Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM
Sehemu ya 21
Walimaliza kuongea wakaongozana mpaka walipokuwa wakina mama pamoja na baadhi ya ndugu, Muda huo huo Gari nyeusi ilikuwa inaingia katika geti la nyumba ya masoud ndani ikiwa imewabeba Seid na Hamad.
Walishangaa sana baada ya kuona kuna watu wengi wengine wakiwa wanalia, walipita mpaka sehemu ya paking kisha wakashuka wakiwa katika mshangao wa kuitaji kujua nini kinaendelea.
Hamad alikuwa anajulikana na masoud kwa kuwa ni mtoto wa mtu mkubwa, Seid alijua fika anakuja kumuona baba yake ambae hajawai muona tokea azaliwe, akiwa na shauku kubwa ya kumuona alivyo mtu aliemtesa mama yake. Wakiwa katika mshangao walitembea mpaka sehemu palipokuwepo kikundi cha watu watano, walimvuta mmoja pembeni ili kumuuliza kinachoendelea...
" Ndugu yangu vipi hali yako ,, Hamad alimuuliza jamaa aliejulikana kwa jina la Faki.
" Hali yangu nzuri sijui kwako.
" Salama salama! ,, sisi bhna ni wageni hapa tumeshangaa kuona tunafika na kukuta watu wengi wengine wanalia kuna nini! ?
" Mtoto wa mheshimiwa kafariki.
" Mtoto wa mheshimiwa kafariki!!? Hamad aliuliza kwa mshangao, huku mioyo ya wote wawili ikianza kwenda mbio. ,, nani ?
" Huyuu mtoto wake wa kike Raya.
Ilikuwa ni kama suprize ya maumivu kwao, walijikaza kiume nguvu ziliwaishia ghafla, walimuaga jamaa waliemuuliza wakasogea pembeni, walilijadili jambo waliloambiwa bila kulipatia jibu, wakaamua kukubaliana na matokeo, wakaenda kujiunga na wengine huku wakiwa na wazo la kukaa ili kupeleleza kujua kiundani zaidi.
Watu walizidi kujaa kila muda ulivyo zidi kwenda mbele, maandalizi ya mazishi yalianza kuandaliwa ili saa kumi wampeleke katika nyumba yake ya milele, kila mmoja bado alikuwa na swali la mbona ghafla namna hii, wengine wakiisi kitu nyuma ya pazia... Baada ya muda flan kupita, magari ya police yaliingia tena eneo la msiba, yalimshusha maiti ikiwa tayari imefanyiwa vipimo vyote, iliingizwa ndani kwa ajili ya kukoshwa na kuagwa na baadhi ya ndugu ambao walikuwa bado hawajaamini, ilipotimia saa kumi kamili waliipeleka makaburi ya mwana kwerekwe kuzika.
" Hamad naomba usisahau kunionesha mzee!! ,, Seid alimshtua rafiki yake kipindi wanaenda kuzika, asije kusahau kumuonesha baba yake, kwani yeye hamjui.
" Oooh God, na nlishasahau kabisa, ngoja tukifika makaburini huko ntamkuonesha kama hakutokuwa na mizengwe ya watu.
" Ila Kweli kifo ni ghafla rafiki yangu, Raya kweli kafariki?
" Nimeambiwa Kajiua ,, Hamad alimjibu shot.
" Acha basi nani kakuambia? ,, Seid aliuliza kwa mshangao.
" Nlipata kuongea na Mke wa baba yako dk tatu tu pale nlipokuacha nkakuambia naenda chooni.
" Yah yah.
" Kanambia kuwa kajiua, sababu kapigwa!, yani tuseme kajiua kwa sababu ya baba yako mwenyewe.
Seid alibaki ameduwaa, alishindwa aongee nini ndani ya sekunde kadhaa.
" Hivi uyu mzee ana akili gani huyu lakini ?
Alijiuliza swali ambalo hakuwa na jibu lake, hamad hakuweza kuongea akawa bize na uendeshaji, msafara wa magari zaid ya kumi uliokuwa unaisindikiza maiti ya Raya uliingia katika makaburi ya m/kwerekwe, kaburi tayari lilishachimbwa, hawakuweza kupoteza muda, waliitoa maiti iliyokuwa ndani ya jeneza kwenye gari, wakaiweka karibu kaburi, zoezi la kufanya mazishi likaanza.
" Huyu ni dada yako inabidi usogee mbele pale ili japo kumwaga mchanga wa mwanzo mwanzo ,, Hamad alimwambia Seid, Seid ilibidi asogee mpaka karibu na kaburi, machozi yalikuwa yanataka kuanza kumtoka, aliliangalia jeneza mara mia mia huku akijiuliza kama ni raya aliomo ndani au laa, mawazo yalimpeleka mbali na kumkumbuka Raya kipindi wanaupanda mlima kilimanjaro, hakuweza kuvumilia machozi yalibubujika kwenye mashavu yake.
" Eh Mungu mpokee vizuri dadaangu, nlichelewa kumjua ila nimemjua, Unasema katika vitabu vyako, tusiwalaani wazazi lakini mimi naomba unisamehe kwa kumlaani baba yangu, kiukweli kwa vitendo alivyovitenda kwa mama yangu pamoja na Raya namlaani kila hatua anayopiga.
Aliwaza Seid akiwa analiangalia jeneza, waliingia watu wanne ndani ya kaburi, shuka liliwekwa juu, watu wakaanza kupepea akiwemo Seid, chini kwa chini maiti ilianza kupitishwa ili kuwekwa mwanandani sehemu ambayo ndo inapowekwa maiti ya kiislam.
Mazishi yalipomalizika watu wote walitawanyika, wengine wakirudi nyumbani kwa Masoud...
" Ama kweli umauti ni ghafla yani huyu binti aliekuwa ameingia chuo ndo aliefariki kweli? ,, alisikika jamaa mmoja akisema.
" Ndo hivo amy, hii ni mifano kwetu sisi, bint wa watu hakuumwa sijui nini kimemkuta maskini, pale mema yake tu ndo yatayomsaidia.
" Kibaya zaid ni kuwa ndo kwanza alikuwa chuo, hata kuyafaidi maisha alikuwa bado.
Ilikuwa Minong'ono ya watu tofauti tofauti, waliokuwa wanatoka kuzika makundi kwa makundi.
Hamad na Seid nao walirudi nyumbani kwa masoud wakiwa na gari lao, Waliposhuka kwa mbali Hamad alimuona masoud, akamshtua Seid huku akimfata masoud kwenda kumsalimia.
alipomfikia walishikana mikono wakasalimiana kisha akampa pole, Seid nae alisogea akampa mkono masoud, masoud bila kujua anaepeana nae mkono ni kijana wake, kisha Seid nae akatoa pole kwa Masoud.
" Aisseeee pole sana Sheikh Masoud pole sana.
" Amina nshapoa.
" Huyu ni rafiki yangu anaitwa Seid niko nae chuo tunapigana tuje kulisaidia taifa, Seid huyu ni sheikh wangu anaitwa Masoud.
" Umesema uko nae chuo e!
" Yah yah.
" Karibu sana kijana, Karibu sana.
Seid aliitikia asante akiwa anawaza juu ya baba yake, alivyomuangalia sura yake na vitendo vyake haviendani, alionekana ana sura ya upole ambayo haioneshi ukatili hata kidogo.
" Mbona sura yake na vitendo vyake ni vitu viwili tofauti?
Alipoteza mawazo hayo juu kwa juu akakumbuka maneno ya wahenga, hakuongea chochote muda wote wa maongezi kati ya masoud ambae ni baba yake na Hamad, alikuwa ni mwenye kusikiliza tu huku akipiga jicho mara moja moja kwa masoud.
" Ila kuna kitu kimoja kimenichanganya kidogo sheikh masoud, , japo ni kazi ya Mungu ila mbona imekuwa ghafla kiasi hicho, ,,, kwa nini nasema hivyo! ? ,, ni jana asubuhi tuliachana nae Raya tukiwa tunatoka kilimanjaro, sasa imetushangaza kidogo hii. ,, hamad aliuliza swali la mtego kuskilizia atajibu nini ikiwa yeye ashazipata fununu za chini chini zote.
" Ni swali gumu sana kwangu kijana kulijibu kwa sababu bado niko kwenye uchungu sasa hivi, ila kiufupi hata mi mwenyewe sielewi, Yah sielewi kabisaa! kwa sababu nlikuwa seblen na mke wangu tunaingia ndani mtu kashafariki, tukapiga cm police waje wafanye kazi yao haraka.....
" Aisee pole sana Shee wangu.
" Asante sana,
Alijibu kisha akaomba awaache kuna kazi anaenda kuzifanya kama baba wa familia, Seid na hamad hawakuwa na muda wa kukaa tena, kuzika tayari walishamaliza, kitu walichokuwa wamekuja kukiangalia tayari washapata jibu lake, waliona hawana la kuwakalisha, waliingia ndani ya gari wakaanza safari ya kurudi makwao.
Waliongea mengi mpaka kufika mjini, seid alishuka na kupanda gari la kurudi shamba jioni hiyo, waliachana huku hamad akimwambia kesho atamfata asubuhi na mapema kwenda chuo.
Hamad alipofika nyumbani akamkuta mzee wake pamoja na mama wakiwa wamekaa sebleni, alisalimia nae akakaa alianza kuwaambia kila kitu kilichotokea, Mzee Shaibu alikuwa anamfahamu vizuri masoud, alipopatiwa taarifa hakuitaji kupoteza muda, alimuomba mkewe ajiandae waende kumpa pole kwa kufiwa.
Mida ya saa moja Seid nae alifika nyumbani, akamkuta mama yake tayari ashalala, aliita, bi najma akatoka kumfungulia mwanae, aliingia ndani akionekana hana furaha hata kidogo, hakuitaji kumwambia chochote mama yake, lakini alilazimika kumwambia kila kitu baada ya kuona anapata maumivu makubwa sana ndani ya moyo wake. Bi Najma hakuamini swala la kufariki kwa Raya, aliuliza mara kumi kumi huku machozi yakiwa yanaanza kumtoka, aliumia zaid alipoambiwa masoud ndo kasababisha kifo chake, alitoa maneno mengi ya laana juu ya masoud, paji lake la uso likiwa limechafuka kwa machozi.
Siku ilipita kwa majonzi ya kufariki raya ghafla, pia ilikuwa siku ya historia kwa baadhi ya watu, akiwemo seid na hamad.msiba uliendelea katika nyumba ya masoud, watu wa karibu pamoja na ndugu walilala kwenye nyumba hiyo, ndugu wote wa upande wa kike walikuwa wanamuangalia masoud kwa jicho tofauti akiwa mbali nao, na akiwa karibu walijaribu kuwa nae sawa ili asije kushtukia chochote.
Asubuhi na mapema Seid na hamad walienda chuo rikizo tayari ilikuwa imeisha, walipofika waliingia moja kwa moja ofisini kupeleka taarifa ya msiba wa mwanafunzi wa chuoni hapo Raya, Walimu walizisambaza taarifa kwa wanafunzi haraka baada ya kuzipata, masomo ya siku hiyo yalibidi yavunjike, Chuo chote kilienda nyumbani kwa Masoud kwa ajili ya kutoa pole pamoja na michango yao ambayo tayari waliichanga.
Walimu pamoja na wanafunzi wote wa chuo baada ya kuwa tayari wamewaona wahusika msibani, walirudi majumbani mwao huku nao wakiwa wanajiuliza kwa nini amefariki ghafla kiasi hicho, masikitiko makubwa ya kumpoteza mwanafunzi aliokuwa na bidii chuoni yalipita kwa baadhi ya walimu, Siku nayo ikapita watu wakiwa wako kwenye majonzi makubwa.
Siku ya tatu ambayo ndo ilikuwa siku ya mwisho kukaa msibani iliingia, Mama mzazi wa Yulaina na Sauda pamoja na ndugu wote wa upande wa yulaina ( mabibi, mashangazi, mamama wa raya) walikaa sehemu ya pamoja kwa ajili ya kulijadili jambo ambalo liko mbele yao.
" nimewaiteni hapa, kulijadili jambo tulilokuwa tumepanga muda mrefu, nadhani muda ndo huu umewadia, aliekuwa kizuizi ni mtoto lakini nae ashaondoka. ,, Mama Yulaina au mama sauda/lubna alisema kuwaambia kundi la watu zaid ya 20 aliokuwa amekaa nao.
" Mimi kwanza nataka kujua, miaka miwili aliokaa na wewe lubna hajajua kama una udugu na Yulaina? ,, aliuliza moja ya ndugu.
" Yah, nlijaribu kufanya juu chini ili asijue, kwani nayakumbuka sana maneno ya dada, ila naumia kumpoteza raya, Dadaangu alinambia nimlinde ntamwambia nini mimi kama Raya amefariki, atanielewaje Dadaangu mimii jamanii ,, Aliongea Sauda akiwa analia.
" Usijali mwanangu, Dadaako yuko radhi nawe, wala usijali kuhusu hilo kwa sababu umeyafanya yote haya, ukakubali kumsaliti hadi mwenzako sababu yake. ,, alisema mama yake.
" Hapa kilichopo mdogo wangu, hii kazi bado tunakuachia wewe uimalize, mimi ntakuelekeza kwa babu yangu flan hivi aliewahi kunisaidia, huyo babu anatumia uganga wa kitabu, akimtengeneza mtu anatengenezeka kisawa sawa, sawa mdogo wangu! , ,, Dada mkubwa alizungumza ambae ndo alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia hiyo akafata Yulaina.
" Ok dada nimekuelewa.
" au nyie mnasemaje? ,, aliuliza tena dada mkubwa.
" Hapa hakuna cha mnasemaje? ,, kama alivyoona raha kufupisha maisha ya mtoto wetu, akafupisha na ya mjukuu wangu pia, ndivyo anatakiwa afurahi akiwa na maumivu.
Waliongea mengi ndani ya kikao chao bila mtu yoyote wa nje kujua, Sauda bado alikuwa ni mtu wa kulia kila wakati kwa kumpoteza Raya, upo muda Masoud alimuuliza kitu gani kinapelekea alie kila muda, wakati mtoto si wake, Sauda hakumjibu chochote zaid ya shot kati " siitaji uniulize maswali ya kipumbavu wakati mtoto nimeishi nae miaka miwili.
Harakati tofauti za hapa na pale ziliendelea ikiwa ni siku ya mwisho ya maombolezi, Usiku uliingia watu wakapumzika, Sauda bado ilikuwa ngumu sana kupata usingizi, hasa kumbu kumbu za dada yake zikimuingia kichwani.
" Hivi mke wangu hii hali itaendelea mpaka lini? eti! ,, Masoud alimuuliza Sauda wakiwa kitandani ,, yani we kila muda kulia kila muda kulia mpaka lini mamaa!!!
Sauda hakujibu chochote, aligeuka upande wa pili machozi yakiwa yanamtoka, masoud alimwangalia mkewe kisha nae akageuka upande wa pili kulala ,, Ok Sawa! ,, kama umeamua hivyo kulia kila muda sawa!......
Usiku wa saa Tisa sauda akiwa amelala, Mwanga mkubwa ulitokea pembeni na alipokuwa amelala sauda, Mzimu wa Yulaina ukaja ghafla na kukaa pembeni yake, Usingizi tayari ulishampitia na kuwa mbali kindoto, Yulaina alimuangalia mdogo wake akaachia tabasam, akauweka mkono wake kwenye macho ya sauda, Sauda akawa amefumbua macho. alishtuka sana kumuona dada yake, alimuangalia bila kummaliza machozi yakiwa yanamlenga.
" Sistaa! ,, alimuita kimshangao kwa sauti ya chini.
" Yes! its me Lubna! ,, Yulaina aliongea kumjibu sauda macho nae yakiwa yanalengwa lengwa na machozi ,, Nimekuja kukupongeza mdogo wangu kwa kazi nzuri uliyoifanya, umeonesha kiasi gani unanithamini sana dada yako, nlikuambia tu siwezi kuishi tena na aliesababisha ni Masoud, nkakuitaji uolewe nae ili kulipiza kisasi ukakubali bila kuelewa hata kwa nini nlikuambia hivyo. Ndugu zangu wote wanajua tu masoud ndo aliesababisha kifo changu, ila hawajui kitu gani kilipelekea mimi kufariki, naomba kuanzia leo usilie kwa sababu ya kufariki kwa mwanangu raya, mimi niko radhi nawe, nna dk kumi tu za kukuambia kitu gani kilipelekea mimi kupatwa presha na kufariki.
Lubna,, Angalia ukutani pale tafadhali,,
Sauda aliangalia ukutani akaona kitu kilichojengeka kama luninga, akafanikiwa kuona siku ya kwanza dadaake alipoingia kwenye ndoa, Furaha ilivyokuwa imetanda ikiwa imeambatana na vicheko visivyoisha, na namna masoud alivyomtimua mke wake wa kwanza kisa Yulaina.
******
Miaka 21 Nyuma.......
" Mke wangu karibu sana, kuanzia leo hapa ni kwako, asanteni sana ndugu zangu kuniunga mkono kwa kumuoa Yulaina hapa! na kumuacha yule mluga luga. ,,, yalikuwa ni maneno ya masoud akiyasema mbele ya ndugu zake,,
" Yani kaka, huyu ndo umetuletea wifi sasa, maana yule! aaaagh kwanza hata kuongea hajui, anajifanya mstarabu sana, bora umemuacha bhna. ,, alisema mdogo wa masoud.
waliongea mengi siku hiyo mida ya saa moja usiku baada ya kumfukuza Najma, ndugu wa masoud kwa kuwa ulishaingia usiku ilibidi walale, asubuhi na mapema waliamka, wakaaga na kuondoka zao, Masoud alifungua ukurasa mpya wa maisha akiwa na mke wake mpya, waliishi kwa furaha na amani ndani ya nyumba, baada ya miezi kadhaa kupita Yulaina alijifungua mtoto wa kike ambae walimpatia jina la Raya, kikiwa kama kiunganishi kizuri cha ndoa yao, Ilipopita miaka kumi mbele wakiwa na maisha mazuri ya kitajiri, furaha, vicheko, na kuweka vitendawili kwa watu kutokana na mapenzi mazito waliokuwa wakioneshana, Matatizo yakaanza baada ya kuhamia mwanamke mzuri aitwae Samira katika kampuni aliyokuwa akifanya kazi masoud, na kupangwa kwenye ofisi moja.
Masoud alitokea kumtamani Samira, walipeana namba za cm wakaanzisha mawasiliano ya mara kwa mara, hazikupita wiki tatu, wakaingia kwenye mapenzi, Samira alikuwa ana kwake alikokuwa akiishi peke yake, Masoud alianza kubadilika hasa alipokaribishwa kwa samira na kupewa vionjo onjo ambavyo pengine alikuwa akivipata toka kwa yulaina ila kwa kuwa vilikuwa vinatolewa kwa mwengine akaviona vipya.
" Mme wangu, Mbona naona siku mbili tatu hizi hauko sawa kwa nini ?
Ni swali ambalo yulaina alimuuliza masoud baada ya kuona haelewi ratiba zake siku za karibuni.
" Kazi tu zimebana sana mke wangu.
" ndo siku nyingine kulala huko huko au na mimi muda wangu umeisha ,, Yulaina aliuliza katika hali ya huzuni.
" Hapana mke wangu naomba usiseme hivyo, basi nisamehe sirudii tena.
Alimsamehe bila kujali chochote kwa sababu alikuwa anampenda, siku zilivyozidi kwenda mbele ndivyo jamaa alivyozidi kubadilika, ilifika muda yulaina akawa anaitaji kupata tendo la ndoa halipati kwa muda masoud akidai amechoka,
Yu alishindwa kuvumilia tabia hiyo ya mmewe kubadilika kila siku, ikabidi aanze kufatilia nyendo zake ili ajue kwa nini mmewe amebadilika kiasi hicho......
Tukutane Sehemu ya 22