Mapenzi yana kanuni zake,  kanuni ambazo usipozifuata huwezi kupata furaha uliyotarajia. Unapotokea  kumpenda mtu, hiyo ni hatua ya kwanza lakini omba sana upate ile bahati  ya kumpenda mtu ambaye naye anakupenda kwa dhati.
Kwa bahati mbaya ukitokea  kumzimikia mtu ambaye wala hana hata chembe za penzi kwako, utaumia sana  na kama utalazimisha kuwa naye, utakuwa unajitafutia vidonda vya tumbo.
Hata hivyo, wapo waliobahatika  kuwapata wapenzi wa ukweli lakini kwa kushindwa kwao kujua yapi ya  kufanya ili kudumisha penzi, leo hii wameachika na bado wanaranda  mtaani.
Kwa kifupi ni kwamba, unapoingia  kwenye uhusiano na mtu na ukabaini naye anakupenda, hutakiwi kubweteka  bali unatakiwa kutumia utundu na ubunifu wako katika yale ambayo  yatamfanya huyo mtu wako ahisi wewe ni wa pekee kwake.
Ninapozungumzia hayo, namaanisha  ubunifu kwenye mambo mengi ambayo hakika nikianza kuyaelezea hapa,  nafasi inaweza isitoshe ila kwa leo nigusie utundu katika uwanja wetu  ulee wa kujidai.
Faragha ni eneo muhimu sana ambalo linaweza kubomoa au kuimarisha ndoa. Ninapozungumzia hilo, ni kwa wote yaani mke na mume.
Mwanaume anatakiwa kumridhisha  mkewe kwa kiwango kinachostahili. Kusiwepo mazingira ya kupeana mambo  kiduchu kwani ikiwa hivyo lazima mke atakosa furaha iliyokamilika.
Ila sasa leo nataka niwazungumzie  kwa kirefu wanawake. Kuna wanawake ambao wamebahatika kupata wanaume  wanaowapenda sana na kuwapatia kila wanachohitaji.
Hawa wanatakiwa kujiona ni wenye  bahati kubwa kwani kwa hali ilivyo sasa, wanawake wengi wanatafuta  wanaume wa kuwaoa hawawapati.
Kinachonishangaza ni kwamba, kuna  baadhi ya wanawake ambao wako ndani ya ndoa lakini wamejisahau kwamba  wana jukumu la kuwapa waume zao furaha ambazo hawawezi kuzipata  kwingine.
Ukijaribu kuchunguza utabaini  wanawake wengi walio ndani ya ndoa siku hizi wanasalitiwa sana. Hii ni  kwa sababu wamekuwa waongeaji sana lakini wanapokuwa faragha unaweza  ukadhani siyo wao. Hawajui kitu, wamekaa kama magogo tu halafu eti  wanadhani hawatasalitiwa na ndoa zao zitadumu, zitadumu kwa misingi ipi?
Mwanamke akae akijua kwamba,  mumewe ni kama mtoto ambaye anatakiwa kubembelezwa huku akipewa vitu  vitamu ili kumpumbaza asishawishike kutoka nje. Ukiwa kwenye ndoa kisha  ukachukulia kila kitu poa tu eti kwa kuwa tayari ulishapendwa ipo siku  utajikuta ni mke wa pambo la nyumba tu.
Mtaani kuna utitiri wa nyumba  ndogo, wanaume walioanzisha makoloni hayo nje ya ndoa zao walikosa wake  sahihi ambao wanaweza kuwashikilia waume zao.
Matokeo yake sasa nyumba ndogo  hizo ndizo zinazooonekana kuwashika waume za watu siku hizi na  wanafanikiwa kwa kuwa ni watundu na wabunifu.
Sasa kwa nini wewe mwanamke uliye  ndani ya ndoa usifanye kama yale wanayofanya nyumba ndogo? Kuna dada  mmoja nilizungumza naye hivi karibuni akaniambia eti amenuniana na  mumewe huu ni mwezi wa pili baada ya mwanaume wake huyo kutaka afanyiwe  mambo ambayo yeye aliona kinyaa kuyafanya.
Kabla ya kumjibu kwanza niliguna,  sababu ya kuguna ni kwamba niliyagundua hayo mambo ambayo aliona kinyaa  kumfanyia mumewe. Niseme tu kwamba, mapenzi wakati mwingine ni uchafu,  wanaojua mapenzi wanajua kwa nini nasema hivyo.
Nilichomjibu mwanamke huyo ni  kwamba, kama mwanaume huyo anampenda amfanyie kila atakacho isipokuwa  kukubali kufanya mapenzi kinyume na maumbile na nikamwambia kuwa,  mapenzi ni uchafu hivyo hayo ambayo anaona kinyaa kumfanyia mumewe ndiyo  ambayo wengine wamekuwa wakiyafanya na wamefanikiwa kuzishika ndoa zao.
Naomba niseme tu kwamba, huenda  unajiamini kuwa ni mzuri na umbo la kuvutia kiasi kwamba, ni rahisi  kupata mwanaume wa kuoa lakini tambua bado utakuwa na kazi kwenye  kuidumisha ndoa na kuhakikisha hukaribishi mazingira ya mumeo kutafuta  nyumba ndogo.
Hakikisha unaonesha uanamke wako  ili hata kama huyo mumeo atatoka nje, iwe ni kwa tamaa zake tu lakini  mambo ya msingi uwe unampatilizia.