TAFUTA HAPA
AINA NNE ZA WANAUME WASIOFAA KATIKA NDOA
KATIKA MAKALA YALIOPITA TULIZUNGUMZIA MASWALA YA WANAWAKE WANAO SABABISHA MAISHA MAGUMU NDANI YA NDOA ZAO... leo nakuja na makala hii nyingine iitwayo
AINA NANE ZA WANAUME WASIOFAA KATIKA NDOA
1.ASIEPENDA KUFANYA KAZI, AKISUBIRI ALISHWE NA MKE.
Huyu ni hatari kwa sababu hatokuwa na ujasiri wa kumkemea mke pale anapokosea kwa kukhofia mke asije kasirika na kusitisha huduma ya kuilisha familia.
2. ONJAONJA
Huyu ni mwanamume anaependa kuoa na kuacha bila ya sababu,huyu ni hatari kwa sababu anazichezea sheria za Allah na kuwadhalilisha wanawake,talaka inakubalika ktk Uislamu lakini imewekwa ktk nafasi ya mwisho ikiwa hatua zote muhimu zimeshindikana.Kuoa na kuacha bila ya sababu za msingi hakukubaliki ktk Uislamu.
3.ALMANNAAN.
Huyu ni mwanamume anaemnunulia mkewe vitu vya aina mbalimbali kisha anaanza kujitangaza nje.
Huyu ni mtu hatari kwa sababu kitendo cha kumpa mtu kitu kisha ukaanza kujitangaza kinaharibu malipo na kinathibitisha kwamba lengo lake lilikuwa si kupata radhi za Allah bali ni kutafuta sifa kwa watu.
4.ASIE NA WIVU
Huyu ni mwanamume alieridhia mkewe achezewe na wanamume wengine au Mkewe aoneshe mapambo yake kwa wanamume wengine.
Na hili tunalishuhudia katika jamii utakuta mwanamume anamruhusu mke atoke ndani ya nyumba akiwa amevaa mavazi yasiyostiri mwili hatimae anawapa mtihani wale wanamume barabarani.Asiekuwa na wivu haingii peponi.
5. MWENYE MANENO MACHAFU
Huyu ni Mwanamume ambae anapokorofishana na mkewe hukimbilia kutoa maneno machafu kama vile kumwita mke "Mbwa"Ngedere"nk.
6.MJINGA
Huyu ni Mwanamume asietaka kujifunza mambo ya dini yake,na kwa ajili hii utakuta hamudu kuilea familia ktk maadili anayoyaridhia Allah mtukufu.
7.ALMUSRIFU.
Huyu ni mwanamume mwenye kutumia pesa yake na vitu vingine kwa fujo khaswa pale anapopokea mshahara wake.
Israafu ktk matumizi ni haramu.
8.MSHIRIKINA
Huyu ni mwanamume ambae alieiweka mbele shirki ktk mambo yake hata mtoto wake akiumwa MALARIA atampeleka kwa mganga wa kienyeji.