TAFUTA HAPA

DUDU WASHA 40

DUDU WASHA-40
.
Ilikuwa ni aibu kwa Secilia pia Didi ambao walipewa muda wa kuwatosha kujiweka sawa ambapo walioga vyema na kuvaa mavazi mengine kisha wakaketi sebuleni kwa ajili ya kuzungumza na Junior,hofu kubwa ya Secilia ni kwamba Martin akijua suala hilo itakuwa aibu kubwa sana na ndoa yake inaweza kuvunjika
,,,kwahiyo shemeji nakusikiliza,japo kidogo tu nikuonje na mimi,,,aliongea hivyo Junior ambapo alimkera kweli Secilia aliyekuwa hana namna ya kufanya
,,,nakuomba kaka umsamehe tu,tufanyie ubinadamu,,
,,,tena ukae kimya we kijana,Pumbavu,
toka hapa sebuleni,umepewa lifti sasa umepiga Honi mpaka umechoka,kenge wewe!,,,alifokewa hivyo Didi ambaye alinyanyuka na kuondoka hapo Sebuleni,akawaacha Secilia na Junior
,,,haya sasa,niambie lini utakuja kwangu,na uhakikishe utakaa masaa zaidi ya matatu,,,alisisitiza hivyo Junior ambapo alimsogelea kwa karibu kabisa
,,,jamani,Junior hilo suala ni gumu sana na wewe unajua,,,
,,,ugumu unauleta wewe mama,,!,mbona Didi umempa,sikiliza,naona nikupangie Ratiba kabisa,leo alhamisi,Jumapili nakuhitaji majira ya saa mbili asubuhi mpaka saa sita au saba kabisa,,,
,,,naomba unisamehe Junior,tusifanye hiko kitu,naomba unipe njia nyingine nitafanya kwa hilo ni ngumu kwangu,,,
,,,sawa,hamna shida,ukiweza fanya haya mambo mawili na nitakuacha huru,moja,,,mwambie kaka Martin ulichokifanya na Didi pia umwombe msamaha mbele yangu,mbili,,,niruhusu nimwonyeshe hizi picha zenu wakati mnashughulika,haya sasa kazi kwako,usinambie kama utashindwa au utaweza,ukija Jumapili nitajua umeshindwa kumwambia kaka na usipokuja,tena ukichelewa hata dakika moja tayari nitakuwa nimeshamtumia kaka hizi picha,,,,alimaliza kuongea hivyo Junior kisha akaondoka bila kuongeza neno lolote
,,,hivi ndio nitaachika,,?,Martin akisikia haya itakuwaje jamani,,mungu wangu nisaidie,,,na Didi sijui ataenda kuishi wapi masikini wa mungu,,,au nikimbie tu hii nyumba,,Junior,,!,kwanini imekuwa hivi,,?,nina uhakika ameathirika,sasa kwanini anafanya hivi jamani,,,au nijiue nikwepe hii aibu,,?,,,alijiuliza maswali hayo kichwani mwake ambapo bado alikuwa njia panda asielewe ni uamuzi upi auchukue kukwepa aibu kubwa kama hiyo
Moja kati ya vitu ambavyo unatakiwa kuwa macho sana katika maisha ni NDOA,unatakiwa kuilinda mchana usiku,ni zawadi ya kipekee kama heshima ambayo wengine wanaililia kila siku ila wanaishia kuchezewa na wanaume mwishowe kuzalishwa na kutelekezwa japo hakuna anayependa kufanyiwa hayo,pia wapo wanaume wanaokesha kutafuta wanawake kwa ajili ya kutulia nao katika maisha na kufunga nao Ndoa lakini hawapati japo kwa asilimia ndogo
Jambo la kwenda nyumbani kwa Junior na kufanya naye mapenzi lilimuumiza sana kichwa Secilia aliyekuwa analia tu,wakati mambo hayo yanaendelea Martin hakujua chochote,muda mwingi aliutumia kwa Halima mwanamke aliyeshika ujauzito wake,Didi alichokuwa anawaza ni maisha yake jinsi yatakavyokuwa baada ya Martin kugundua jambo hilo
Tukirudi kwa upande wa Sefu ambaye taarifa zilienea sana kuwa ameathirika kwani watu walishaanza kupata nyepesi za mtaani kuwa Sefu ni mmoja kati ya waliotembea na Walda,uwoga ulimjaa Sefu ambaye hakuwa na amani ya moyo hata kidogo,alichokifanya Sefu,alifungua safari mpaka Hospitarini ambapo jambo hilo lilikuwa kati yake na Mungu wake,moja kwa moja alipima damu yake ambapo alipopewa majibu hakuamini kabisa macho
,,,dokta,embu naomba uniambie kama ninao au sina,,,aliongea hivyo Sefu huku kijasho chembamba kikimtoka,alionekana kuchoka bila hata kufanya kazi ngumu
,,,usijali,punguza Jazba kwanza,jazba yako haiwezi kubadilisha majibu,hivyo ni vyema ukatulia mtoto mzuri na kusikiliza majibu yako sawa eeh?,,aliongea kwa ukarimu Daktari huyo aliyekuwa mama Fulani wa kikubwa
,,,haya Daktari,,,alijibu Sefu kwa upole
,,,unajua,haijalishi majibu yatakavyokuwa,unatakiwa kuyapokea kama yalivyo,ukiwa hauna Ukimiwi haimaanishi wewe ni mzima sana,na unatakiwa kuzingatia ngono salama,pia usiwe mtu wa kufanya mapenzi na wanawake tofauti tofauti,hiyo huatarisha maisha sana hususani kwenye maambukizi ya magonjwa mbalimbali sio UKIMWI tu,,,,vile vile ukiwa na UKIMWI sio mwisho wa maisha kijana wangu,wengi hudhani hivyo na kukata tamaa mpaka kufikia hatua ya kujiua au kuchukua uamuzi wa kuueneza kwa makusudi madai yao hawataki kufa peke yao,lakini amini nakuambia hiyo ni dhambi kubwa sana katik aulimwengu huu,,,
,,,ndio nimeshaathirika hivyo jamani,ukiona Maongezi yanakuwa mengi ujue tayari hivyo,,,Sefu alianza kulia kabisa huku chozi likimtoka kwani alikariri kwamba maelezo yakiwa marefu ujue tayari umeathirika
,,,hapana kijana wangu,nilikuwa nakupa ushauri tu,tena usilie kwani machozi yako yanaweza kuwa uchuro kwako,wewe ni mzima kabisa,,,
,,,Dokta unasema,,?,,Sefu hakuamini alivyoambiwa ni Mzima alirukaruka huku akishangilia chumba kizima
,,,tulia mwanangu,sasa sio kwamba ni mzima basi ndio ikawa fungulia nyuki au mbwa,utulie pia nakushauri baada ya miezi mitatu kupita uje upime tena,sawa,,?
,,,sawa Daktari wangu,nakupenda sana,,,Sefu alijikuta akisema hivyo na kuchukua majibu kisha kuondoka huku akiwa na furaha isiyo na kifani,huku Nyuma Daktari yule mama wa kikubwa aliishia kucheka tu alipomsikia Sefu akimwambia anampenda sana
Ile Sefu kabla hata hajafika mbali kutokea hapo Hospitari akasikia anaitwa jina lake kwa nyuma na sauti nyororo ya mrembo,,,,jamani Sefuuu,,kha,,!,
alipogeuza shingo yake alikutana uso kwa uso na Shani yule anayaishi mitaa ya kwa Zungu,ndiye yule aliyekutana naye kwenye basi mpaka wakafikia gesti na kusuguana,,,,Sefu jamani,mwenzio nilikuwa nimebanwa kweli nyumbani hivyo leo niko na rafiki zangu nimewasindikiza Hospitari,naomba utafute mahali pazuri tutakapotumia hata masaa matatu tu unitoe hii hamu niliyokuwa nayo,maana zimejaa haswa,kuhusu gharama nitalipa kikubwa ni wewe tu mpenzi wangu,,,,aliongea hivyo Shani bila kumpa nafasi Sefu ya kuzungumza ambapo alipomaliza kuongea hivyo,marafiki zake walimvuta mkono na kuondoka naye,,,,tutawas
iliana,,,ilikuwa ni kauli ya Shani aliyompa Sefu baada ya kuvutwa na rafiki zake,,,,Itaendelea