TAFUTA HAPA

MPE RAHA MPENZI WAKO KWA MESEJI HIZI

 



Moyo wangu umekupenda wewe peke yako, kamwe sifikirii kwenda kwa mwingine. I luv you honey...


Hata kama nitajidanganya kwamba sikupendi, moyo wangu umeganda kwako na hakuna dalili za kukuacha, wewe ni wangu peke yako dear...


Hata kama watasema mengi kiasi gani, kwako wewe nitaendelea kuwa mpole, maana nakupenda sana...


Siyo rahisi kuishi bila wewe, maana wewe maishani mwangu ni sawa na maji katika maisha ya binadamu. Mwaaaaa


Ni kweli nakiri ndani ya nafsi yangu kwamba nilikukosea mpenzi wangu, naomba unisamehe na unipe nafasi nyingine katika moyo wako mpenzi wangu. Nakupenda sana, pokea busu mwanana....mwaaaaaaaa...