TAFUTA HAPA

Simulizi: MSAMAHA WA MAMA ( SEHEMU YA 4)

Riwaya: MSAMAHA WA MAMA!
Mwandishi: Seid Bin Salim.

Sehemu ya 4

Mjukuu wangu!, mwaka 1992 wakiwa tayari wana miaka miwili  ndani ya ndoa yao, lilitokea Tukio ambalo sitolisahau katika maisha yangu yote ya duniani, na hicho ndo kitu ambacho nahisi najma ataendelea kulaani juu ya babaako japo yapo mengi mabaya aliyomfanyia na najma kuyavumilia, ila kwa hilo tukio!, Kama baba yako atakaa siku moja chini na kulifikiria, basi naamini siku moja atarudi kwa mama yako akiwa amepiga magoti chini akiitaji msamaha, kwani ni wanawake wachache sana wanaweza kujitolea kwa jinsi alivyojitolea mwanangu najma ili kuokoa maisha ya mmewe.

"kilitokea nini?
Ni swali nlilouliza baada ya kuona amenifumba na mimi nlitaka kwenda nae sawa.

"Swali zuri, mwaka 1992 baba yako akiwa anatoka chuo baada ya kumaliza kufanya mitihani, aligongwa na gari lililokuwa linaenda mbio, na dereva kutokomea kusiko julikana, vijana walioliona tukio hilo walijaribu kulifatilia gari lililosababisha ajali na kukimbia bila kufanikiwa, haraka walimpeleka hospital ya mnazi mmoja darajani. Najma alipopata taarifa alizimia, alipozinduka aliomba aende hospital haraka akamuone mmewe kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo kwake.

Alipimwa ndani ya siku mbili, ndugu wa masoud pamoja na Najma waliitwa ofisini kuelezwa kinachoendelea, ndipo waliambiwa Anaitaji kuongezewa damu na figo ili kurudisha uhai wake kwani figo moja limekufa na lililobakia halina nguvu za kujitemegea.

Mjukuu wangu! ndugu zake wote waligoma kutoa damu kwa Masoud wakidai wana damu ndogo hata figo pia kumtolea walishindwa, mwanangu akasema bora nife mimi kuliko mme wangu, akaomba apimwe damu kama magroup yanaendana atatoa, na kama mafigo yake mawili yanafanya kazi basi atatoa moja, alisema hivyo huku akiwa anabubujikwa na machozi na ishallah machozi aliyoyamwaga siku hiyo mungu atayalipa tu.

Docta alimuomba aingie kwenye chumba cha maabara, alipimwa damu na kukutwa ana group A kama masoud na mafigo yake mawili yako vizuri ndipo opration ya kutoa figo na damu ilianza.

Walifanya opraishen vizuri, baada ya siku kama tano hivi, masoud akawa mzima, alimshukuru sana mke wake, walifurahi sana siku hiyo maisha yakasonga mbele.

Baada ya miezi mitatu, matokeo ya vyuo yalitoka, masoud alipata  maks nzuri, akachaguliwa kuwa miongoni mwa wanafunzi bora wa chuo cha suza, matajiri wenye makampuni makubwa walimuita kwa ajili ya kuongea nae ili awafanyie kazi zao za kiofice, Mungu akamuwekea wepesi na kufanikiwa kujiunga na kampuni moja kubwa tu iko huko mjini.

Ilikuwa ni kama sherehe kwa najma, Hakuamini kama mme wake atapata utajiri wa mali ndani ya miaka michache kiasi hicho, aliinua mikono yake juu mwanangu na kumuombea mmewe kwa mungu ili mali zake ziwe na baraka.

Masoud baada ya kupata kazi kutoka kwenye makampuni yaliyokuwa yanaongozwa na wazungu, alikabidhiwa nyumba na gari la kutembelea, Walitakiwa wahamie mjini yeye na mke wake. ndugu wote waliitana wakaandaa kashuguli kadogo ka kumuombea dua. Alimchukua mkewe pamoja na ndugu zake wengine wakaenda mjini kupaona.

Najma hakuamini kama ipo siku moja angeishi kwenye nyumba ya kifahari haraka hivyo, siku ya kwanza alipofika alizimia zaid ya mara moja kwa sababu ya mshangao, wapo baadhi walimcheka kwa ushamba lakini haikuwa ushamba bali mazingira tu yalimchanganya, tokea kuzaliwa kwake alikuwa hajawai kukanyaga kwenye nyumba yenye mandhari nzuri..

Masiku, wiki, miezi ilikatika baada ya kuamia mjini, shida zote ziliwakimbia na utajiri kupisha hodi, unene ulianza kuiandama mili yao kutokana na kurizika na vyakula wanavyokula, namna walivyokuwa wametakata kwa pesa hukuweza kuwajua kirahisi kama ulipotezana nao miezi mitano au zaid.

Nakumbuka siku moja mwanangu alikuja kunitembea akiwa na gari dogo la kutembelea, tuliongea mengi akanipatia pesa za matumizi, ila katika maongezi yetu nkamwambia "mwanangu, mali hizo ni za mwanaume, siku yoyote anaweza kukuacha na wanaume wa siku hizi wasivyokuwa na haya,  anaweza asikupe chochote japo mali mmechuma wote, hivyo basi kuna kijishamba kinauzwa hapo jirani laki tatu na nusu, inabidi ukinunue kisha uweke watu wajenge japo kijibanda, maisha yanaweza kukushinda huko utakuja uendelee na kwako.

Mwanangu hakuwa mbishi, alinisikiliza ila akanambia sasa hivi hizo pesa hana akipata tu atakuja kulinunua, sasa sijui alisahau! au vipi maana sikumuona tena.
Maisha yao yalisonga mbele, shamba kubwa la masoud lililokuwa huku kijijini, kwa kuwa walikuwa hawaishi tena, nyumba iliyokuwa imejengwa ndani ya shamba iliendelea kuwepo, waliitwa watu wakalima mpunga, na mazao mengine ambayo walihisi badae yatawaingizia faida.

Mjukuu wangu mimi niishie hapo!!, mengine itabidi ukamuulize mama yako nahisi atakuambia, mbane usimpe nafasi japo yanamuuma lakini atakuambia tu kwa kuwa ushaupata mwanzo wake, akikusimlia yeye ni vizuri zaid kwani kuna vya siri nsivyovijua na wewe kwa kuwa unaonekana kuwa tayari una akili anaweza kukuambia, cha mwisho nnachokumbuka mimi, ilikuwa ni usiku wa tareeeeeeeee!  12 mwezi wa 5 mwaka 1993 ambapo tayari alikuwa na mimba yako, alikuja hapa akiwa analia na kijibegi flan hivi kidogo, kumuuliza kulikoni akasema "mama wee acha tu, sikuamini kama masoud anaweza kunifanyia hivi mimi? nliyoyashuhudia kwake yanatosha, na alivyonitesa mimi nkavumilia vyote na mwisho kudai talaka yangu mungu atanilipia tu, kwani nimemvumilia vya kutosha, kiukweli mamaangu bado siamini kama kupata mali tu angebadilika kiasi hiki.

sikuitaji kumuuliza zaid kwa sababu wanaume mi nawajua hasa wakishapata mali, sikumshauri akadai haki yake wala nini, kwa sababu asingeweza kutokana na upole alionao mamaako, nlichomuambia akae chini amuombe mungu wake atamsaidia, wasipolipana hapa duniani basi watalipana kwa mungu.
Ila kwa alichomfanyia kama amefanyiwa kweli mambo aliyoniadisia basi naamini ipo siku moja tu mungu ameipanga kwa kuwa malipo hapa hapa duniani!!, hatta siangaiki najua ipo siku na sisi tutacheka tu kumuona masoud akidhalilika, na kiungo cha mwanangu kilichoko mwilini mwake Nshallah kitamtafuna taratibu!. Alisema bibi.

"Bibi naomba unambie tu kila kitu nadhani mama hatoweza kunambia chochote mimi!

nliongea huku machozi yakinilenga, nlijikuta nkijuta baada ya muda mrefu kumuhisi mama vibaya kumbe alitendewa unyama kwa mujibu wa maneno ya bibi, bibi nae japo macho yalikuwa yakizee lakini yalianza kuiva alipokumbuka mambo yaliyomkuta mwanae, alinigomea kabisa kunambia chochote kilichoendelea, tayari nlishakuwa na mzuka wa kujua kila kitu kilichomtokea mama, sikupoteza muda nlimuaga bibi na kumuambia ntakuja kukusalimia kesho, nlitoka mbio mpaka ndani nkachukua baiskel yangu na kuanza kurudi nyumbani haraka, njia nzima moyoni mwangu kulikuwa na maneno ya" Lazima leo mama anambie ukweli wote sikubali, kumbe baba yangu ndo mshenzi wa tabia hayawani mkubwa!!!.

kama pedeli zingekuwa zinaongea nadhani siku hiyo zingeongea kuwa zinaumia kwa jinsi nlivyo kuwa nazikandamiza. Hazikupita dk kumi tayari nlikuwa nyumbani, nlishuka kwenye baiskel nkaiegesha kwenye mti wa korosho uliokuwa mbele ya nyumba yetu, nliingia ndani kwa kasi nkiita mama, mama tayari alikuwa shambani ikabidi nimfate huko huko.

nlipoingia shambani, nlimkuta anapariria, nkamuita. aligeuka na kunangalia huku akiniitikia.

" Shkamoo
"maraaba mwanangu umerudi baba.
"Ndio nimerudi, mama kuna kitu nataka tuongee ila ndani.
"um we mtoto mbona unavisa hapa haiwezekani kwani?.
"inawezekana ila naomba twende ndani.
"hhmm sawa.

aliniskiliza akanambia nichukue baadhi ya vitu. tulipoingia ndani alikaa kitandani kisha mimi nkavuta kisturi ili kumkalia kitako.

"Mama!, Naomba unisamehe mamaangu kwanza nimekukosea sana, siku zote nlikuwa nahisi uenda ulimtendea ubaya baba ndo maana hutaki kunambia chochote kuhusu yeye, ila bibi kaniambia kila kitu kilichokukuta na kunambia mengine utanambia wewe, nakuomba mamaangu unambie kila kitu kwani kufanya hivyo mimi ntapata msukumo flan wa kunifanya niwe na hasira za kusoma kwa bidii katika masomo yangu ili siku moja niwe na maisha bora, tafadhali mama.

Nlisema. Sikuweza kumuangalia machoni mama.
macho yake yalishabadilika nlipomtamkia maneno hayo, uso wake ulishakaa kihuruma, nlikumbuka maneno ya wahenga ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni, ukimwangalia unaweza kujikuta unashindwa kumuua na kukuua wewe.
"Mwanangu, bibi yako kakuambia kitu gani.?
aliniuliza kwa mshangao, nami nkamjibu.
"amenambia baba alivyokuoa mwaka 1990, mliishi kwa raha, matatizo yalianza alipopata mali, naskia alikutesa sana ndo maana ukarud nyumbani, hakuitaji kunambia vyote kwa sababu hayo mengine kasema hayajui vizuri, naitaji kujua ukweli wote mamaa! please nambie kila kitu mama angu niwe na amani, hata nkiwa natembea niwe najua ukweli wote nnao.

Mama hakuwa na jinsi, baada ya kusikia bibi ashanambia nusu, aliona haina maana tena akaamua kunisimlia kila kitu kilivyokuwa.

" Ni kweli mwanangu, baba yako anaitwa Masoud, ila namchukia kwa yale aliyonifanyia, na sikufundishi hata siku moja umchukie babaako kama utamwona, kwani waswahili wanasema mpende aliemtendea ubaya mtu muhimu katika maisha yako.
Sikuitaji kukuambia chochote kwa sababu ni story inayoniumiza ndani ya moyo wangu kila nkiikumbuka, na najaribu kuisahau moyoni lakini huwa nashindwa.
Babaako alikuwa ni mtu mzuri sana, alikuja kubadilika ghafla baada ya mimba yangu kuanza kukua, na sitomsameehe mpaka kiama kinasimama kwa alichonifanyia....

Mama alianza kulia, huruma iliniingia lakini nlionesha ukakamavu ili niujue ukweli wote hata nsiotakiwa kuujua nliitaji kuujua.
"nadhani bibi yako amekuambia mpaka tulivyohamia mjini. Alisema.
"Ndio mama
"Ok!! ni kweli tulihamia mjini mara tu baba yako alipoajiriwa kwenye kampuni kubwa na kupatiwa nyumba kubwa ya kuishi, nlifurahi sana nkijua ndo mwisho wa matatizo yangu, nliinua mikono juu na kumshukuru Mungu kwa kuniondolea tabu zilizokuwa zimenizunguka. bila kujua mabaya zaid yanakuja mbele yangu. hapo ndipo nlijua kweli ng'ombe wa maskini hazai na watu kama sisi tumezaliwa kwa ajili ya mikosi.

Tulikaa miezi sita kwa furaha huko mjini, hali yangu ilianza kubadilika kila leo bila kujua tatizo ni nini, kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo baba yako kwangu alinipeleka hospital haraka kupima vipimo vyote ndipo nkakutwa nna mimba ya mwezi mmoja.

Mme wangu alionekana mwenye furaha, tulikumbatiana mbele ya docta alietupatia majibu hayo, lakini nilishangaa kipindi tunarud nyumbani kwenye gari hakuniongelesha chochote na kila nlipomuongelesha hakujibu.

tulipofika nyumbani ilibidi nimuuliza.
"Tatizo nini mme wangu?

Nliongea kwa huruma na sauti ya chini kwani tayari nlishahisi kuna kitu nimemkosea mme wangu na mimi nlikuwa sipendi nimkosee kwa lolote.

Nlipomuuliza hivyo aliniangalia sana kwa jicho la husda mpaka nliogopa, alionekana kuwa mtu alojawa na hasira, aligeuka akanipa mgongo kisha akanambia " SIITAJI KUZAA KWA SASA HIVI.

TUKUTANE SEHEMU YA TANO