Riwaya: MSAMAHA WA MAMA
Mwandishi: SEID BIN SALIM
SEHEMU YA 10
Mhalifu alikalishwa kwenye kiti na kutolewa kitambaa chake cha usoni, Kila mmoja alitoa macho na kukaa katika hali ya siamini, kuwa sura anayoiyona mbele yake ndio sura iliyofanya unyama wa kumpiga ticha risasi, na kuwaangaisha watu kiasi chote hicho cha kuwaangaisha.
Songa nayo......
Maneno tofauti tofauti yalisikika yakisemwa baada ya kumuona mhalifu sura yake, wengine walikuwa bado hawaamini kama anaeonekana mbele yao ndo mhalifu mwenyewe, Kamanda mkuu wa kituo hicho cha malindi alisogea pembeni yake kwa ajili ya kumuoji huku watu wote waliokuwa wamekizunguka kituo wakiwa wametoa macho yote..
" Mr Richard!, Kamanda alimuita mtuhumiwa jina lake, halikuwa geni kwa wengi hasa watu wanaofanya kazi katika vyombo vya dola.
" Kitu gani umekosa katika jeshi la police mpaka ukaamua kufanya unyama ulioufanya!?, Jeshi lilikuwa linakutegemea wewe mr richard, kumbe we ndo adui wa Serikali?. Alimuuliza.
Alikuwa analitumikia jeshi la police na alikuwa moja ya mapolice waliokuwa wakitegemewa katika uhodari wa utendaji kazi, kila mmoja alikuwa haamini kama mr huyo ndo ameangukiwaa na aibu hiyo ya mwaka, yeye mwenyewe akiwa ameinamia chini.
Waandishi wa habari kwa mara nyingine walifika katika kituo cha police kumuangalia mtu huyo, nao hawakuamini baada ya kufika na kuingia ndani wakiuliza
"Mtuhumiwa yuko wapi?
Na kuambiwa mr richard ndo mtuhumiwa mwenyewe. walianza kuchukua picha na video fupi fupi kama kawaida yao, walimuangalia mr bila kummaliza, hawakuitaji kupoteza muda kamanda mkuu alimuuliza tena.
"Nani amekutuma!?
Mr richard hakujibu chochote, maiki za kituo cha tv ya Z B C tayari zilikuwa ziko mbele ya mtuhumiwa, mwandishi mmoja alimsogelea na kuuliza
"Mr Richard we ni moja ya mapolice muhimu sana Zanzibar, na nakumbuka siku moja niliwahi kukuoji mimi mwenyewe ukakemea vikali unyanyasaji wa kijinsia na kusema unawachukia sana watu wanaotoa siri za serikali na kusaliti jeshi la police, vipi umekuwa wewe leo au unahisi jamii ilipokeeje jambo hili!?
Mr Richard hakuweza kuuinua mdomo wake kuongea chochote, alionekana kuwa kimya, machozi taratibu yalianza kumtoka, kosa alilolifanya lilikuwa ni aibu kubwa hasa kwa maaskari mbele ya wananchi. Walimuomba aseme aliemtuma, huku minong'ono ya wengine wakisema uenda ameshawishiwa vikubwa kwa kupewa pesa nyingi ndio maana akafanya kitendo kama hicho, askari mkubwa kama huyo inaitaji moyo kufanya tukio alilolifanya.
Hamad alitoka nje akitikisa kichwa, Cm yake iliyokuwa mfukoni ilianza kuita, aliitoa haraka na kuangalia jina akakuta ni my patna akajua ni seid.
" My Friend. Aliita kwa mbwe mbwe.
" Nishafika mjini hapa Ticha kalazwa mnazi mmoja sio? Aliuliza seid.
" Ndugu yangu kabla hujafika huko njoo hapa kituo cha malindi uione aibu ya mwaka.
" Aibu ya mwaka!? mbona unanishtua.
" Nakuomba uje ujionee na uamini, kila siku nikikuambia Serikali yetu ya Tanzania hamna kitu huwa unanitania kwa kusema mi sio mtanzania njoo sasa ujionee.
" niko maeneo haya ya sheri nakuja sasa hivi. alisema akakata cm.
Seid hakuwa mbali sana na maeneo ya kituo kutokana na stend ya magari yatokayo shamba kuwa maeneo hayo hayo, alitembea haraka haraka kwenda alikoambiwa, Hamad hakuingia ndani akimsubiri swahiba yake. Hazikupita dakika tano tayari alikuwa ashafika kituoni na kufanikiwa kumuona rafiki yake bila kutafuta kutokana na uwazi uliokuwepo.
Wlikumbatiana na kusalimiana.
" Vipi kuhusu Ticha?. ndio lilikuwa swali la kwanza la seid kwa hamad.
" Nimemuuliza Fatha amenambia risasi imetolewa na anaendelea vizuri, naomba twende ndani ukayaone ya musa na yanayonifanya mimi nipingane na Serikali yetu kila siku.
Walitembea mpaka ndani, Walipofika Seid alishangaa sana kumuona mr richard akiwa amekalishwa kwenye kiti na pingu mikononi, Hamad maneno yalimtoka mbele ya mkusanyiko wa watu.
" Haya mimi ndio yananifanya niichukie Serikali ya Tanzania kila kukicha, jionee mwenyewe Seid Jionee, Unadhani sisi wanafunzi tunaoitaji kuingia chuo mtu kama huyu anatufundisha nini zaid ya kutufundisha tusome tuje kuwa majambazi wakubwa, huu ni upumbavu na ujinga wa watu waliokalia viti vinene kuwakandamiza wanyonge, Cha ajabu kesho na kesho kutwa utasikia yuko mitaani anadunda baada ya kusugua Jela..
Watu wote waligeuka kumuangalia Hamad, bado seid alikuwa katika hali ya kupigwa na bumbu wazi kwa anachokiona, kauli ya hamad iliwashtua wengi, wengine walipiga makofi kwa kijana kuongea maneno mazuri bila woga. Seid alimvuta rafiki yake nje tena baada ya kuona baadhi ya watu wanaweza kumchukulia vibaya.
Zaid ya watu 30 na waliokuwa eneo hilo mbali na maskari, walimuomba mr richard aseme ukweli kuhusu tuhuma iliyoko mbele yake, japo itaendelea kuwa aibu lakini kidogo itapungua kwa upande wake .
" Kitu gani kimemkuta Mr Richard?, au sie huyu ambaye tulikuwa tunamuangalia juzi alipokuwa akihojiwa Z B C!?. Seid alimuuliza hamad baada ya kutoka nje kidogo.
" Yeye ndo amempiga risasi ticha.
" Are you serious?
" Hata mimi sikuamini kama wewe kutokana na maneno yake mazuri anayoongea pindi anapohojiwa ila imebidi niamini.
Kipindi wanaendelea kuongea walishangaa kuona mr richard wanamtoa ndani akiwa amefungwa pingu na kumuingiza kwenye gari ya police.
Watu wote waliokuwa ndani ya kituo nao walitoka vichwa vikiwa chini, baba yake alipofika karibu nae alimuuliza.
" Fatha vipi?
" Imepigwa cm na wakubwa wakaitaji mr richard apelekwe dar kwa sababu yeye sio mzanzibar, na serikali ya bara ndio itatoa hukumu juu yake.
Aliachia kicheko hamad.
" Nlijua mambo kama haya yatatokea tu, kwa upuuzi huu baba yangu nakuomba nitakapomaliza kusoma usije kuwa na mawazo ya mimi kuwa miongoni mwa watu wakubwa serikalini, bora nikafanye kazi nje ya nchi nionekane sio mzalendo lakini sio hapa kuendekeza huu upuuzi ujinga mkubwa. Kesi ishaisha hiyo, akifika dar itapigwa cm tu mtu kauawa au kafungwa kumbe yuko mtaani, kuna mkono wa mtu mkubwa umezunguka hapa. Alisema Hamad
"Mwanangu usiwe na imani hizo nakuomba. Alisema mzee shaibu.
kila mmoja aliekuwa ndani ya kituo alitoka akiwa anasema lake, wengi walitegemea mr richard kusema japo aliemtuma lakini haikuwezekana,watu walitoka eneo hilo na kwendelea na kazi zao kila mtu akilaani juu ya utendaji mbovu wa viongozi serikalini.
" Baba huyu anaitwa Seid hukuwai kupata bahati ya kumuona, Nasoma nae na nategemea kuingia nae chuo kwa sababu tuko level moja, Ila anaitaji msaada mkubwa sana rafiki yangu kutoka kwako wewe baba. Hamad aliachana na mada za mr richard akaingiza nyingine.
" Msaada gani?. Aliuliza mzee shaibu.
" Matokeo yake yameuzwa.
" Yameuzwa?.
" Yah, ni kama Mungu tu Ticha alimpigia cm kabla ya matokeo yake kutoka na kumwambia kuwa amepata matokeo ya juu kuliko mwanafunzi yoyote, ila yalipowekwa ubaoni, kaonekana hata nukta za chet cha form six hana, tukajua moja kwa moja yameuzwa kwa sababu hali yake ni duni kidogo na anasoma kwa bidii ili kitabu siku moja kije kumuokoa.
"Basi!. Mzee shaibu alisema aliposikiliza maelezo ya mwanae. picha nzima aliona kama inamjia machoni mwake ya Ticha kupigwa risasi na Richad, akasema basi akitikisa kichwa.
" Basi nini Fatha..
" Nishaelewa kila kitu, hii ishu itakuwa inahusiana kwa karibu sana na Ticha kupigwa risasi.
" Kwa nini mzee wangu.
" Naomba upaki gari lako sehemu nzuri, mpande gari langu Tufike wizara ya Elimu, Kijana pole sana kwa kuchukuliwa matokeo yako nakuahidi yatapatikana kwa kuwa hilo jambo limefika kwangu.
" Asante Sana baba.
" Umesema nipaki gari kwa nini wewe usiwe kwenye gari lako kisha sisi wawili tukaja na hili langu.? Aliuliza Hamad.
" Hakijaharibika kitu ili mladi tufike tu, kijana namba yako ya chuo unayo vizuri na detail zako zote?. Mzee shaibu alimgeukia Seid akamuuliza kuhusu detail zote za matokeo.
" Ndiyo ninazo.
" Basi usijali mimi ndio professa, sio jambo la kuumiza kichwa, ingieni kwenye gari, mkitangulia nyie sawa au mimi ili mradi tukutane wizara ya Elim. Alisema mzee shaibu.
Wakiwa hawajaingia hata kwenye magari Cm ya mzee shaibu iliita, kabla ya kupokea aliwambia "Ingieni kwenye gari tu mwende mimi nakuja.
Seid na hamad walitembea mpaka kwenye gari, mzee shaibu alipokea cm iliyokuwa inatoka kwa mke wake akimuulizia kinachoendelea, alimueleza kila kitu huku nae akitembea taratibu kuingia katika gari lake leusi.
Baada ya kupita nusu saa, Mzee shaibu tayari alikuwa katika ofisi za wizara ya elimu, viongozi wazito wazito waliokuwa ndani ya ofisi hizo walishangaa sana kuona magari ya mzee anae heshimika sana serikali yanatia timu katika ofisi zao.
Maprofesa waliokuwa wamevalia suti nyeusi walitoka nje kwa ajili ya kusalimiana na Mzee huyo pia kumkaribisha ndani.
Gari lililokuwa limewabeba Seid na Hamad lilikuwa pembeni ya magari matano ya msafara wa Mzee shaibu, hawakushuka kwanza mpaka pale watapoambiwa washuke kama walivyokuwa wamepanga, vioo vyeusi vilivyokuwa kwenye gari lao viliwafanya wasionekane na mtu yoyote. Maprofesa kadhaa walimchukua mzee na kuingia nae ndani wakipiga nae story mbili tatu kuhusu hali za familia, nyuso zao zilionekana kufurahi muda wote mpaka walipofika moja ya ofisi za watu wakubwa waliojaa Elimu ndani ya mjengo huo na kumuacha hapo.
Hakuwa na muda wa kupoteza mzee shaibu,
Alienda moja kwa moja hadi kwenye ofisi ya mkuu wa kitengo cha usimamiaji wa mitihani ya Form Six na matokeo kiujumla. Kwa kuwa alikuwa anazijua vizuri ofisi zote zilizomo ndani ya jengo hilo la wizara ya elimu hakuitaji kuelekezwa, aliwahi kufanya kazi humo humo akiwa kama mkuu wa usimamiaji mitihani ya chuo kikuu kabla ya kustaafu na kuamua kuwa mzee wa serikali.
Alifungua mlango na kuingia ndani sura yake ikawa uso kwa uso na sura ya profesa aliejulikana kwa jina la sharif, sharif alipomuona mzee shaibu alitabasam, akamsalimia wakajuliana hali huku mzee shaibu akikaa kwenye kiti kilichokuwa mbele ya meza kubwa.
Baada ya kusalimiana walianza kupiga story za hapa na pale, mwisho mzee shaibu alimuuliza kuhusu mitihani ya form six, wanafunzi waliopanda na kushuka pamoja na hali za kimatokeo.
Sharif alionekana kushtuka baada ya kuulizwa maswala ya matokeo, alijaribu kujibu mkato mkato kumpoteza mzee shaibu juu ya upandaji wa wanafunzi na kushuka katika matokeo ya pamoja na shule zilizofanya vizuri, mzee shaibu hakuonekana kurizika kwa majibu yake ikabidi amuombe Computer ambayo ina machapisho yote ya mitihani ili kuangalia kila kitu kwani nae alikuwa zaid ya Profesa kwenye hizo ofisi na anayajua maswala yote ya usimamiaji mitihani hasa katika idara ya kucheza na akili kwenye matokeo.
"Maalim Shaibu. Sharif alimuita mzee shaibu akiwa anazunguka katika kiti na kupapasa kitambi chake. " Mtoto wako kapita sheikh wangu, vipi unaitaji maswala kama haya tena wakati mtoto wako kafaulu?, mwanao kapata nukta za juu bhana, ebu tuongelee mengine hayo tuachane nayo. Alisema.
"Kufaulu kwa kijana wangu sio tatizo naitaji niangalie zaid nukta zake maana nyie hamchelewi wataalam wa mambo haya. Alisema kimasihara kuangalia sharif atajibu nini.
"Hapana bhana maalim achana nayo, hayo mambo yetu sisi.
Mzee shaibu alizidi kupata sura nyingine baada ya kukataliwa kupewa computer yenye ifadhi zote za mitihani ya form six, Alibadilika ghafla akawa mkali na kumuomba profesa sharif atoe compute la sivyo watafika mbali katika vyombo vya dola, Ila bado profesa aliona kama masihara na kusimamia msimamo wake wa kuwa hawezi kufanya hivyo huku akihoji kwa nini anaitaji kompyuta yenye siri za mitihani ya wanafunzi.
mzee shaibu tayari alikuwa acheki tena, aligonga meza kwa nguvu na kumuitaji profesa atoe computer.
"Nlikuwa nakueshimu sana ila kwa hiki kitu ninachokihisi kama kimefanyika kweli, Nakuapia mbele ya Mungu umeangamia, maisha yako yanaingia hatarini wakati wowote, usilete utani na vyombo vya dola wakati we ni msomi unaitwa profesa, nimekuja hapa nacheka lakini sasa hivi naomba unione kama chui yuko mbele yako. Alisema mzee shaibu.
Sharif alijaribu kuonesha ukakamavu licha ya kuambiwa maneno mazito lakini mzee shaibu aliendelea kumuhisi kushiriki juu ya uuzaji wa matokeo ya seid.
" Mzee wangu kiukweli naona sikuelewi, umeingia kwa upole sasa hivi naona umekuwa mshari ghafla kwa nini?
" Huelewi?
" Yeah, I don't understand you mzee shaibu, just be serious for what talking. ( Ndio, sikuelewi mzee shaibu, jaribu kuniweka sawa kwa kile unachokiongea ).
" Ooh, kweli viongozi sisi sisi ndio tunaozuia maendeleo ya nchi kwa kutaka masilahi yetu binafsi. Ok labda nisikuzungushe, Naitaji mitihani ya wanafunzi wote wa form six wanaosoma Green secondary school. Alisema mzee shaibu.
Sharif alishtuka akawaza kitu moyoni mwake. ** Green school kuna mwanafunzi tumeuza matokeo pale, ndio anachotaka nini? ** alisema na nafsi yake.
" Mzee wangu hiyo mitihani sina hapa ofisini. Alisema mara alipomaliza kuwaza.
" Iko wapi?
" Nadhani itakuwa kwenye ofisi ya kumbu kumbu za mapeipa.
" Wao, unadhani itakuwa katika ofisi ya kumbu kumbu za mapeipa. Alirudia maneno yake.
" Yeah.
" Ok Nashkuru kwa jibu lako. Mzee shaibu alijibu hivyo na kuinuka kwenye kiti akasimama na kumwambia.
" Nadhani hunijui vizuri profesa sharif, Mimi ni zaid ya profesa na ndio maana unaona hata serikali nzima ya Zanzibar inanieshimu, Rais anapoitaji ushauri lazima aje kwangu mimi, hakufanyiki kikao chochote ikulu lazima mimi niwepo, kama unajitia usomi wakati mimi nimesoma mpaka ubao ukabomoka, Utakuja kuniona mbaya mr Ila! nakupa ovyo tu, Ndani ya masaa manne mbele, Naitaji ukweli uanikwe juu ya kuuza matokeo ya kijana masikini anaetegemea kitabu kuja kumuokoa maishani mwake sihitaji upumbavu, haiwezekani kijana wa watu afaulu kisha hata matokeo ya cheti asipate ujinga huo hauwezi kuendekezwa katika idara ya Elimu, laa sivyo ripot nazipeleka kwa waziri wako.
Baada ya kuongea hayo alitembea mpaka karibu na mlango kwa ajili ya kutoka nje. Kabla ya kufungua aliitwa na sharif, sharif tumbo tayari lilikuwa joto, kiti alichokalia aliona kama kinamuumiza kijasho chembamba kilianza kumtoka baada ya kusikia habari za kupeleka taarifa ya kuuzwa matokeo ya form six kwa waziri wa Elimu.
" Naomba urudi mzee wangu ukae kwenye kiti. Alisema sharif. Mzee shaibu alimuangalia.
"Nadhani huna cha kuniambia nikakuelewa wakati ushasema mapeipa hayapo. Alisema.
" Naomba uje ukae mzee wangu. Alisema kwa mara ya pili mzee shaibu akarudi akakaa kwenye kiti.
" Niko tayari kukuambia ukweli wote ila naomba iwe siri yangu mimi na wewe na nakuahidi matokeo yatarudishwa kama ilivyotakiwa, kwa sababu ni kweli matokeo yameuzwa na yameuzwa kwa mtoto wa Tajiri maarufu tu hapa Zanzibar baada ya kutoa kitita cha pesa za kutosha ili mwanae apite.
Profesa Sharif aliongea jasho tayari likiwa linamwagika usoni mwake, alikuwa amevaa miwani midogo ya duwara ilibidi aivue baada ya kuona kama haoni, Upara wake ulianza kuloana loana jasho japo A/C ilikuwa inapuliza.
Tukutane Sehemu Ya 11 Hapa hapa. Waalike Marafiki Pia.