mwisho wakajilaza kitandani wakiwa wamekumbaliana. ?nakupenda sana Julieth na kama Mungu akiruhusu nitapenda uwe mke wangu? James alijitahidi kusema maneno matamu ili kumfariji mpenzi wake huyu mpya ambaye alionekana wazi kutoridhishwa na maamuzi yaliyofanyika. ?nakupenda pia James, ni muda mrefu sana sijapenda kama ambavyo nimekupenda wewe? alisema Julieth na akashindwa kuyazuia machozi yake. ?no no no, don’t cry baby? alisema James huku akimfuta machozi Julieth na kumkubatia tena.
James alikaa na Julieth mule chumbani kwake mpaka akavusha hata muda ambao kipindi kilipaswa kuisha. Julieth alimuelezea juu ya mpenzi wake aliyepita ambaye ndiye pekee aliyewahi kuwanaye, alikuwa ni kijana mwenye asili ya Kiarabu ambaye alikutana naye wakati akisoma O’level, shule zao zilijenga mazoea ya kutembeleana na kufanya mitihani ya pamoja ili kujipima uwezo. Julieth na kijana huyo ambaye alimtaja kama Farid walishindwana kwa sababu kuu mbili, moja ikiwa tofauti ya dini zao lakini ya pili ilikuwa kushindwa kwa Farid kutekeleza malengo ya Julieth ambaye hakutaka kumpa uhondo mpaka ndoa, mwisho Farid alijaribu kumbaka Julieth baada ya kuona kupewa penzi kistaarabu ni jambo ambalo halikuwepo. ?yani
alinitamkia kabisa kuwa hawezi kufanya upumbavu wa kusubiri mpaka ndoa wakati aliona kabisa ndoa kati yetu haikuwepo kutokana na tofauti zetu za dini? alielezea Julieth story ambayo hakupenda kuielezea kwa watu kwani aliona ni ya aibu pia ilikuwa ikimsababishia kulia. ?pole sana, hakufanikiwa lakini?? aliuliza James ambaye alikuwa ameguswa sana na story ile. ?hapana, rafiki yake ambaye tulikuwa kwao wakati hayo yakiendelea alinihurumia, akafanikiwa kuzuia rafiki yake nami nikapata nafasi ya kukimbia? alielezea Julieth huku akifuta machozi. ?wewe ni mwanaume wa tofauti sana, kwani wanaume hutaka mapenzi tu kwa mwanamke lakini nimegundua kwako hicho sio kipaombele? alisema Julieth na kumfanya James ahisi kuwa huenda hiki kilichomkuta huko nyuma ndicho kilisababisha akataka sana kumpa penzi akidhani kama hatompa huenda akamkosa kama alivyomkosa Farid. ?kufanya tedo ni kitu cha ziada tu kama unampenda mtu kwa dhati, kitu cha kwanza ni kuhakikisha anaendelea kuwa wako kwa gharama yoyote, mimi niko tayari kusubiri mpaka mpaka ndoa, wala sitokuwa na lalamoko lolote, alisema James ili kumtoa wasiwasi mpenzi wake huyo. ?no, nimechagua mwenyewe kufanya na wewe, usininyime tafadhali? alisema Julieth.
Jamani mko hai humo ndani?? ilikuwa sauti ya mama yake Julieth akiuliza huku akigonga mlango. Muda ulikuwa umeenda sana James na Julieth wakiwa wamejifungia mule ndani. Walishtuka wakaona kitasa cha mlango kikinyongwa kama mtu aliyeko nje alitaka kuufungua mlango ule, ?mmmh! Mbona mmejifungia?? alihoji mama yake Julieth kwa wasiwasi.
****************************************
ITAENDELEA