TAFUTA HAPA

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 2)

Sehemu 2

Machozi yalishaanza kunitoka, mama nae tayari alikuwa anabubujikwa na machozi kwa nilichomuambia.

" mamaangu mimi nateseka sana mwanao, naomba unambie kuhusu baba niteseke kwa kuchekwa kuishi na mama yangu lakini nkiwa tayari nimeujua ukweli wote, nkienda shule mimi natukanwa mama, mara naambiwa hivi mara vile unasikia raha gani hasa mwanao nnavyofanyiwa vitendo kama hivyo? najisikia vibaya mamaagu nambie ukweli niujue, kikubwa kipi hasa unanificha?

nliongea nkiwa nabubujikwa machozi. Sikuamini juu ya sauti ya huruma nliyoitumia kuongea. kama mama bado angeshindwa kunambia ukweli hatimae kutoka alikokuwa amesimama na kuingia ndani..

kiukweli nliumia sana kwa kitendo cha mama, nlimgeukia akiwa tayari amenipa mgongo nkajaribu kumuita bila kuitika, alipoingia ndani maneno ya hasira nlijikuta yakinitoka bila kujali kama ananisikia au laa.

"Najua unafurahi sana nnavyoteseka, hunipendi mama Hunipendi, unanifanya niishi kama mnyama wakati ni binadam kama wengine kwa nini lakini? au na wewe sio mama yangu uliniokota?

Nlikunja miguu yangu na kuiweka mikono juu nkainamisha uso na kuendelea kulia.

Mama baada ya kuingia ndani alipanda moja kwa moja hadi kitandani, aliendelea kulia kwa uchungu kutokana na kitu nnachomuuliza kila siku kumuuma, sikufahamu kwa nini haitaji kunambia ukweli, nlikuwa mtu wa kulalamika kila leo ili aniambie, nlijaribu kumkomfyuzi kwa kutumia akili zangu za utoto japo anambie tu baba yangu yuko wapi lakini bado sikufanikiwa.
alikuwa mtu mwenye huruma sana, Kwa nlivyomzoea sikuitaji kuamini kama ni roho ya mama yangu huyu huyu anaekubali mwanae nilie kila siku kisa baba, alinijengea mazingira ya kuamini uenda kuna siri nzito sana anaificha nsiifahamu, ila nlijipa moyo wa kuamini ipo siku ntaujua ukweli hata kama ntachelewa, na kilichokuwa kinanipa imani ni methali tunazosoma kila siku shule, huku Nkiapa kwa mungu kama nkiujua ukweli na ukawa uko tofauti ntatokea kumchukia sana mama yangu japo namuona kila siku kuangaika peke yake juu yangu.

Baada ya kulia kwa muda mrefu nliingia ndani nkamkuta mama yupo kitandani akiwa bado ana uwekundu wa macho, nlijua moja kwa moja amelia sana ilibidi nimsogelee na kumuomba anisamehe, nlimpenda sana lakini ni hasira tu ambazo zilikuwa zikinipelekea nimuulize kuhusu baba kila leo japo nlikuwa najua kabisa nkimuambia suala hilo anachukia hata kama alikuwa anacheka.

"Nisamehe sana mama ni hasira tu ambazo huwa zinaniingia mpaka kukuuliza jambo hilo ambalo najua linakukera kila leo. Nlisema kwa upole.
alinishika kichwani huku machozi yakimtoka upya.

"Nimekusamehe mwanangu.

tabasam la machozi liliingia usoni mwangu, nlimuangalia mama nkamshika machoni kumfuta machozi yaliyokuwa yanamtoka. Aliniangalia kwa huzuni machozi yakiwa bado yanamlenga, nlipogonganisha macho yangu na yake nkajua kuna kitu atakuwa ananisikitikia na kunionea huruma sana.

"ngoja niende jikoni nikuandalie chakula si unaona usiku huu unaingia? ,, aliongea akiwa anainuka kitandani mama.
"ndio mama.
"sawa, basi mi naingia jikoni chukua vitabu usome usome hapa, giza likiingia utawasha kibatali nkimaliza kupika ule ulale kesho uwahi shule sawa baba!.
"kesho jumaa mosi.
"Eh nlisahau kabisaaa! kumbe kesho uko nyumbani.
"ndio
"bado si mbaya, mtoto kulala mapema ni wajibu wake, nkimaliza kupika utakula ulale kesho tuamkie shambani sawa baba.
"Sawa mama.

Aliinuka na kusogea sehemu vilipokuwa vyombo, alichukua sufuria mbili, kiberiti pamoja na mfuniko kuelekea nje kulikokuwa na jiko.
Kipindi anataka kutoka nlimuita.
"Mama naomba unirushia huo mkoba wangu wa shule.
aliangalia sehemu ulipo mkoba, akanirushia na kwenda nje kwa ajili ya kupika.
*********

Mama huyu aliejulikana kwa jina la Bi najma baada ya kuingia jikoni na kuanza kupika, Dimbwi zito la mawazo lilimshika ghafla kipindi amekaa pembeni ya mafiga, alishika tama na kujiuliza vitu ambavyo majibu yake yalikuwa ni magumu sana kwa wakati ule lakini pia ni mepesi kwake kuyajibu, Kijana Seid aliendelea kujisomea ndani akisubiri chakula kiive, japo alikuwa mdogo lakini aliamini Elim ndo msingi wa maisha na ndo kitu pekee cha kumuondoa kwenye umasikini walionao yeye na mama yake Najma.

"Sijui mwanangu anafikiria nini mpaka kuniuliza kuhusu baba yake kila siku, laiti kama angekuwa anajua yaliyonikuta na uchungu nnaousikia, asingeniuliza kuhusu huyu mwanaume,
Uhmm ila ipo siku ntamwambia ukweli kwa sababu ni haki yake, Eh mungu nisaidie, sina nia ya kumficha mwanangu namuonea huruma tu mtoto mdogo anataka kujua mambo makubwa na mazito. Alisema peke yake maneno ya kiutu uzima najma.
aliendelea kuwa na mawazo mpaka chakula kilipoiva, alikitoa jikoni akazima jiko na kuingia ndani akiwa na sufuria mikononi.
**********

Nligeuka nkaangalia mlangoni baada ya kusikia mlango ukifunguliwa.

"bado unasoma mwanangu?, aliniuliza akiwa anaweka sufuria chini.

"ndio mama, ushamaliza?. Nlimjibu na kumtupia swali.
"bado kula tu hapa, nakuwekea chakula kwenye sahani kipoe mi naenda kuoga, endelea kusoma nkirudi kitakuwa kishapoa ule utandike ulale sawa!?
"Sawa nimekuelewa.

” au unataka nikutandikie?,, aliniuliza swali lililonifanya nitabasam.
“ hapana mama ntatandika tu mwenyewe. Lakini mama maji hamna unaenda kuoga nini?
nlimuuliza nlipokumbuka vidumu nimeviacha bombani.
"Itabidi nioge haya haya ya kunywa ntafanyaje sasa, wee si umeacha vidumu bombani?

Nlikaa kimya sikuwa na la kuongezea, alimimina maji yaliyokuwa kwenye ndoo ya maji ya kunywa na kwenda kwenye bafu lililopo hatua 20 mpaka 30 kutoka kwenye nyumba yetu kwa ajili ya kuoga.
Giza tayari lilishaingia, nlishusha kanga iliyokuwa kwenye dirisha kama pazia ambayo ipo mpaka leo kuzuia mbuu wasiingie ndani, nlichukua kibatali nkawasha, nlikisogeza karibu na daftari langu nlilokuwa nasoma, nkaendelea kupitia baadhi ya maswali na majibu kujijenga vizuri kiakili.

Somo nlilokuwa nkipenda tokea niko darasa la kwanza ni Hisabati, nlikuwa tayari kufeli masomo mengine lakini si somo hili, nlihakikisha napata mia chini ya mia kila mtihani unaokuja mbele yangu wa hesabu, hata walimu waliokuwa wakinifundisha hesabu walifahamu wazi kuwa nalipenda na kufanya juu chini wakinikazania kuhakikisha sifeli. maks zangu kubwa zilikuwa ni tisini mpaka mia. Walimu wote shuleni walinipenda kutokana na adabu, heshima na mwenendo mzuri wa masomo yangu darasani.

Namshukuru sana Mungu wangu na mama yangu pia aliekuwa kipau mbele kuhakikisha nakuwa vizuri masomoni, alikuwa yuko tayari kufanya lolote kuhakikisha pesa yoyote iliyotakiwa shuleni inapatikana, akili nlizokuwa nazionesha pamoja na jitihada aliamini ntafika ngazi za juu katika masomo.

nlikuwa darasa la tatu tu lakini walimu wote walinipenda kuanzia usafi na kwa mengine mengi nliyokuwa nayo ambayo mwalimu kama mwalimu anapenda kuona kwa mwanafunzi.

Mama alitoka bafuni na kunikuta nkiwa bado najisomea, alisogea pembeni yangu akanangalia nami nliinua uso wangu nkaachia tabasam baada ya kumkuta mama amenitazama.

"Mbona unaniangalia mama?, nlimuuliza
"Hapana mwanangu, nioneshe mlipo soma leo.

nlifunua madaftari tuliosoma siku hiyo nkamuomesha, alifurahi sana alipokuta good good masomo yote matatu, alipomaliza kukagua alianza kunifundisha hesabu za mbele kama ilivyokuwa kawaida yake,,
Pesa za kunipeleka tution hakuwa nazo, hivyo yeye aliamua kuwa mwalimu wangu wa nyumbani hasa katika masomo mawili hesabu na kiswahili, kupitia yeye nlipata mwangaza mkubwa sana darasan na kuonekana bora kila mara kutokana na kukifanyia mazoezi kitu cha mbele kupitia mama.

Ilipofika saa mbili kamili, mama aliniomba nifunike madaftari nkale kisha nlale, nlifanya hivyo madaftari yangu yote nkayaweka kwenye mkoba, nliinuka na kwenda kutundika mkoba wangu kwenye kimsumari kilichokuwa mlangoni, nkachukua chakula kilichokuwa juu ya ndoo na kuanza kula.

"Mama wewe huli? nlimuuliza baada ya kumuangalia na kumuona hana mpango wa kula.
"Nakula mwanangu, we kula ulale sawa baba.

Sikuongea tena kwa sababu kiazi kilikuwa mdomoni, sekunde kadhaa zilipita nkamuangalia tena, nlivyomuona ni kama mtu ambae alikuwa yuko mbali sana kimawazo.

"mbona unaonekana una mawazo? Ilinibidi nimuulize swali hilo, aliniangalia na kunambia sina mawazo ya aina yoyote mwanangu maliza kula ulale....
******

Najma aliendelea kumuangalia mwanae Seid, alitingisha kichwa akimsikitikia baada ya kukumbuka mengi mazito kwenye kichwa chake kuhusu mwanae.

"Masikini mwanangu anaonekana ana akili sana, Nakuomba mungu umuongoze apate kile kilichomo akilini mwake na cha ziada, nami naomba unisaidie nipate riziki zangu kwa njia nzuri nimsomeshe mwanangu uenda ndo msaada wangu mkubwa. Uhm maisha haya!!!, baba mtu yuko mjini huko anakula vyakula vizuri, analalia kitanda kizuri, mwanae analalia vyakula vigumu kama hivi kwa nini wanaume wako hivi lakini, japo angekuja basi kumchukua mwanae akaishi nae huko kwa sababu ana maisha mazuri, mimi aniache na shida zangu nlizonazo. Aliwaza kichwani mwake jicho likigonga usoni mwa seid wakati yuko bize na kula...
*****