SEHEMU YA 3
Kutokana na mapenzi ya mama aliyonayo kwangu, alipanga zamu ya kulala kitandani kwa wiki moja moja.
ni maisha ambayo tulishayazoea, ilipokuwa ikifika zamu yangu mama analala chini,na ikifika zamu ya mama kama hapo, mimi nalala chini.
Namshukuru Mungu amenijalia usingizi wa haraka, huwa nkiweka ubavu sigeuki mara mbili tayari nakuwa nimesinzia, nlipoingia kwenye neti hazikupita dk tano tayari nkawa mbali sana kindoto, sikuweza kushtuka wala kuelewa chochote kilichoendelea kwa upande wa mama mpaka asubuhi ya saa moja nliposhtuka.
sikushtuka kwa uwezo wangu bali ni kwa sababu ya mlango wa kutokea nje baada ya kusikia mama anauburuta kuufungua, nliamka na kukaa kwenye neti nkipikicha pikicha macho ambayo bado yalikuwa na usingizi.
"Shkamoo mama ,,nlimsalimia huku nkiwa naona kama malue lue mbele yangu kwa sababu ya matongo tongo ya kuamka nliyokuwa nayo pembezoni mwa ncha za macho yangu.
Mama aligeuka akaniitikia shkamoo yangu.
"umeamka baba? ,, aliniuliza.
"ndio mama nimeamka.
"vizuri mwanangu, basi toa neti uingize uvunguni kama kawaida, ukimaliza upige mswaki, kuna kiazi hapa kilibakia jana unaweza kukimalizia ili utafune chochote kisha utanifata shambani sawa!?.
"Sawa mama.
nlimuitika nkiwa natoka kwenye neti, alimalizia kufungua mlango akatoka nje kwa ajili ya kwenda shambani.
Nliamka na kuchukua kisturi kilichoko pembeni ya mlango nkanyagie ili kupatia juu ilipo neti, nlipanda nkaitoa kisha nkaikunja na kuiingiza uvunguni mwa kitanda. Nlichukua mswaki wa mti ambao nautumia kila siku na maji kidogo yaliyokuwa kwenye ndoo kwa ajili ya kunawa usoni..
Nadhani watoto wengi wamepitia katika hali hii hapa nliyokuwa nayo mimi, miongoni mwa vitu nlivyokuwa sivipendi ni kuoga, kwa nnavyokumbuka mpaka siku hiyo nlikuwa na zaid ya mwezi mzima sijui maji yanawekwaje mwilini, ilifikia kipindi nkawa nagombana na mama yangu kwa sababu ya kuoga.
nlimaliza kupiga mswaki nkaingia ndani, nkafunua kwenye sufuria na kukuta viazi viwili, nlivitoa vyote nkala kwa sababu nlikuwa tayari nna njaa, nlimfata mama shambani kumsaidia kulima na kupariria baadhi ya sehemu ambazo zilipandwa viazi vitamu, mpaka ilipofika saa nne na robo tulitoka nshambani kama kawaida yetu yeye akiwa amebeba viazi mimi kuni za kupikia ambazo huwa nazitafuta humo humo shambani kwa kuangaika baadhi ya sehemu zenye miti miti.
ni kama nlivyokuwa nimezoea na kufanya siku zote, nkitua kuni nachukua vidumu naenda bombani nkirud nasoma mpaka chakula kinapoiva. na siku hiyo nlifanya hivyo hivyo kwa kuwa nlishazoea bila kukumbushwa nafanya.
Ilipofika saa saba, mama alipanda kitandani ili apumzike japo nusu saa kabla ya kurudi tena shambani, nlimfata kitandani alipokuwa amelala na kukaa pembeni yake huku nkimuita.
"Naomba niende kumsalimia bibi kisha jioni narudi. Nlisema.
"Mwanangu unataka kukimbia kazi? ,,mama aliniuliza kiunyonge akionekana kulemewa na usingizi.
"Hapana mama, nna wiki mbili sasa hivi sijamwona bibi, naenda kumsalimia tu nakurudi mamaangu, kesho ni jumaa pili ntakuwepo nyumbani na ntafanya kazi.
"Sawa mwanangu baiskel yako si ni nzima?
"ndio mama.
"sawa msalimie sana
"Ok mama asante kwa kuniruhusu.
hakujibu, aligeuza ubavu wake akageukia sehemu ya pili akitafuta usingizi.
nlitoka nkafungua mlango na kuurudishia, nkaingia kwenye chumba kilichokuwa na baiskel, nlitoka nayo nje nkapanda na kuanzisha safari ya kwenda kwa bibi moyoni nkiwa na nia ya kwenda kumbana ili anambie ukweli wowote kuhusu baba au mwanaume aliempa mama mimba mpaka nkazaliwa mimi.
Kutokana na nlivyokuwa napenda kuendesha baiskel, sikumaliza dk 28 tayari nlikuwa kwenye nyumba ya makuti ambayo alikuwa akiishi bibi peke yake maeneo ya matemwe zanzibar.
nliegesha baiskel huku nkimuita, nlimuita zaid ya mara nne bila kuitika, nkaingia ndani bila kufanikiwa kumuona, nlijua maeneo yake yote anayokuwa akipenda kuwepo kama si ndani.
Nlingiza baiskel yangu ndani na kwenda nyuma ya nyumba kulikokuwa na mti mkubwa wa mnazi, nkajua lazima atakuwa huko na kama si huko basi ni kwenye shamba la karafuu.
Nlifanikiwa kumkuta chini ya mnazi nyuma ya nyumba akiwa anasokota mkeka, pembeni yake akiwa na jagi la maji pamoja na kikombe kikubwa, miguu yake alikuwa ameinyoosha akikazana kusokota mkeka.
nlimnyatia kwa nyuma ili nimzibe macho kama kumsaprize.
"Nishakuona mjukuu wangu huna haja ya kunyata tena. Alisema bibi.
nlijikuta nasema "Duh" bibi mwanga huyu" kimoyo moyo kisha nkamuuliza" umenionaje bibi wakati sijakuona kugeuza macho kama si uchawi?
"harufu yako naijua mjukuu wangu,.
"um harufu yangu?
"ndio.
"Ah hakuna lolote ndo maana mabibi mnaambiwaga wachawi hivi hivi, sijaona ukigeuza uso, niko nyuma yako hata kama ni harufu duh, Shkamoo bibi.
"Maraaba maraaaba baba ujambo!
"sijambo bibi.
"mama yuko wapi!
"yuko nyumbani amelala kasema nimsalimie sana.
"ok sawa, niko nasuka mkeka wa harusi hapa au hutaki kunioa unaniongopea.
nliishia kucheka bila kujibu chochote, nlimuangalia bibi anavyosuka mkeka, dk kadhaa zilipita tukiongea vitu flan vya kawaida kama bibi na mjukuu wake huku tukifurahi na kucheka sana.
Nlikatisha maongezi baada ya kuona tunachokiongea kinazidi kunoga wakati point ya msingi iliyonipeleka sijaiongea, nlimuita na yeye akaniitikia kwa haraka huku akiwa analamba kidole chake kipate mate flan ya kushikiza vizuri ukilii za kusukia mkeka.
"bibi naomba nikuulize swali nisameee lakini kabla ya kukuuliza.
alinyanyua jicho lake na kunitazama akanambia Uliza kisha akaendelea kusuka mkeka.
"Bibi tokea nizaliwe sijawahi muona baba, na sijawai kuambiwa kama amefariki au laa naomba unambie bibi kama unajua chochote.
Baada ya kumuuliza nlikaa kimya nkashikilia tama nkiwa nimekunja miguu huku nkimuangalia bibi anavyokazana na mkeka. Hakujibu swali langu, alikaa kimya ndani ya dk moja, aliachia pumzi kisha akauweka pembeni mkeka.
"Kweli mjukuu wangu umekuwa mpaka unauliza kuhusu baba!, aya nambie unataka ukweli gani!?
"wowote bibi ikiwezekana unambie tu aliko baba.
"usijli mjukuu wangu, ukweli utaujua tu kwa kuwa umeuitaji, Ni Stori ndefu na inataji moyo kuisimlia, hasa mama yako ngumu sana kukwambia, anajisikia uchungu sana pale alipo ila anavumilia ili kuhakikisha anakulea vizuri na kukupatia Elim, na kwa kuwa umeuitaji ukweli mimi ntakusimlia yale nnayoyajua ujue kila kitu kwa sababu mama yako ukimuuliza chochote kuhusu baba yako anaweza kufa kutokana na yaliyomkuta. Ila Njoo kesho asubuhi ndo ntakuambia leo sikuambii!
"aaaaagh bibi kwa nini usinambie sasa hivi?, hujui kiasi gani nateseka bibi, nkishaujua ukweli hata nkiteseka poa tu, naumia kwa kuwa naona yanayonikuta kisha sijui chochote naomba unambie sasa hivi tu. Nlisema. Alinipiga jicho la sekunde kadhaa kisha kuniuliza.
"Babaako unamjua anaitwa nani?
Kiukweli Lilikuwa ni swali gumu sana kwangu kwa sababu sijawai kuambiwa baba yangu anaitwa nani, kumbu kumbu ambazo nlikuwa nazo ni kumbu kumbu za jina la Sharif ambalo nliambiwa ni la babu yangu na ndo jina nnalotumia shule.
"Bibi!, mama hajawai kunambia jina la baba yangu, tokea nlipoanza shule nliandikishwa kwa jina la Said sharif, nlipokuja kumuuliza sharif ndo jina la baba alisema la Babu.
"ni kweli mjukuu wangu, Sharif ni babu yako, Mwanangu najma hakuitaji utumie jina la baba yako kwa sababu anamchukia sana kwa vitendo alivyo mfanyia.
Bibi alitoa kikombe kilichokuwa juu ya jagi nkamsaidia kumimina maji ya kunywa. Alikunywa taratibu alipomaliza alirudishia kikombe, akasogea nyuma kidogo kwa ajili ya kuegamia kwenye mti, alitoa sauti ya "E, E, E, e akiashiria uchovu wa mgongo baada ya kuukalisha bila kuuegemesha sehemu muda mrefu, aliachia pumzi kisha akaanza kunipa ukweli kuhusu baba, huku na mimi nkikaa makini kumsikiliza.
"Mjukuu wangu, waswahili wanasema Usichokijua ni sawa na usiku wa kiza.
"Pia kilichoko nyuma ya pazia huwezi kukijua mpaka liondoshwe au uambiwe.
nlijikuta nadakia maneno yake, na kumbakiza akicheka.
"kweli umekuwa inabidi unioe tu sasa hivi, alisema kiutani akaendelea kunipa story... nakumbuka ilikuwaaaaaa! Tarehe 05/02/1990 Wazee wa baba yako ambao ni babu zako, walipiga hodi kwenye nyumba yangu hii na kuleta barua ya kumuoa mama yako, kutokana na mila za hapa kijijini kwetu nliipokea vizuri na mimi hapo nguvu bado zilikuwemo hata macho yangu yalikuwa mazima, nliisoma, nlipomaliza nkawauliza.
"Ni nani mmekuja kumtolea hii posa?
walijibu kwa kusema "mtoto wetu Suudy japo bado anasoma lakini anaitaji kuoa, na tumeona tuoe katika ukoo wako mama kwa sababu ukoo wako una heshima zote.
Mjukuu wangu mama yako ndo alikuwa amemaliza darasa la tisa, sikuweza kukataa, nliongea nao muda mrefu tukapanga mambo ya mahari, Najma mama yako nlimueleza akakubali na baada ya wiki mbili ndoa ikapita.
masoudy ambae ndo baba yako mzazi. wakati huo alikuwa amemaliza form six anasubiri majibu yake.
Waliuanza ukurasa wa ndoa baada ya ndoa kupita na walikuwa wanapendana sana sana zaidi ya sanna. kila mmoja aliiangalia ndoa yao kwa jicho la tatu kutokana na mapenzi mazito waliyokuwa wakioneshana.
wakienda shamba wanaenda wote, kisiman kuchota maji wotee, sokoni wotee, kiufupi kila sehemu.
Baba yako wapo waliomuita mume bwege kwa alivyokuwa akishugulika kumsaidia mama yako, mara anafua nguo na watu wanamuona, mi mwenyewe nliwai kumkuta anaosha vyombo nlipomuuliza akasema namsaidia mke wangu kachoka leo, siku nyingine anapika, na kufanya vingine vingi kama kumsaidia mkewe.
katika shamba lao walipanda mpunga mwingi pamoja na mahindi, wakiamini vitawasaidia sana mbele kiuchumi au hata kipesa.
Walifanya mengi ndani ya miezi michache ya ndoa yao, na kupata mafanikio mengi ambayo kila mtu wa hapa kijijini aliyatamani.
Baada ya miezi sita kupita. masody alipata furaha mpya katika maisha yake alipopata matokeo ya masomo na kukuta maks zake ni za kwendelea, wiki kadhaa zilipopita akajiunga na chuo cha Suza (univarsty of Zanzibar).
Najma alimjali kwa kila kitu mmewe,
masoudy unene ulianza kuuandama mwili wake kutokana na maanjumati aliyokuwa akiyapata kwa mkewe na kumfanya arizike. Ila Alama ya kuuliza ilianza kupita pande zote mbili yani kwangu na familia ya masoudy baada ya kuona mwaka umeisha wakiwa katika ndoa hata dalili ya najma kubeba mimba haipo, ndipo kikao cha familia zote kilifanyika ikabidi tulazimike kuwaweka chini kuwauliza, walichotujibu ilitulazimu tuwe wapole na kurizika kwa majibu yao.
"waliwajibu nini?
nliingilia tena maongezi ya bibi baada ya kuona sijaelewa vizuri.
"Swali zuri, walituambia wamepanga wasizae mpaka masody amalize chuo.
Maisha yalisonga mbele, siku na miezi ikakatika, mapenzi yao yakionekana kuwa marudufu kila siku.
Mjukuu wangu!, mwaka 1992 wakiwa tayari wana miaka miwili ndani ya ndoa yao, lilitokea Tukio ambalo sitolisahau katika maisha yangu yote ya duniani, na hicho ndo kitu ambacho nahisi najma ataendelea kulaani juu ya babaako japo yapo mengi mabaya aliyomfanyia na najma kuyavumilia, ila kwa hilo tukio!, Kama baba yako atakaa siku moja chini na kulifikiria, basi naamini siku moja atarudi kwa mama yako akiwa amepiga magoti chini akiitaji msamaha, kwani ni wanawake wachache sana wanaweza kujitolea kwa jinsi alivyojitolea mwanangu najma ili kuokoa maisha ya mmewe.