1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine: Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza unavyotakiwa kuishi na mwenza wako. Hivyo basi, chukua muda wa kutosha kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na makala mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya mahusiano, zitafakari vema ili kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.
2. Upekee wa mambo: Tambua kuwa tabia ya mpenzi wako inaweza kuwa ni ya kipekee, mazingira pia ya tukio linalokufanya utake ushauri au maoni kwa wengine yanaweza kuwa ni ya kipekee, hivyo ushauri au maoni utakayopokea yanaweza yasikusaidie moja kwa moja katika suluhisho lako. Ukitambua hili, utafanya bidii ya kujenga uwezo binafsi wa kuchambua tatizo unalokumbana nalo katika mahusiano na kutafuta suluhisho kabla ya kutegemea watu wengine.
3. Mwenye maamuzi ni wewe: Ni kweli kuwa kuna nyakati ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa watu wengine, na zaidi sana watu wenye uelewa sahihi na unaowaamini, hakikisha kuwa unatambua kuwa wewe mwenyewe ndio mwenye kubeba lawama ya maamuzi utakayochukua.
4. Kuwa na subira: Usichukue maamuziya haraka katika mahusiano hususani uamuzi wa kuamua kuwashirikisha watu wengine habari ya mambo yahusuyo uhusiano wako. Unapofanya uamuzi wa kuwashirikisha wengine kwa haraka unajinyima nafasi ya kulichunguza jambo kwa ufasaha hususani madhara yanayoweza kutokea kwa kuwaeleza wengine, au kama ni tatizo, basi kufikiria njia sahihi ambazo ungeweza kuzitumia kupata suluhu ya tatizo.
5. Fungua njia za mawasiliano kati yenu: Pengine chanzo cha wewe kutaka kuzungumza mambo ya ndani yanayohusu mahusiano yenu kwa watu wengine ni kwakuwa umekosa nafasi ya kuzungumza kwa ufasaha na mwenzi wako. Tafuteni nafasi za kutosha, jengeni mazingira ya kuzungumzia mambo yenu kabla ya kutaka kuwashirikisha watu wengine.
6. Kuweni peke yenu:
Hata kama hautaki kueleza watu kuhusu mambo yanayoendana na maisha yenu, mazingira unamoishi yanaweza kuchangia watu kutaka kuingilia mahusiano yenu –kwa kutoa maelekezo, ushauri au maoni kuhusu muishivyo wewe na mpenzi wako. Inapobidi hakikisha hamuishi karibu na wazazi wenu, ndugu au rafiki wa karibu. Au haufanyi kazi na mwenzi wako sehemu moja, kwani hiyo itakuwa njia rahisi sana ya watu kuona mnavyoishi. Inapobidi kuwa karibu na watu wengine , hakikisha mnakubaliana wewe na mwenza wako namna bora ya kuendesha mawasiliano kati yenu mbele za watu, ili msiwape nafasi ya wao kumi‘soma’ na kisha kuanza waje waanze kutoa ‘maelekezo’ ya vile wanavyoona mnapaswa kuishi.
7. Nenda ‘darasani’ : Kumbuka mahusiano yanahitaji sana uelewa mkubwa wa jinsi ya kufanya mawasiliano fasaha, kuelewa hisia za mwenzi wako, kutambua mbinu za kusuluhisha migogoro, na zaidi sana kufanya mipango ya muda mrefu ya uhusiano wenu. Jizoeshe kusoma makala na vitabu mbalimbali vyenye kuboresha ufahamu wa mambo ya msingi kama hayo tuliyoeleza hapo juu. Mfano wa makala unazoweza kusoma ni kama vile: MADHAIFU MATANO KATIKA MAPENZI
Share:
Categories Mahusiano
Email This
BlogThis!
Share to Twitter
Share to Facebook
RELATED POSTS:
KANUNI 3 ZA MSINGI ZA MAWASILIANO SAHIHI NDANI YA FACEBOOK NA WHATSAPP
FANYA HIVI KUEPUKA INGIA KATIKA NDOA AU MAHUSIANO MACHUNGU
ZIFAHAMU ATHARI HIZI ZA WHATSAPP, FACEBOOK, INSTAGRAM KATIKA MAHUSIANO
FANYA HIVI KAMA UNATAKA UFADHILI WA MASOMO AU MTAJI WA BIASHARA
UFANYE NINI KUTIMIZA NDOTO YA KUISHI MAISHA YA KIMATAIFA ?
Newer Post Older Post Home
0 COMMENTS:
POST A COMMENT
Search for:
Search...
Contact Us
Name
Email *
Message *
Follow by Email
Email address...
Popular Posts
KANUNI RAHISI ZA KUJIFUNZA KIINGEREZA: SOMO LA 1
SEHEMU YA KWANZA Msingi mkuu wa kufahamu lugha ni kujua jinsi sentensi zinavyoundwa kwakuwa sentensi ndio haswa tunazotumia katika maz...
MBINU ZA KUJIFUNZA ENGLISH KWA URAHISI NA HARAKA -1
Kwa uzoefu wangu wa kujifunza na kuweza kutumia lugha nne tofauti yaani Spanish, English, Zulu na Xhosa nimejifunza kuwa kuna mambo amba...
FANYA HIVI KAMA UNATAKA UFADHILI WA MASOMO AU MTAJI WA BIASHARA
Kama wewe ni mmoja wa wanaotafuta ufadhili wa masomo au msaada wa kifedha ili ujiendeleze kielimu au kibiashara , basi makala hii inakuh...
UNATAKA BUSINESS PLAN TEMPLATE AU SAMPLE? CHEKI HIZI
Kama unataka kuandika business plan (Mchanganuo wa biashara) na unahitaji kuona sample (muundo wa jinsi inavyoandikwa) basi makala hii f...
JIFUNZE ENGLISH:MAMBO 6 YA KUFANYA ILI KUJIFUNZA ENGLISH KAMA HUJUI KABISA
Badala ya kuita kichwa cha habari jinsi ya kujifunza English kama hujui tungeweza pia kusema jinsi ya kujifunza lugha yoyote ya kigeni k...