TAFUTA HAPA

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 8)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM.

SEHEMU YA 8

Wakati wao wanaingia ndani upande wa pili  Hamad na Ticha wakiwa njiani wanarudi mjini ghafla walikutana na gari nyeusi imezuia bara bara mbele yao, walipata mshangao sana wakapunguza mwendo kisha wakasimama, upande alikokuwa amekaa Ticha alitokea mtu amevaa nguo ya kumfunika uso wake kama gaidi akamtandika Risasi Ticha na kutoeka. Alikimbia fasta mpaka kwenye gari hilo leusi lililokuwa limezuia bara bara kwa mbele akaingia ndani na kukanyaga mafuta, tairi zilizungushwa, rami ikasuguliwa vizuri jamaa akatoeka kimuundo huo akimuacha ticha katika wakati mgumu wa jeraha, risasi ikimpatia maumivu makali mno ya kushindwa kustahimilia na kupoteza fahamu.
*****

Seid na mama yake waliingia ndani wakiwa na furaha ya kutembelewa na wageni na kuachiwa chochote kitu, walijua siku hiyo uhakika wa kula vizuri upo.

"Mama leo nadhani tunakula nyama. Alisema Seid akiwa amekaa chini amejiegamiza ukutani na mguu mmoja kuusimamisha, alimuangalia mama yake aliekuwa anajifuta futa jasho usoni kwa kutumia khanga yake aliyokuwa amejifunga.
"Heee mwanangu unawaza kula tu wewe baba.
"Sasa tufanyie nini hiyo fedha uliyopatiwa?. elfu 20 chukua kumi lete tule vizuri leo.
" Ila kweli mwanangu, basi hapa itabidi uchukue baiskel yako uende sokoni uchukue japo nyama na viungo viungo hivi, Mu