TAFUTA HAPA

Hadithi:Penzi La Mpangaji Sehemu Ya #12


“Dogo, dogo, dogooo. Sisi ndo wakubwa hapa. Yale mavazi tunayo na hawa wauguzi niliwaambia yule ni mdogo wangu na wewe ni mdogo wangu,hivyo yeye alikuwa kama anakuangalia wewe hapa”.Alijibu jamaa.
“Ha ha haaa, kweli umecheza hapo”.Niliongea huku nampa tano.
Baada ya hapo tuliongea maongezi mengine na baadae alikuja mwalimu wangu na tukaenda shuleni huku nikimuahidi yule jamaa muuguzi kuwa nitakuwa namtembelea mara kwa mara. Hizo ndizo zikawa tabia zangu pale shuleni nikizidiwa na hamu ya kufanya uasherati.
**********
Baada ya kumaliza elimu yangu ya kidato cha nne, ndipo niliporudi Morogoro iliponyumba ya Baba na nikaanza maisha ya uraia. Kwa kuwa sikuwa sana mzoefu pale Morogoro,zile tabia zangu za kishetani nikawa nimezificha kiasi chake hadi pale kaka zangu walipoamia kwenye makazi yao binafsi.
Walipoondoka ile nyumba ikawa kubwa sana,hasa ukizingatia kuwa baba alikuwa ni mtu wa kusafiri safiri sana,si mwajua kazi za treni?. Ndipo baba aliamua vile vyumba vingine viletwe wapangaji ambapo kodi ya pango itakayopatikana, asilimia 70 nitachukua mimi kwa ajili ya kujikimu maisha yangu hasa kimavazi na mambo mengine madogo madogo.
Tulipata wapangaji watatu, lakini kuna mmoja yeye alikuja na familia yake yote. Bwana yule alikuwa ni mwalimu wa Sekondari na mke wake alikuwa anafanya kazi kwenye kiwanda cha sabuni cha pale pale Moro.
Walikuja na mtoto mmoja ambaye walisema ndiye mtoto wao wa kumzaa,aliitwa James. James alikuwa ana miaka kama kumi hivi na alikuwa darasa la tatu. Pia katika familia hiyo waliambatana na mfanyakazi wa ndani aliyeitwa Maimuna, na pia alikuwapo mtoto wa kaka yao ambaye yeye aliitwa Stela.
Stela alikuwa kidato cha pili na alikuwa ni mzuri balaa. Kabila la wapangaji wale ilikuwa ni Wanyaturu, kabila ambalo lilibarikiwa kuwa na wananchi weupe na wenye kila sifa za kuitwa wazuri