TAFUTA HAPA

Hadithi:Penzi La Mpangaji Sehemu Ya #2

Sehemu ya 2
Nilijiregeza kiasi kwamba nilishindwa hata kutembea,hivyo nikaletewa kile kiti cha wagonjwa wasiyojiweza ili kinisaidie kuingia hospitali. Baada ya kuniingiza mle, yule mwalimu akabaki nje kwa ajili ya kusubiri majibu yatakayotoka kwa yule aliyenipokea.Ile kufunga ule mlango niliyoingilia, nilinyanyuka haraka na kuanza kuongea na yule muuguzi aliyenipokea huku nikimshawishi kwa uongo mwingi ili asinidunge sindano zao,hasa diripu.
“Kaka, unataka hela hutaki?”. Nilinyanyuka na kumtupia swali yule jamaa aliyekuwa anahangaika kunisukuma na kile kiti cha wagonjwa.Kitendo cha mimi kunyanyuka vile ghafla,kilimfanya kidogo ashtuke na kuhisi kuwa nimechanganyikiwa.”Wewe si unaumwa wewe? Au ndiyo Malaria inakupanda kichwani?.Aliuliza yule kaka.”Tulia kaka, skonga kuna ukame sana. Hapa bila kuzuga naumwa basi kule skonga ningebaka wenzangu. We sema, unataka hela au hutaki”.Nilijitetea kidogo na kurudi kwenye mada yangu.
“We unataka ufanye nini? We mwenyewe kwanza ni mwanafunzi,halafu unaniulizia mfanyakazi kama nataka hela. Inakuwaje hiyo?”.Jamaa alikuwa mbishi kuelewa,ila nikamsawazisha.
“Sikiliza Bro, mimi hapa siumwi. Cha msingi, wewe nibandike bandike hayo madiripu halafu muite huyo ticha aje kuniona. Usimruhusu aende kwa daktari,kwani ukifanya hivyo utakosa hela”.Nilimwambia hayo huku nikimwangalia usoni nikisubiri jibu lake.
“Ehee, nakusikiliza dogo. Au ndo umemaliza?”.Yule muuguzi akauliza tena.”Kwani Bro hujanielewa wapi? Mbona unakuwa na fuvu gumu?”.Nilimuuliza kwa jazba kidogo huku nasukuma kichwa chake kwa kidole cha shahada.”Dogo sikiliza, hapa tunasaidiana. Mimi nikikuwekea hayo madiripu,nitapataje hiyo hela?”. Jamaa aliniuliza swali hilo.
“Kumbe tatizo ni hilo. Akija we zuga kuwa unanihurumia sana,halafu mwambie bei ya haya madiripu pamoja na hela ya msosi wangu nitakao kula nikiwa hapa. Usimruhusu aende kwa daktari mkuu, maliza hapa hapa. Mwambie wewe utapeleka taarifa zote ofisini”.Nilimaliza na yule muuguzi kwa tabasamu,akachukua maplasta na kuanza kubandika ile mirija mikononi mwangu bila ya zile sindano, wakati huo ilikuwa ni mida ya saa saba mchana.