TAFUTA HAPA

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya Saba) 07

Related image

Sehemu ya:7 
Mtunzi: Agatha Francis 

aliposema yale, mke wa Baraka alitulia, nakufanya mwenyekiti aseme"ndugu zangu hapa si mahali pa marumbano, sasa basi mzee Moto kuanzia leo hii, mali waachie vijana hawa kwani si ya kwako", aliposema hivyo mzee Moto alikunja uso wake alinyanyuka na kuondoka bila kusema kitu chochote. 

Mke wa Baraka alimshukuru mwenyekiti kwa kuwasaidia suala lile, kwani tayari walichanganyikiwa lakini mpaka...
muda huo Mark hakuzungumza kitu chochote, mwenyekiti alisisitiza utulivu kwa Mke wa Baraka kwani uwapo mjamzito kelele na marumbano havitakiwi kwani haipendezi, mkewe Baraka alikubali nakuhaidi kua mtulivu mpaka atakapo jifungua. Basi waliaga na kuondoka. 

Walipofika nyumbani Baraka na Mark walikaa chini ya mti kipindi hicho mke wa Baraka akiwa anapika, Mark alionekana kutumia simu bila mafanikio hali iliyomfanya Baraka kuuliza, shemeji vipi tena, mbona kama haupo sawa?, Mark alishusha pumzi mmmnh, nakusema namtafuta mama Careen lakini hapokei simu wala hajibu ujumbe ninaotuma, sina amani kabisa shemeji yangu, sina amani mimi, aliongea hayo nakujikuta machozi yakimtoka. 

Baraka alimuhurumia sana shemeji yake, alipokua anambembeleza mlio wa ujumbe katika simu ya Mark ulisikika, Mark alifuta machozi nakuufungua na ujumbe ulisomeka hivi, "Mpenzi wangu Mark, sikulaumu kuhusu leo, ila nakulaumu kwanini hukuniambia kama kuna mwanamke mwingine kijijini ili mimi nisifike huko, Careen nitamueleza nini?, si unajua tulivyokuzoea, sawa wewe mchukue huyo mwanamke lakini mimi nitaishi vipi bila ya wewe?

Nina mkosi gani mimi kila mwanaume ananiacha njia panda?", ujumbe ule ulimuumiza sana Mark alijikuta akimpa simu shemeji yake ili na yeye asome ujumbe ule, Baraka aliumia sana baada ya kusoma ujumbe ule mara simu iliita tena, alikua mama Careen, Mark alipopokea simu alikutana na sauti ya Careen, "baba mbona leo hujafika nyumbani?, alafu mama anaumwa kichwa", 

Maneno yale yalimuumiza sana Mark na kujikuta akikata simu ambayo hakupiga yeye,Baraka aliyaona maumivu ya shemeji yake kulingana na alivyoonekana, alimsihi kua mtulivu ili afanye maamuzi ya busara, "tulia shemeji yangu ila mimi ushauri wangu uko palepale ata ukioa huku lakini jua utaishi vipi na mama Careen... Usikose 8