Riwaya: SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA..
Mwandishi: SEID BIN SALIM
SEHEMU YA 11
Ilipoishia......
" Unajisikiaje unapolazwa kwenye kitanda cha matibabu kwa ujinga wako wa kushoboka mwenyewe?. Usipende kuyaingilia maisha ya watu usiowafahamu kijana, sio kila tunda lililong'aa unaweza kulila likakuongezea afya mengine yashaoza ndani japo nje yanang'aa ukila tu mara unapoteza maisha, ukitoka hapa kamshukuru sana profesa kwa sababu ndo amefanikiwa kukuombea msamaha lakini ningekupatia vitasa mpaka hiki chuo ukihame, Bora ukorofishane na mvuta bangi mtumia madawa kuliko kukorofishana na mimi ambae sijawai kutumia hivyo vitu ila akili yangu ni zaid ya watu wanaotumia hivyo vitu. Najua ulinitamani kwa sababu mimi ni mtoto mzuri navutia, jicho jicho tako tako na nna vitu vyote vinavyomfanya mwanaume awe chizi, simaanishi wale wasiokuwa navyo hawampati mtu no, ila asilimia kubwa ya wanaume wanapenda mwanamke wa aina hiyo, kama ungenikuta katika enzi zangu ungenipata, ila sasa hivi umechelewa sana na baada ya kunipata ndo kama hivyo unaambulia kipigo, Sorry brother, lile bifu langu limeisha, ila popote utaponiona, nione kama dada yako au mwanaume mwenzako ambae ukinivulia nguo naweza kukutengeneza kama ambavyo mwanaume mwenzako ukimvulia nguo anavyokutengeneza. Good day and!, Samahani kwa maneno yangu kama nimekuboa, but lile bifu letu limeisha. Usimwone kila msichana mzuri unaweza kuupata mwili wake kuuchezea kwa jeuri ya pesa zako au cheo cha wazazi wako, ukiwa hivyo utaumia kwa sababu kuna wanawake wazuri zaid yangu na wao ni vichaa walivuta bangi kabla ya kutoka kwenye matumbo ya wazazi wao zaidi yangu.
Songa nayo......
Alisema lucky kisha akanyanyuka na kuondoka zake, Deniss alimshukuru Mungu maana alishahisi utumbo ndani haufanyi kazi, maneno aliyoambiwa aliyakariri na kuitaji kuyafanyia kazi, aliukumbuka msemo wa waswahili MTU HUJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA nae alitaka kujifunza kutokana na makosa yake binafs aliyoyafanya japo yamempelekea kuumia.
Alirudi room lucky akafungua mabook kwa ajili ya kusoma, moyo wake ulikuwa na morali wa kupitia masomo kutokana na maneno ya profesa aliyoambiwa, aliwaangalia Amina na tunu akawakuta wako bize na mambo yao, kwenye kidole chake cha pili kutoka mwisho kulikuwa na pete mbili tofauti ambazo huwa hazivui kokote anapokuwa, alikisogeza kidole hicho mdomoni akaibusu pete moja ya kwanza kabisa, aliiangalia ndani ya dakika moja na nusu mpaka mbili machozi yakaanza kumbubujika.
" Kweli hakuna wa kumuamini katika maisha zaidi ya mama, yeye pekee ndo anaweza kukuonea huruma pindi utaponyanyaswa akikumbuka uchumbu aliopata leba, nakupenda sana mamaangu na chozi lako unalomwaga juu yangu mpaka kesho daima Mungu atalilipa. nakukumbuka natamani nije niukumbatie mwili wako, ila nahisi nna alegi na hiyo nyumba pamoja na watu unaoishi nao, wewe ndo ndugu yangu wa pekee kwenye hii dunia, siku ambayo mumeo ( edwad ). Na mtoto wako wa kiume ( brayan ) watakufa nahisi ndo siku ntayocheka mpaka jino langu la mwisho lionekane, hawakufanya lolote baya ila nahisi kupoteza malengo yangu na kamwe sitothubutu kurudi nlikotoka nkaipoteza tena furaha yako mamaangu.
Alisema lucky moyoni mwake huku machozi yakiendelea kumtoka, ilivyoonesha alikuwa anamchukia sana baba yake na kaka yake brayan kwa kitu kisichojulikana, mwisho aliuapia moyo wake kusikoitaji kurudi alikokuwa kwa ajili ya kuzuia chozi la mama yake jenipha, alitamani kifo cha baba yake na kaka yake kifike ili afurahi ( Haijulikani walimfanyia nini kipindi ambacho alikiita ni cha enzi zake, lakini anawachukia kuliko maelezo )...
Maryam muda huo huo alikuwa anafika masaki maduka mawili alipoelekezwa na mama yake. foleni haikuwepo kubwa alitumia saa moja na nusu pekee kufika, maduka mawili aliyaona lakini nyumba za eneo hilo zilimchanganya sana, kulikuwa kuna vijana wa boda boda wawili watatu eneo alilopo ikabidi ashuke kuuliza, walipomuona tu jinsi uzuri wake ulivyokuwa unavutia walijikuta wanabadili mada na kuanza kumzungumzia yeye, hadi alipowafikia akawasilimia wote wakaitikia.
" Nzuri mrembo uko poa.?
" Yah namshukuru Mungu. Alisema akitoa miwani. Naitwa maryam, samahanini naulizia kwa mzee edwad.
" Unaulizia kwa mzee edwad?. Walishangaa kuona binti anaulizia kwa huyo baba.
" Yah.
" Wee ni mgeni maeneo haya.?
" Ndio ni mgeni.
" Yani huyo mzee anavyojulikana hapa kisha ukiulizia kama hivyo aisee inashangaza sana, si yule mkewe ni daktari mhimbili?.
" Ndo huyo huyo.
" Pita bara bara hii hapa moja kwa moja, unauona ule mnazi mrefu kule mbele?. Alisema kijana mmoja akinyoosha kidole kumuonesha mnazi uliokuwa mbali kidogo mwendo kama wa dakika tano kutoka hapo.
" Yah nimeuona.
" Basi ndo hapo hapo nyumba nyeupe, rangi yake bado mpya imepakwa juzi si unajua matajiri tena, alafu bati lekundu.
" Nawashukuru sana Mungu awabariki.
" Akubariki na wewe pia mama ee.
" Asante. Alisema akafungua wallet yake na kutoa elfu hamsini akawapatia.
" mtanunua japo maji mpoze kiu ya jua.
" Asante mama asante. Walimshukuru akarudi zake kwenye gari.
" Eh!, huyu dada ana roho nzuri kama yeye mwenyewe masikini ya Mungu asante mama. Alisema mwenye boda boda.
" Mnadhani nisingekuwepo mimi mungezipata hizo?.
" Kwa nini tusizipate.
" Dem kaangalia face hii, kaona ameelekezwa na kijana mwenye sura nzuri nini chotara la kipemba ndo maana katoa.
" Toka zako mjinga wee msiiu!, mtoto katoa kwa roho yake nzuri inavyomtuma, angeenda kumpa mbuzi basi maana hata yeye sura anayo, mtoto ana roho nzuri wewe yule sii nyie mna roho kama bamia.
Walizozana wakawagawana pesa na kumuombea dua maryam ili Mungu amuongoze, elfu 50 ilikuwa pesa ndogo sana kwake kutokana na maisha ya kishua aliyonayo ila kwao unga unga hasa kwa maisha ya kibongo ilikuwa pesa ndefu...
Alikanyaga mafuta hadi kwenye mnazi alikoelekezwa, alipoangalia kweli nyumba yenye rangi nyeupe bati lekundu aliiona, alisogea kwenye geti akapiga honi na kutokea kijana mmoja aliekuwa mlinzi wa getini.
" Sorry hapa ndo kwa mzee edwad?. Alifungua kioo cha gari akamuuliza kijana huyo aliefahamika kwa jina la kaiza.
" Yah ndo hapa unamuitaji?. Aliuliza kaiza. Kabla ya kujibu kwenye mlango mdogo getini alitokea mwanamama aliekuwa amevalia dela zito na mtandio mkubwa wa kutupia kichwani.
" Unafanya nini huko nje?. Aliuliza mwana mama huyo.
" Kuna mgeni hapa namsikiliza.
" Nani?.
" Simjui ni mwanamke.
" Rudi ndani ntaongea nae.
Kaiza alirudi ndani mwanamama akatoka nje karibu na gari la maryam.
" Binti unasemaje?. Aliuliza.
" Shikamoo.
" Kabla sijaitikia shikamoo yako nambie unasemaje.
" Samahani mama nlikuwa naulizia kama hapa ndo kwa mzee edwad.
" Unamuuliza kwa ajili ya kufanya nae biashara za umalaya sio?. Hivi binti hamjui kama huyu mzee ana mke na familia inamtegemea?. Kwa kuwa mnajua ana mali hamjali hata umri wake mnajiegesha tu kwake sio ee. Alisema mama huyo kumwambia maryam maneno yalimfanya bi dada ajisikie vibaya sana, hakujua kwa nini ameambiwa hivyo ila moja kwa moja akafahamu kuwa huyo ndo jenipha mwenyewe mke wa mr edwad. Na kwa picha iliyokuwepo ilionesha mzee huyo hajatulia anafanya umalaya wa kupindukia kwa vitoto vidogo ndo maana mama yake akamwambia sii mtu mzuri.
" Mamaangu mimi ni kama mwanao, naomba utumie busara za kiumama kunikaribisha kwako. Sii kila msichana utaemwona ana tabia mbaya za kutembea na mume wa mtu, shida ya kuisaidia familia yako ndo imenifikisha hapa, nna moyo mwepesi wa kumsaidia mtu nnapoona ana matatizo, ila nafika tena kwa tabu kubwa ya kuelekezwa kisha unantukana kama hivyo mamaangu kweli?. Nsamehe bure na sikulaumu kwa sababu najua nini una maanisha, Naitwa Maryam ni mwanafunzi wa chuo kikuu dar es salam, nna kitu muhimu naitaji kukueleza kuhusu Mwanao LUCKY, au wewe sio mama yake?. Alisema maryam na kumfanya jenipha ashtuke, alijikuta sura yake inanywea kwa maneno aliyoongea kumtamkia maryam na kitu anachoambiwa muda huo.
" Lucky?. Aliuliza kwa mshangao.
" Yah lucky.
" Lucky huyu huyu mwanangu precious lucky?. Aliendelea kuuliza kwa mshangao jenipha, macho yalibadilika maryam nae kidogo nae akashangaa, jina la precious ndo kwanza alikuwa analisikia kwake hakuwai kusikia kama lucky anaitwa precious, ilibidi amwitikie tu hivyo hivyo, ndipo mamaa jenipha alimuomba bibie amsamehe kisha akamuitaji kaiza afungue geti kubwa ili gari la maryam lipite ndani, alijua uenda kuna mengi kweli anaitaji kuambiwa kwani mwanae ana siku nyingi sana ajamtia machoni..
Maryam alipita kwenye geti hadi ilipokuwa paking, kulikuwa na magari zaidi ya kumi ya bei mbaya macho yakamtoka, alipaki gari lake akashuka ndani ya mchuma na kuongozana na ma jenipha hadi ilipokuwa seble ndogo ya faragha, alikutana na sura nne tofauti wanaume wawili nmmoja mzee mzee ambae alihisi uenda ndo mzee edwad mwenyewe na mabinti wawili, alikaa kwenye sofa akasalimia jenipha akaenda kwenye friji kumchukulia kinywaji.
Baada ya kumletea alimkaribisha sana akamtambulisha watu walioko mbele yake.
" Binti huyu ndo mr edwad mwenyewe uliemuulizia, huyu ni mwanangu anaitwa brayan, na hawa ni wadogo zangu wananisaidia kazi za ndani kutokana na ubize nlionao.
" Ok nashukuru kuwafahamu, mimi kama nlivyokuambia hapo awali naitwa Maryam natokea mbez beach samaki ila niko chuo kikuu. Huruma yangu ndo imenifikisha hapa, na nimeumia sana uliponambia maneno nsiyoendana nayo kabisa mamaangu. Chuoni nna mwaka mmoja na miezi sasa, katika room nnayokaa bweni nna binti naishi nae, tokea niishi nae simjui baba yake mama yake wala ndugu yake yoyote, nkimuuliza kuhusu familia yake anasema ana mama tu duniani hana ndugu mwengine yoyote, maisha yake yako tofauti sana na wanafunzi wa chuo wote, anaweza kuwa amekaa akaanza kulia ukimuuliza kwa nini anasema tuachane nae, so hicho kitu kimeniumiza sana na nimefanya juu chini kuhakikisha nnamsaidia kwa kutumia pesa au njia nyengine aweze kurudi katika hali ya kawaida baada ya kugundua hayuko sawa. Mimi pekee ndo rafiki yake chuo kizima, Anaitwa Lucky na bicha yake hii hapa sijui kama ndo mwanenu au nimekosea nirudi nyumbani. Alisema maryam watu wote wakiwa wanamsikiliza, alikuwa vizuri katika uongeaji kitu kilichopelekea kila mmoja kupenda ongea yake, mwisho alimpatia jenipha cm yake aangalie picha ya lucky kama ndie mwanae au sie..
Lilipotajwa jina la Lucky mzee edwad na brayan waliangaliana, walionekana kupitisha mshangao wakakaa vizuri kuiona hiyo picha kama ndie au hapana.
Jenipha alipoiona picha tu hapo hapo alitoa macho ya mshangao akaweka mkono mdomoni, machozi yalianza kumtoka kilio cha nguvu nacho kikapisha hodi, alimpatia cm mtu mwengine akaangua kilio kilichomfanya mwanae wa kiume brayan amsogelee na kumuitaji anyamaze. Alimuomba mama yake anyamaze akaishika cm na kuiangalia picha, kweli alikuwa lucky mwenyewe akamuangalia baba yake na kumuambia ndie, Mzee edwad alihisi presha kupanda akapata mshtuko kwa kuambiwa hiyo ndo picha ya mwanae, chozi la kiutu uzima lilimtoka akachukua kitambaa cha kujifutia akajifuta..
" Ina maana mwanangu lucky yuko mzima?. Aliuliza mzee edwad akimwangalia maryam.
" Ndio baba. Alijibu. Mzee edwad nae alianza kugugumia kwa uchungu, alionekana kuumia sana.
" Ooooh my daghter uko wapi mamaa siku zote hizo?. Alisema mzee edwad huku brayan nae machozi yakianza kumtoka..
" Ina maana bado uko hai?. Alisema mzee edwad.
" Mwanangu uko wapi mwanangu. Alisema jenipha akiwa analia.. Mwanangu umenifanyia nini mwanangu rudi mama mama yako nakufa mimi, umeniua mwanangu kwa nini umefanya hivyo jamaniiii Hiiiiiiiiiiiiii hiii hii hiiiiiii, Mwanangu najua ulikufa tukakuzika kabisa kumbe uko hai kwa nini walimwengu wako hivi mama jamaniii, kaburi lako kabisa lipo lucky lipo lipo lipo kumbe uko hai uko wapi kama hujafa mwananguu!!,, yuuuuuu mwanangu mimi, binti niambie ukweli mwanangu yuko wapi nimfatee mimi, nakufa mwana wa marehemu mimi jenipha jamaniii huuuuuuuuu, Ukoo wako wote unajua ulishakufa na kila siku tunaenda kaburini kwako siamini mimi siaminiii hiiiiiiiii hihihihiiiiiii..... alilalamika jenipha kwa kilio cha kupanda na kushuka huku mwanae brayan akimbembeleza aweze kunyamaza.
** Kwa nini familia inajua lucky amekufa?.
** Kwa nini Lucky anamchukia baba yake na kaka yake wakati wao wanaonesha kumpenda na kumkumbuka kutokana na taarifa za uzima wake walivyozipokea?
** Maryam yupo katika hali gani baada ya kupata hizo data za kugundua Lucky kwao anajulikana alishakufa?.
** Kitu gani kilipelekea hadi lucky kujulikana amekufa wakati yuko mzima ?
NINI KITAENDELEA KATIKA EPISODE YA 12 ?