TAFUTA HAPA

JAMANI MIE UKAHABA SASA BASI" PART 5

INAENDELEA HAPA:
Baada ya kuvutana sana kati ya Mwalimu mkuu na Mr. Brown ofisini ikabidi mwalimu mkuu akubali kuwa mpole na kurudisha pesa japo sio zote ilibidi mwalimu mkuu atoe nusu ya pesa zilizolipwa, Mr. Brown alilipa ada Shilingi laki moja na nusu ikabidi mwalimu mkuu atoe nusu ya pesa hizi Shilingi elfu sabini na tano na kumpa Mr. Brown. Mr. Brown akapokea zile pesa Shilingi elfu Sabini na tano akamchukua binti yake JENIFER wakaondoka na kuelekea nyumbani kipindi wapo njiani wanaelekea nyumbani, Mr. Brown alikua na hasira sana akamwambia binti yake JENIFER "We mtoto leo tukifika tu nyumbani chukua nguo zako na uondoke nyumbani kwangu sitaki kukuona, mshenzi wewe!". Walipofika nyumbani tu Mr. Brown akaanza kumuhadithia mke wake Mrs. Brown yaliyotokea shuleni kuhusu binti yao JENIFER na akamwambia Mrs. Brown kuwa hataki hata kumuona aondoke nyumbani kwake lakini kwa maamuzi haya ya Mr. Brown mke wake Mrs. Brown hakuafikiana nayo akamwambia mume wake
"SASA MUME WANGU UNAMFUKUZA MTOTO AENDE WAPI WAKATI HAPA NDIO KWAO, UNADHANI ATAENDA WAPI? KAMA MAJI YAMEISHAMWAGIKA MAKOSA NDIO KISHAFANYA HAKUNA JINSI NI KUMSAMEHE NA TUKAE TUSHAURIANE TUJUE TUNAFANYAJE MUME WANGU PUNGUZA HASIRA". Mr. Brown akamjibu "HAIWEZEKANI MIMI SITAKI HATA KUMUONA HUMU NDANI AONDOKE SITAKI KUMUONA". Mrs. Brown nae akamjibu "KAMA UNATAKA HUYU BINTI AONDOKE HUMU NDANI BASI JUA NITAONDOKA NAE SIWEZI KUKUBALI BINTI YANGU AONDOKE AKAPATE SHIDA WAKATI KWAO ANAPO, UKIMFUKUZA JUA NAMIMI NAONDOKA HUMU NDANI" Baada ya Mrs. Brown kumuambia Mume wake Mr. Brown maneno hayo ghafla Mr. Brown alisema kwa sauti kali ya juu "SAWA MKITAKA MUONDOKE WOTE, SIWEZI KUFUGA UPUMBAVU KAMA UNAONA NAMUONEA MTOTO WAKO MFUATE MUONDOKE WOTE PUMBAVU!". Mrs Brown akamjibu "EH E! TAFADHALI BABA WEE, USINITUKANE NGOJA TUKUPISHE UBAKIE NA NYUMBA YAKO SIO UNIFOKEE. MPUMBAVU MWENYEWE!. Ghafla Mr. Brown alikurupuka na kumvamia mke wake Mrs. Brown na kuanza kumpiga makofi huku akimwambia
"YANI WEWE UNADIRIKI KUNIAMBIA MIMI MPUMBAVU, WAKATI JENIFER KAFANYA MAKOSA DHAHIRI. HIVI MIMI NINAVYOHANGAIKA KUTAFUTA PESA ZA KUMSOMESHA HALAFU ANALETA UPUMBAVU UNAFURAHIA ETI EEH!"