TAFUTA HAPA

Hadithi:Penzi La Mpangaji Sehemu Ya #1

Mnamo mwaka 2008, nilimaliza kidato cha nne katika shule ya Tabora Boys. Baada ya kumaliza shule,nilirudi zangu nyumbani Morogoro kwenye nyumba ya baba na kuanza maisha mengine kama raia wa kawaida.Nyumba ile ilikuwa kubwa sana, na ilionekana kubwa zaidi baada ya kaka zangu kuondoka na kwenda kuanza maisha ya kujitegemea. Kaka yangu wa kwanza alienda Arusha, wa pili akaenda Dar na wa tatu yeye alienda Dodoma, hiyo yote ni katika saka za maisha.
Shule niliyotoka yaani Tabora Boys, kwa kifupi ilikuwa haina wanawake. Wanawake tulikuwa tunaonana nao Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo tulijumuika nao pamoja katika ukumbi wa chuo cha Uhaziri kilichopo pale pale Tabora. Yaani namaanisha kuwa, kila ilipofika Ijumaa ya mwisho wa mwezi, zile shule zilizokuwa na jinsia moja pale Tabora ,zilikutana na kubadilishana mawazo huku wale wenye wapenzi wakienda mbali zaidi kwa kubadilisha na kukabidhiana viungo vyao vya mwili.
Mimi nilikuwa msanii tu! Yaani sina demu wala nini, tabia yangu ilikuwa ni kuchukua wasanii wenzangu wale wasiokuwa na wanaume. Kwa siku hiyo moja ya Ijumaa, niliweza “kugonga” watoto si chini ya wawili,kila mmoja kwa wakati wake.Tabia hiyo ilikomaa sana katika mwili wangu,kitu ambacho kilisababisha niwe kila wakati nataka “kula mizigo” . Hivyo pindi hamu ilipokuwa inanikamata sana,nilijifanya naugua ili wanitoe nje ya shule eidha kwa kunipeleka hospitali au kunipa rikizo ya muda mfupi.
Kitendo cha wao kunipa nafasi hiyo, kilinifanya niwe natoroka mahala wanaponiacha na kwenda zangu sehemu zangu maalum kwa ajili ya kujichukulia “mizigo” ya “kugonga”, na pindi nilipokuwa nakosa sana mizigo hiyo, basi nilihamishia majeshi yangu kwa yeyote nitakaye kutana naye lakini wa jinsia ya kike.
Nakumbuka siku hiyo nilishikwa na hamu ya kufanya ule upuuzi kiasi kwamba nilishindwa hata kwenda darasani. Kitendo kile kilifanya yule msimamizi wa wanafunzi pale shuleni kuniona kama naumwa,hivyo aliniongoza hadi hospitali moja ya pale Tabora na nilipofika, ndipo nikajidai naumwa zaidi.