Sehemu ya:10
Mtuzi: Agatha Francis
Mark alijibu"sawa" basi walitoka tena nje aliagana na dada yake na safari ya kurudi mjini ilianza na aliongozana na Suzy. Walipokua njiani hakuna aliyemsemesha mwenzie, Mark alikua katulia tu wakati Suzy akishangaa shangaa mandhari ya njia walizokua wakipita, kifupi alionekana ni mshamba tu maana jinsi alivyovalia na alivyokua akishangaa mtu huwezi uliza, utajua tu mtu huyu ni wakijijini.
Basi walifika nyumbani, Mark alimkaribisha Suzy ndani kisha aliaga na kutoka akidai hatochelewa atarudi, Suzy aliuliza "jamani Mark yaani tumefika tu...
unaondoka na unajua mimi mgeni jamani", aliongea kwa madeko, Mark hakujibu kitu akafungua mlango nakutoka, Suzy alibaki ndani peke yake.
Mark alitembea mpaka alifika katika mgahawa wa Mama Careen kwani alikua na uhakika atamkuta huko, ni kweli alimkuta mama Careen akiwa anahudumia wateja wake, lakini mama Careen alipomuona Mark alimfuata akampa kiti na kusema "subiri kidogo Mark", aliendelea kuhudumia wateja wake na alipomaliza alirudi pale nje alipokua ameketi Mark.
"habari za huko utokako Mark", mama Careen alianza, Mark alijibu mama Careen naomba unisamehe kwa yaliyotokea kwa dada yangu, sikupanga iwe vile mimi, mama Careen usijali Mark mimi nimesahau kabisa ndiyo maana naendelea na kazi wala usijali lakini mwanamke mwenyewe umeonana nae?swali hilo liloshusha machozi kwa Mark, mama Careen alisema kwa upole".
Mark siunajua tupo nje hapa tena kazini si vizuri ukalia kama nimekuumiza basi usijibu utanijunijibu siku nyingine tafadhali futa machozi, Mark alisema"mama Careen mwanamke yupo nyumbani roho yangu inaumia sana mama Careen amini mimi nakupenda wewe Yule si chaguo langu bali la ndugu zangu niamini na kukuhakikishia hilo mimi sitafunga naye ndoa nitakuoa wewe mke wangu, mama Careen akasema
"usijali nenda kafanye maisha na mwanamke aliyeko nyumbani mimi nijue nitamlea vipi mwanangu pia muheshimu tu kama mkeo na na ufunge naye ndoa kwani mimi ndugu yako hajanikubali na hatokuja kunikubali kamwe katika maisha yake", kauli ile ilimuumiza sana Mark alijikuta akiondoka eneo lile bila kuaga, mama Careen alisikitika sana kwani alimpenda Mark lakini hakua na chaguo maana ndugu hawakumkubali..
Usikose 11