TAFUTA HAPA

Hadithi:Penzi La Mpangaji Sehemu Ya #4

Niligundua kuwa yule jamaa alikuwa ni muuguzi wa zamu ambaye ana cheo kidogo,na katika hospitali ile,wanafunzi walikuwa wana sehemu zao maalum kwa ajili ya kulazwa na siku hiyo kulikuwa hakuna mwanfunzi aliyeletwa zaidi yangu.Niliingia viwanjani na kuanza kutafuta mwanamke wa kutuliza maumivu yangu huku nikiwa na hamasa kubwa ya ujana wangu ambao sikufahamu kuwa ni maji ya moto.
Kiukweli soko lilikuwa limedoda siku ile, hadi saa kumi na moja na nusu, nilikuwa sijapata goma la kunisuuza maumivu yangu, hivyo niliamua kurudi zangu hospitali na breki ya kwanza ilikuwa ni kuingia kwenye ile wodi na kubandika yale madiripu na kisha kuanza kupiga kelele kana kwamba nilikuwa nimetoka usingizini.Haikuchukua hata dakika, yule jamaa alikuja huku katabasamu na kuniuliza.
“Vipi dogo, umefanikiwa?”.
“Aaah, huko majanga tu! wamehadimika kama bia ya bingwa”.
“Kwa hiyo, vipi sasa?”.
“Leo usiku nitatoroka, nitajifanya napunga upepo halafu naondoka. Nitarudi baadaye”.
“Hapana dogo,hiyo ya usiku sikuruhusu. Ukipigwa je? We tulia, kesho tutapanga tena”.
“Poa kaka, ila naumia mwenzako”.
“Tulia dogo, vumilia hadi kesho. Sasa hivi naondoka, namuachia maagizo muuguzi mwingine. Toa hayo madiripu halafu jifanye umepata nafuu kidogo”.Jamaa aliongea hayo na kutoka nje ambapo aliniacha mimi nabandua yale maplasta na kisha kukaa kitako.
Baada ya dakika tano,yule jamaa muuguzi aliingia na muuguzi mwingine ambaye nilipomtazama moyo wangu ukawa kama umekufa ganzi. Nikashindwa kuyatoa macho yangu usoni pake na kunifanya nizidi kushikwa namshawasha mwingine wa hali ya juu.
“Habari yako mgonjwa”.Ilikuwa ni sauti tamu na nyororo ikipita masikioni mwangu na kusababisha akili na ubongo wangu kuhama kwa muda na kujenga fikra za kishetani katika mwili wangu.”Dogo unasalimiwa, mbona umekaza macho? Malaria ndiyo inazidisha kasi nini?”. Aliuliza yule jamaa muuguzi kitu ambacho kilinifanya nitoke katika yale mawazo yangu potofu.
“Hamna Dokta, sema akili yangu inawaza itakuwaje hadi kesho ikiwa hivi hivi. Poa dada, mambo vipi?”.Nilimjibu yule jamaa muuguzi na kumsalimia yule muuguzi aliyeingia naye.