TAFUTA HAPA

STORI YA KWELI YA AJABU NA YAKUSISIMUA

Kulikuwa na mzee mmoja ambaye alikuwa tajiri sana, Mzee huyu alibahatika kuwa na binti mmoja na ambaye alimpenda sana na hata
kumwandika kuwa mrithi wa mali zake zote pindi mzee atakapoiaga dunia.

Mzee huyu alimiliki biashara kubwa sana sana na zenye kuingiza kipato kikubwa na aliogopeka
sana sana katika eneo hilo hasa kwa kwa utajiri wake na ukatili wake pia.

Siku moja mzee huyo alipata taarifa kuwa mtoto wake wa pekee alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kijana mmoja ambaye anatoka
katika familia isiyojiweza na tena ya kimaskini sana,na wazai wake walikuwa wakifanya kazi katika
moja ya mashamba ya tajiri huyo.

Yule tajiri alijawa na hasira na kuona kama ilikuwa ni fedhea kubwa sana kwa familia yake
na akamuita binti yake na alipomuuliza binti yake alikubalia, mzee kwa hasira akawafukuza
wale wazee na kuahidi kutoa fedha nono kwa polisi yeyote atakaye mtia mbaroni kijana Yule.

Basi kijana Yule ikabidi amfuate binti na kumwambia hali halisi na kuwa sasa wazazi wake wako katika hali mbaya na yeye anasakwa hivyo
ni vyema wakiachana maana anaona Maisha yake yapo hatarini pamoja na familia yake.

Binti Yule akawa akiiba fedha na kuwapelekea wazee wale ili wajikimu na baadae akamshauri
Yule kijana kuwa wakimbie waende mbali wakajifiche na kuanza maisha yao wakiwa kama mme na mke. 

Baada ya mabishano ya siku
kadhaa Yule kijana akakubali na binti akachukua fedha nyingi za kuweza kuanza maisha popote
pale watakapoamua kuishi.

Yule tajiri alipatwa na butwaa na hakuamini kama binti yake kakimbia, akaamua kuwachukua
wazazi wa yule kijana na kuwafunga bila mafanikio na kuamua kuwaachia huru. 

Mkewe na yule tajiri aliendelee kuhuzunika na kunung’unika kwa muda wote mpaka mmewe
akaamua kutoa tangazo kwenye magazeti ya nchi ile na kusema amemsamehe mwanae hivyo
arudi tu na ameafikiana nao kuwa waoane. Hivyo warudi kwa ajili ya harusi.

Taarifa zikamfikia yule kijana akiwa na mpenzi wake yule mtoto wa tajiri, kwa pamoja wakaamua kurudi na wakapokelewa na yule
mzee ambaye akawaambia kuwa watafunga harusi mapema wiki itakayofuata na gharama
zote zitakuwa zake na yule kijana
atashirikiana na yule binti katika kusimamia mali za yule mzee.

Siku tatu baadae wakaamua waende kuandaa suti na shela kwa ajili ya harusi, waingia kwenye
duka la nguo za harusi binti alivyaa shela ikawa imemkaa safi sana na yule kijana naye suti ilimfaya aonekanye maridadi sana,akaamua
kabla ya kuvua ile nguo avuko barabara aende akanunue ice cream maana binti Yule alikuwa
anapenda sana kula ice cream.

Wakati kanunua ile ice cream na anavuka barabara gari likamgonga yule kijana na yule binti baada ya kuona vile alimkimbilia na
alipofika pale damu iliruka na kutengeneza doa kwenye ile shela, wakamchukua na kwenda nyumbani ambako baadae mazishi yalifanyika.

Baada ya mazishi binti Yule aliendelea kuhuzunika na hakutoka ndani kabisa.

Siku moja baada ya miezi kadhaa kupita usiku akiwa kalala alimtokea bibi mmoja na kumwambia katika ile shela kuna doa hivyo
anatakiwa alifuo litoke au balaa litamtokea. 

Yule binti kweli asubuhi aliamka na kwenda kuitazama ile shela na kukuta ina doa, akafua sana mpaka doa akaona limeoptea. Lakini
alipolala tena Yule bibi akamtokea tena na kumwambia lile doa halijatakata hivyo afue tena
au balaa itaikumba familia yake.

Siku ya pili akaamka na kufua lakini kila alipofua yule bibi alimtokea na kumwambia vile viele,yule
binti akaona sasa kachoka ni vyema amshirikishe mama yake.

Mama yake akashangaa sana kwani
naye aliota ndoto kama ile ile na alikumwa akiogopa kuwashirikisha. Mama na mtoto wakanya siri na kulifua tena lile shela na hata
baada ya kulifua yule bibi aliwatokea tena na kuwaambia kuwa bado doa lipo.

Mmmh kazi ikawa ngumu ikabidi wamshirikishe baba, baba naye kumbe wamekuwa akitokewa na
yule bibi na akawa anona sio vyema kuwashirikisha wanafamilia.

Basi baba akawaamuru waichukue ile shelana kwenda kuifukia. 

Baada ya kuifukia Yule bibi aliwatokea na kipindi hiki alikuwa mkali zaidi na kuwaambia wana siku mbili tuu za kulifukua lile shela na kulifua mpaka doa litakate la sivyo kuna jambo kubwa litawatokea .

Familia nzima walilifua kwa ushirikiano na wakakubaliana kuwa sasa limetakata na wakalianika na kulipiga pasi baada ya kukauka na uliweka sandukuni.
Usiku wakiwa wamelala.waliambia wameshindwa.

Basi familia siku ya pili walikutana na kusimuliana wote wakaonyesha
kuota ndoto sawa. Siku ya pili wote wakaenda kazini na kumwacha yule binti aiwa nyumbani peke yake.

Akiwa kaka peke yake na huku akisubiri mwisho wake huku akilia kwa uchungu na kumkumbuka
mchumba wake yule kijana,mara mlango ukagongwa na baada ya kumkaribisha binti yule alistaajabu kuona ni yule yule bibi mzee ambaye amekuwa akiwatokea usiku. Lakini mara hii alikuwa kashika kopo dogo mkononi na
kumpa yule binti kasha akaondoka zake.

Je unafikiri Yule bibi kizee alimpa kopo la nini?

Jibu ni kuwa alimpa kopo la sabuni ya unga aina
ya omo ambalo hutoa madoa kwa uhakika

Ha ha ha ha ha ha ha ha ni janga sana.
Kama ulisoma huku ukifikiria uchawi shindwaaaaaa