TAFUTA HAPA

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 6)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA 6

Bora nikose kibarua kwa ajili yako madam, naomba unisubiri hapo nje niende nimwambie nimeacha kazi ili japo tuongozane nipajue utapoishi kwa sasa, tuendeleze udugu wetu sababu umenisaidia mengi sana ambayo yalinifanya nikuone wewe ni miongoni mwa watu wachache ambao bado wapo katika dunia hii ya sasa, nisubiri madam nikaage kuacha kazi, kama kazi nitapata kwengine tu.

"Hapana naomba usifanye hivyo, usiache kazi kwa ajili yangu, utanipigia cm na ntakuelekeza siku moja utakuja, hii kazi ndo inayoingiza Riziki yako usifanye hivyo kabisa. Ni maneno nliyomuambia, nkamueleza tu aishi nae vizuri hata huyo alieingia ili kulinda kibarua chake.
Nlimuomba anifungulie mlango niondoke, nlitoka na kukodi tex nkaja hadi kwa bibi yako.

Nliishi na bibi yako kipindi chote cha mimba, bado sikukata tamaa nkijua uenda Mungu atamrudisha nyuma mume wangu akumbuke tulikotoka lakini wapi, nlikuja kuamini kuwa ndo basi tena siku moja nikiwa shambani kwenye hili shamba tunaloishi. maana alisema ameniachia shamba lote. nilikuwa nalima lima ghafla nkaona linapaki gari kubwa na dogo, dogo alikuwemo yeye na huyo mwanamke wake, kubwa walijaa vijana ambao walishuka akawapa kazi ya kuvuna kila kilichoko shambani, sikuweza kuwazuia kwa sababu mwenye mali tayari alikuja, walipo maliza kuvuna akiwa peke yake nilimuuliza.
" nimekukosea nini lakini mume wangu mpaka unafaya haya yote.  hakujibu swali langu zaid ya kunisonya akaenda alikokuwa mwanamke wake, wakaingia kwenye gari na kuondoka.

Mimba tayari ilishakuwa kubwa, nliteseka sana mimi mwanangu, nlilazimika kubeba mzigo wa kuni wakati tumbo tu lilikuwa mzigo tosha kwangu, kiukweli mpaka najifungua nlipitia mengi sana, nlipojifungua ndo nkahamia hapa kwa sababu kwa bibi yako kama unavyopaona kuna chumba kimoja, nliumia sana mwananguuu miimii, baba yako alinifanyia visa vingi sana ambavyo hata vingine havielezeki, naumia miimii naumia mwananguuu nkizingatia nlimueshimu sana Masoud laki ' Laki ' Lakini..
*****

Mama hakuweza kumalizia neno lakini, alianguka kitandani akiwa tayari amepoteza fahamu, nliumia sana kupata story nzima ya baba, machozi wakati wote yalikuwa yakinitoka, nlijikuta nkijuta kuuliza maswala ambayo yalipelekea mama kupoteza fahamu. nilianza kuita Mama! , Mama!, Mama amka lakini hakuamka. ndipo nilichanganyikiwa nikihisi labda amekufa.
Nilikumbuka darasan kwenye somo la kiswahili tulifundishwa namna mtu anavyoweza kuzirai au kuzimia na kupoteza fahamu muda wa nusu saa au saa, nilijikaza kiume nikachukua mfuniko wa ndoo na kuanza kumpepea nikiwa nalia huku nkisikilizia ikifika nusu saa bila kuamka niende kuita majirani waliokuwa mbali kidogo.

Namshukuru Mungu hazikupita dakika kumi mama aliamka, nikamuomba anisamehe sana kwa kumkumbusha machungu ambayo tayari yalishaanza kufutika moyoni mwake, niliumia sana kiukweli siku hiyo, nilimlaani sana baba yangu japo mama alishanambia nsimchukie aliemfanyia ubaya mtu muhimu katika maisha yangu, lakini nlitengeneza chuki na kuwachukia wanaume wote wanaowanyanyasa wanawake.

Tokea siku hiyo nikawa nasoma kwa bidii sikuwa na mchezo kwenye masomo, rafiki asieitaji kusoma sikumuitaji, nilikuwa beneti na wale wenye akili tu pamoja na walimu. nkisoma kwa uchungu ili ikiwezekana siku moja jina langu liwe miongoni mwa majina makubwa Tanzania nimsaidie mamaangu kipenzi alopitia maisha magumu kiasi cha kuwa magumu kwa ajili yangu...
*****

Hizo zote zilikuwa kumbu kumbu za kijana aitwae Seid akikumbuka stori aliyopewa na mama yake kuhusu mambo aliyofanyiwa na baba yake. kumbu kumbu alizozikumbuka akiwa amelala chali kwenye kitanda baada ya kuwa amefanya shughuli za kutwa nzima.

Zilimfanya amkumbuke sana mama yake aliekuwa ameenda kulala kwa bibi ndani ya usiku huo, macho tayari yalishavimba kwa machozi baada ya kukumbuka kila kitu alichofanyiwa mama yake huku akijisemea moyoni.
" Mungu nisaidie matokeo yangu ya form Six yatoke yakiwa mazuri niingie chuo nije nimsaidie Mama. sijui kwa nini wanaume tunakuwa hivi, ila yote sawa tu mungu yu pamoja nae, Umenisomesha kwa tabu nyingi sana mama yangu, zidi kuniombea nifaulu nkusaidie mamaa umeteseka sana.

Seid alifuta machozi yake yaliyokuwa bado yanaendelea kutoka kutokana na mambo mazito aliyoyakumbuka yaliyotokea miaka zaidi ya 11 nyuma, aligeuka akalalia ubavu wa kulia akazima kibatali na kulala usingizi.
Asubuhi na mapema alipoamka alichukua Jembe na panga akaingia shambani kwa ajili ya kupariria baadhi ya mazao na kuchanja kuni.

Tokea azaliwe mpaka anafikisha umri wa miaka 20 hakuwai kumuona baba yake na wala haitaji kumuona kwa matendo aliyoyafanya. aliendelea kuishi na mama yake akiishi maisha ya kipekee kuliko kijana yoyote, alimpenda mama yake kuliko chochote na kumtii kwa kila kitu alichoambiwa akiamini huyo ndo Mungu wake wa pili....

Mwili wa kijana huyu ulikuwa umetanuka mfano wa miraba sita kutokana na kazi nzito alizokuwa akizifanya kuingiza japo pesa ndogo ya kupata hata mboga na chakula chengine, maisha ya tabu yote kijana huyu aliyapitia, kuna muda alihisi mungu hawaoni yeye na mama yake ndo maana wanateseka, huku akijiuliza kwa nini wengine wanajenga majumba ya kifahari wakati wao hata ya udongo hawana.
Ilipofika mida ya saa tatu Bi najma alirudi toka kwa mama yake na kumkuta kijana wake shambani, alimuita mwanae. Seid aligeuka akamuitikia na kumsalimia.

" maraaba mwanangu pole.
" nshapoa mama hawajambo huko?
" ndio mwanangu hawajambo.
" Vipi umenisalimia kwa bibi?
" ndioo!! na yeye anakusalimia.
" Aya sawa mi nipo, namshukuru Mungu umerudi mamaangu, kwa sababu dah usiku nimekuwaza sana, hivi ule unga jana uliisha?. Alisema mwisho akaulizia mambo ya msosi.
"Hapana ulibaki kidogo tu, usijali lakini kuna mchele nimekuja nao kutoka kwa bibi yako shambani.
" wao leo kumbe wali!? hadi raha ukisikia mtoto hatumwi dukani mamaangu ni hapo.
" Uhm hujaacha tu mwanangu?. alisema bi najma huku akiinama na kunyukua vigugu vilivyokuwa vimebakia sehemu aliyolima mwanae.
" Mtoto hakui kwa mama wee, hapo mboga tu ndo tatizo sasa maisha haya!. aliongea akisimama kumuangalia mama yake.
" Ah! hata tukila hivi ivi sawa tu mwanangu ndo maisha yetu tutafanyaje? ukishakuwa masikini unatakiwa ukubaliane na kila kitu, ebu lete jembe nikusaidie upumzike kwanza.
" Acha tu mama hii ni kazi yangu kama kijana vile vile kumsaidia mama. alisema akaangalia mfukon kama kuna chochote akabahatika kukuta mia tano.
" Nna mia tano hapa bora tununue dagaa tonge la mia tano tuchemshe tutolee kuliko kula hivi ivi.
"sawa si mbaya pia. Alisema bi najma.

Kabla ya kuendelea kupariria seid cm yake iliyokuwa mfukon ilianza kuita, alishtuka akapapasa mfuko haraka na kuitoa, kabla ya kuangalia nani anapiga alitikisa kichwa kisha akamuangalia mama yake, bi najma alimuuliza.

" nini?
"Ni aibu mamaangu hii, vijana wenzangu wanatumia masamsung makubwa makubwa, matarch, mimi natumia samsin jamaniii!!.
" Ebu pokea kwanza cm mwanangu hayo mengine yatafata hee!!. Seid aliangalia kwenye screen akaona jina "Ticha". alipokea huku mama akitikisa kichwa na kusema chini chini " jamani shida hizi, mpaka mtoto anajisikia vibaya!"

"Haloo Ticha Salam alaykum.  Alisema seid.
"W/ssalam vipi hali bosi wangu. Alisema wa upande wa pili.
"njema tu mungu anasaidia.
"Uko wapi?
"niko shamba kwetu huku kiwengwa.
"Ok matokeo yanakaribia kutoka kijana, juzi nlienda wizara ya elim nkaona nikuibie vitu. e bhana ndugu yangu umepasua. Alisema wa upande wa pili..
"Ticha nimepasua nini tena?. aliuliza seid akiwa anaachia jembe.
"Yani matokeo yako yako vizuri vibaya mno, umewaburuza Seid form six niamini mimi.
"Eee!!!

Seid hakuweza kuongea chochote, alikata cm uso wake tayari ukiwa umepagawa, japo aliambiwa ni ya kuibia lakini alijikuta na furaha sana, machozi yalianza kumlenga lenga mama yake alisogea karibu na kumuuliza.
" mwanangu vipi! kuna nini?.
Seid hakuweza kujibu, alimuangalia mama yake kisha akaangalia pembeni, macho tayari yalishajaa machozi, mama yake alimuuliza tena.
"Nini mwanangu mbona sikuelewi?
"Mama nimefaulu, Nimefaulu mama!! Eti mimi nimefaulu mimi mama..

aliongea kama mtu asiejielewa, alikaa chini huku akisema Asante Mungu kwa sauti ya kulia, bi najma alimfata na kumwambia ni jambo jema lakini asiamini asilimia mia wakati matokeo hayajatoka, kwa sababu yeye ni maskini matokeo yanaweza kununuliwa pia anaweza kuwa anamtania.

Seid aligeuka na kumuangalia mama yake baada ya kusikia maneno yake.
"Unasemaje mama!, Matokeo yangu mimi yanunuliwe!, sina utani na ticha, ticha ni mtu wangu wa karibu sana lazima alichonambia cha kweli, Mama nshafaulu mimi shida zimeisha, najua naingia chuo mama, naingia tu chuo mimi, Eh asante Mungu.
"Mwanangu ebu punguza munkari!, subiri kwanza hadi yatoke ndo uwe na furaha ya kufaulu kiasi hicho, usiwe hivo wewe ni mtu wa chini mwanangu, mara ngapi matokeo yanachukuliwa na watoto wa wenye mali?
"Mama Mimi ataenunua matokeo yangu Akyamungu naapia mbele yako Namuua,nimekulia kwenye maisha ya shida nna dhiki mpaka nazichukia, kitabu mimi ndo kitaniokoa leo mtu anunue matokeo yangu, nafungua mashtaka au nampiga kipande mama, vyote vikishindikana mimi napelekwa jela nakuapia mamaangu, shida nlizonazo hizi watu walete habari za ujinga naua mimi naua Akyamungu!!!!.

Alijikuta anaongea vitu kwa kupanic baada ya kuambiwa habari za ununuaji wa matokeo wakati ameambiwa kabisa na ticha wake kuwa amewaburuza form six.
"Tumuombe mungu nshallah kwa uwezo wake utapita ila si kujipa uhakika kiasi hicho, kuna mengi pengine jina lako kalifananisha, usiwe na furaha ya kiasi hicho mwanangu.
"Dah mamaangu kipenzi mbona hivyo!, hakulimiki tena hapa nimefurahi na kutibuka pia tuondoke.
Aliongea huku machozi ya furaha yakiwa ndo yanaishia ishia, alinyanyuka akabeba jembe na kumuomba mama watoke shambani, alifika nje ya nyumba yao akatupa jembe chini kisha akamuaga bi najma kwenda kutafuta dagaa tonge (dagaa wadogo wadogo wabichi).

baada ya nusu saa alirudi akiwa na dagaa waliokuwa kwenye gazeti, alimkuta tayari mama yake ashapika wali, ilibidi amsaidie kupika dagaa walipomaliza waliweka msosi chini wakala mchana ukapita....
Tokea siku hiyo seid alikuwa ni kijana wa kuwaza na kuwazua juu ya matokeo aliyoambiwa na rafiki yake mwalimu wake, kila alivyojiuliza alishindwa kujijibu huku uso ukiwa na tabasam kwa kuyafahamu matokeo yake mapema.

Siku na miezi ilisogea mbele, Seid na mama yake waliendelea kuishi maisha ambayo Mungu ndo alieyajua, walipopata walikula walipokosa walilala, kutokana na nyumba yao kuwa peke yake hakuna alieweza kujua maisha yao yakoje, ilikuwa ni siri yao na Mungu wao pekee...
Miezi sita mbele ilikatika, Tarehe 15 siku ambayo ilikuwa ndo siku ya kutoka matokeo ya form six ilifika. seid hakuwa na nauli ya kwenda mjini siku hiyo ilibidi ampigie rafiki yake anaetumia vifaa vya internet na kumuomba aangalie necta ya form six lakini ilishindikana hakuwa na megabite za kuingilia internet siku hiyo, ikabidi afanye juu chini aende mjini akiwa na furaha ya hali ya juu akiamini moja kwa moja yeye mshindi.

Baada ya kufika alienda hadi sehemu yalipokuwepo makaratasi ya matokeo, alifika huku akiwambia wenzake aliowakuta
" Kabla sijaangalia matokeo yangu nimeota kuwa nimeshinda.

Kimya kimya alifika na kuangalia namba yake kwa kutumia kidole. Ghafla Macho yalimtoka baada ya kuiona, mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio akawa katika hali ya siamini, baadhi ya wenzake walimuuliza.
"Bosi vipi mbona kimya!
lilikuwa swali zito sana kwake kulijibu, machozi yalimtiririka kama baadhi ya wanafunzi ambao walikuta matokeo ya siamini wakashindwa kujizuia na kuangua kilio.

Hakuweza kuamini alichokiona Seid, maswali mengi yaliingia kichwani mwake, akawa na msongo wa mawazo, alihisi presha kupanda na kushuka ghafla, taratibu alianza kuanguka chini na kupoteza fahamu, wenzake waliokuwa karibu walimdaka wakampeleka chini pole pole akiwemo kijana mmoja aliekuwa swahiba wake wa karibu aitwae Hamad...

TUKUTANE SEHEMU YA 07