Sikuwa na sababu ya kupaparika na Stela hata kidogo kwa sababu alikuwa ananiambia siri nyingi sana za kwake na za nyumbani kwao.Ila alipokuja kuaribu na kufanya nianze kutaka kumla haraka,ni siku moja alikuja ndani kwangu na kukaa na mimi kisha kuanza kuongea yaliyomsibu siku hiyo mtaani.
“Eti Prince, unamfahamu Lameck?”.Alianza kwa kuniuliza swali hilo.
“Lameck yupi Stela”.Nikamuuliza na mimi.
“Si yule msanii sanii anayekaa kwa Mama Tonga”.Akajibu.
“Ahaaa,kile kinachovalia suruali magotini?”.
“Ha ha haaa,mi sijui. Ila yeye mweupe kidogo,anapenda sana kukaa dukani kwa Mangi”.
“Ee, nishamjua. Kafanyaje kwani”.
“Mmh,eti mmh”.Akawa kama anaona aibu kuniambia.
“Nini? Mbona una guna guna tu!”.
“Eti leo wakati natoka shule akaniita pale dukani kwa mangi halafu akaanza kunitongoza. Halafu alipomaliza akasema nisimpe jibu niende kumfikiria”.Alivyosema hivyo moyo wangu ulijaa na hasira za ghafla,nikatamani nikifate hicho kitozi kinyesi,lakini Prince Mukuru nikajikaza na kuendelea kudadisi.
“Kwa hiyo wewe umeshamfikiria?”.Nikamuuli
za.
“Ha ha haaa,hivi kijitu kama kile mimi nitakipeleka wapi? Nguo zenyewe kina azima,nauli ya kwendea shule anamgongea mlangoni mama yake asubuhi. Sasa atanipa nini yule”.Nilitabasamu kidogo baada ya kusikia hayo, kisha nikajisemea moyoni kuwa,watoto wa kike ni wajinga sana. Yaani yeye anadhani kuwa na mvulana,ni lazima mvulana huyo awe na kitu. Licha ya kuwa na kitu,vile vile ni lazima awe anapewa vitu hivyo yeye.Nikacheka kidogo na kuendelea.
“Sasa kwa nini usimkubalie tu!?”.Nikamuuliza huku natabasamu,wakati huo ilikuwa ni kama njia ya kuonekana sina haja naye.
“Wewee huu mwili wa almasi,hauguswi na mkaa “.Akajibu huku akisimama na kujiangalia angalia.
“Ha ha haaa,kwa hiyo Meck ni mkaa?”.
“Yaani zile ni levo za mkaa,nikimaanisha thamani yake ni mkaa na yangu ni almasi”.Bado niliamini kuwa Stela yupo kimaslahi zaidi na ndio maana aliongea vile.