TAFUTA HAPA

JAMANI MIE UKAHABA SASA BASI" PART 4

INAENDELEA HAPA:Mwalimu KABAVAKO aliwachapa kila mmoja fimbo nne nne, kisha akawarudisha ofisini kwa mwalimu mkuu walipofika ofisini kwa mwalimu mkuu, mwalimu mkuu aliwaambia inabidi awape adhabu ya kukaa nyumbani mpaka uongozi wa shule utakapo kaa kikao na kuwafikiria na kujadili kosa lao ndio wafanye maamuzi ya kuwasamehe au kutowasamehe. Mr. Brown baba yake na JENIFER alijitahidi sana kumbembeleza mwalimu mkuu awasamehe ili waendelee na masomo lakini mwalimu mkuu alikataa katu katu na akamwambia Mr. Brown kuwa "MZEE KOSA WALILOFANYA HAWA WATOTO NI KUBWA SANA TENA AFADHALI YA HAWA WENGINE KULIKO HUYU BINTI YAKO JENIFER, JENIFER KWANZA HANA HESHIMA KADIRIKI KUMSINGIZIA MWALIMU WANGU KUWA KAMTONGOZA WAKATI SIO KWELI HUONI KAMA HUYU MTOTO ANAWEZA KUJA KUTUCHAFULIA SIFA YA SHULE YETU? NI BORA NIWASAMEHE HAWA WOTE LAKINI KWA BINTI YAKO JENIFER SIWEZI KUMSAMEHE" ghafla mwalimu mkuu akabadilisha mawazo pale pale akawaambia wale rafiki zake na JENIFER "NYIE NIMEWASAMEHE NENDENI NYUMBANI MKAVAE NGUO ZA SHULE NA MJE DARASANI MUENDELEE NA MASOMO ILA JENIFER SINTOWEZA KUMSAMEHE SAWA?!" wale wanafunzi watatu ambao ni rafiki zake JENIFER walifurah na hawakuamini kama wamesamehewa wakamshukuru sana mwalimu mkuu na wakamuahidi kuwa hawatorudia tena, wakaondoka ofisini na kuelekea majumbani kwao kuvaa nguo za shule. Huku ofisini mwalimu mkuu akanyanyua simu yake ya mezani akampigia Secretary wake na kumuamuru achapishe barua ya kumsimamisha shule mwanafunzi wake JENIFER. Mr. Brown alijitahidi sana kumbembeleza mwalimu mkuu amsamehe binti yake mpaka machozi yakawa yanamtoka Mwalimu mkuu akamwambia Mr. Brown "MZEE HILI NATOA FUNDISHO ILI BINTI YAKO AJIFUNZE SIWEZI KUMSAMEHE MTOTO MSHENZI SANA HUYU" Mr. Brown alimbembeleza sana mwalimu mkuu lakini mwalimu mkuu alimkatalia katu katu kumsamehe JENIFER na akawaomba Mr. Brown na Binti yake JENIFER watoke nje ya Ofisi wasubirie barua ya kusimamishwa shule binti yao. Baada ya muda Secretary alimaliza kuchapa barua na kuipeleka ofisini kwa mwalimu mkuu, mwalimu mkuu akamwita kiranja mkuu wa shule akamwambia aende kupiga kengere ya dharura ili wanafunzi wote wakusanyike mstarini aitoe barua ile hadharani mbele za wanafunzi. Kengere ilipigwa wanafunzi wote wakatoka madarasani na kuelekea mstarini wakakusanyika wanafunzi wote na walimu wote wa shule hiyo, mwalimu mkuu akaanza kuelezea yote yaliyojiri kwa JENIFER na kuwajulisha wanafunzi kuwa kasimamishwa shule baada ya hapo wakateuliwa walimu watatu wamchape fimbo JENIFER kila mwalimu amchape fimbo tatu, kisha wanafunzi wakaruhusiwa waende madarasani kuendelea na masomo yao. Mr. Brown alijisikia aibu sana kwani binti yake JENIFER alichofanya ni kitu cha ajabu hivyo alikua na hasira sana kilichomuumiza ni Ada aliyoitoa shuleni hapo ya kumlipia binti yake akifikiria jinsi alivyoipata pesa katika mazingira magumu ilimradi binti yake asome lakini JENIFER yote hakujali, sasa kivumbi kikaanza kwa Mr. Brown na Mwalimu mkuu, Mr. Brown akaanza kudai pesa ya ada ya mwaka aliyolipa shule akataka arudishiwe pesa yake ukaanza mzozo ofisini kati ya Mwalimu mkuu na Mr. Brown hatimae wakaanza kushikana mashati ofisini, Mr. Brown anataka pesa mwalimu mkuu anasema hatoi pesa ikawa vurumai ofisini