TAFUTA HAPA

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya Nane) 08

Related image

Sehemu ya:8 

Maana ni mwanamke unayeonesha kua na mapenzi nayeye tena mapenzi ya dhati", wakati wanabembelezana mke wa Baraka alifika pale, hakuonesha kushtushwa na hali aliyoikuta pale, alianza kuandaa chakula kisha akasema"kaka alafu nilisahau jamani, Suzan atakuja maana amesema amekukumbuka sana pia kafurahia nilipomuambia utaondoka nae, kauli ile ilishangaza karibu kila mtu pale kwani hakuna aliyetegemea hilo.

kisha Mark alimgeukia dada yake nakusema"ina maana dada umedhamiria kabisa niondoke na Suzan", ndiyo dada mtu alijibu kwakujiamini, alipomjibu ndugu yake alianza...
kutabasamu huku akiangalia njia ndogo iliyotengenezwa kwa miguu, wote waliangalia kule ndipo walimuona Suzan akiwa anakuja akionesha kutabasamu, Suzan alikua mwanamke mzuri tu aluyekamilika lakini Mark hakumpend kwani mapenzi yake yalikua kwa mama Careen hivyo hakushughulika sana na uzuri wa mwanamke Yule.

Suzan alifika akamkumbatia mke wa Baraka akisema"wifi nilidhani unanidanganya", basi yeye na wifi yake walicheka kisha alisalimia, Mark na Baraka walimjibu vizuri tu bila kinyongo chochote kisha mke wa Baraka akasema mume wangu tuwapishe kidogo wazungumze twende zetu ndani, basi Baraka alimuangalia Mark kisha aliondoka. 

Suzan alibaki pale na Mark, Suzan alianza kwakucheka kisha akasema"mpenzi wangu eti kweli umekuja kukuchukia?, "Mark alijibu nani mpenzi wako?, mimi sijawahi kukutamkia nakupenda ni wazazi na ndugu yangu walikupenda, ata nikikuoa jua naondoka na wewe kwa ajili ya ndugu zangu, mimi tayari nina mwanamke ninaempenda. 

Kauli zile kidogo zimtoe roho Suzan lakini akajipa moyo kwakusema"haina shida mapenzi ni mazoea utanizoea tu Mark kwani mimi nakupenda, alitulia nakujisemea moyoni"pole sana Mark mimi kwako nafuata pesa tu yaani ukiondoka na mimi hapa utanijua mimi nani wazazi wangu tu sielewani nao sembuse familia yako mbona mtanichikia sana kisha alijichekea moyoni. 

Mark aliinuka nakusema mimi naingia ndani, sawa niitie wifi Suzan alisema, basi Mark aliinuka na alipofika ndani dada yake yaani Mke wa Baraka aliuliza vipi tayari?, kaka yake akajibu anakuita basi alijivuta na tumbo Lake nakutoka nje, swali lakwanza lilikua mumeelewana?usikose 9