kutatokea kikwazo kwenye saa nne.
Baada ya kumaliza kula na kunywa, nililala kwa kujiegesha huku akili yangu ikiwa inategea saa nne ifike.
Nini kitaendelea?