TAFUTA HAPA

Siri Chumbani- 1

Huyu ni Manka, mmh jamani Manka anawachanganya akina kaka, wajomba na hata wazee, oshiii! Kwa kifupi hana kasoro, ukibahatika kumuona na kumchambua ungeweza kudhani ukikufuru kuwa pengine mama yake aliamua kumuumba mwanaye mwenyewe na kuhakikisha amekuwa mzuri lakini ukweli kazi hii kubwa ya uumbaji ilifanywa na Mwenyezi Mungu pekee, mtoto ana kisura kilaini kama cha mtoto mchanga, ngozi nyororoo...sijui ana kula nini, meno meupe yenye mwanya wa wastani, akicheka hakika utapenda, wasichana wenziye wanamtamani, wanataka awe na umbo kama lake, wanaume wanaotaka kuoa wanaweke wazuri waliomuona wanachukulia mfano wa Manka, hana maringo hiyo ndiyo sifa yake kuu, ana umbo la kuwateka watu wa kila rika.

Siku hiyo alibaki mwenyewe, nyumbani kwake maeneo ya Sinza kwa Remmy, alikuwa alifanya usafi na baadaye akaendea bafuni kuoga, alijisugua na alipomaliza aliingia chumbani na taulo laini akajifuta maji mwilini na kuanza kupakaa mafuta ya kuirutubisha ngozi yake, kila alipojiona kiooni alimsifu mwenyezi Mungu kwa kazi nzuri ya uumbaji.


Mbele ya Dressing table yake iliyojaa vipodozi vya dharama, alitoa manukato ya J- Lo na mafuta ya Max Clare na St Elizabeth Aden, alipomaliza akapakaa uso wake ‘poda’ kidogo kisha akavaa sketi fupi inchi 12 na kitopu kilichoacha wazi kitovu chake kilichoingia ndani nusu inchi, hali iliyomfanya avutie sana, juu ya kitovu alikuwa na matiti makubwa kiasi yenye kuleta yaliyojaa na kusimama kwa kujitegemea ingawa alivaa sidiria.

Simu ikaita, akatembea kivivu na kuiokota, hakujua ni nani, zilikuwa namba mpya kutoka nje ya nchi.

“Haloo! Manka...Habari za Tanzania!” Sauti ya upande wa pili ilisikika.

“Nzuri, shikamoo!” Manka alishaijua sauti ya mtu aliyepiga.

“Jamani, si nilikuambia sipendi shikamoo, ok, unaendeleaje?” Ilikuwa sauti ya mzee Alex Ganza, mfanyabiashara maarufu jiji la New York na Afrika mashariki, ni mtanzania aliyezaliwa Kilimanjaro na kununua uraia Marekani.

“Safi! Nimekumisi sana Anko!” Manka alipenda kuita Anko, ingawa siri halisi hakuwa Anko.

“Mi’zaidi, naomba uniite mpenzi...Manka hukumbuki nilikulea ili uwe mke wangu!”

“Najua na nakuheshimu kama baba yangu, umenilea na nilikuwa nataka upate mkwe siku za karibuni!” Manka alisema , lakini kauli hiyo ikamtibua Alex.

“Mkwe! Nooo! Usiolewe na mwanaume mwingine, nitakuoa mimi, nakupenda Manka, toka ukiwa na siku moja duniani nilikulea, nataka nile matunda yangu..”

“Sijui kama itawezekana, tayari ninaye mwanaume ninayempenda!”

“Mwanaume gani mzuri kuliko mimi, mwanaume gani tajiri kushinda mimi, mwanaume gani ambaye angeweza kukuokota jalalani na kukusomesha hadi leo una elimu ya juu na unasimamia mali zangu? Wewe ndiye mke wangu, Manka...nakupenda!”Alilalaimika kimapenzi, Manka akajikuta akimuonea huruma, lakini bado alikuwa ana ampendaye.

“Ok, nimekuelewa, njoo basi tuongee vizuri, nakupenda wewe pamoja na huyo mpenzi wangu anayeitwa Boy...” Kauli hiyo ilimrufahisha nusu na kumuudhi nusu, iliyomchukiza ni kwamba anampenda pia Boy.

“Sawa, nimeota ndoto ya ajabu, usiku wa kuamkia leo!” Akabadili mazungumzo mzee Alex Ganza.

“Ndoto gani?”

“Siri ya Chumbani!”

“Unamaanisha nini, sijakuelewa mpenzi!” Naye akaamua kumfurahisha kwa kumuita mpenzi.

“Nikija nitakueleza, mapumziko mema mpenzi wangu!mmwaaa!”

“Na wewe pia! Mmmwaaaa!” Alimaliza na kukata simu.

******


Alipokata simu, akatafuta jina la mpenzi wake anayetingisha mtima wake na kumpigia, huyo ndiye aliyetaka kumkabidhi mwili wake auendeshe anavyotaka.

“Boy, njoo basi unipeleke kiwanja, ninazo hela za kutumia mpenzi wangu, njooo! Nipo nyumbani peke yangu,” alilalamika kikike akizungusha jicho la mahaba, jicho ambalo akikukata lazima apagawe na kudhani anakutamani, mtoto huyu! Mmh!.

“Poa, upo wapi?”

“Njoo nyumbani, msaidizi wangu wa kazi za ndani hayupo, nakupenda sana na usichelewa!”

“Nakuja usijali!”

“Mwili mzima unachemka, naomba ujiandae, kuna zawadi nitakupatia kwanza, ndipo twende zetu viwanja..njoo naumia!”

“Heeh! Unaumia kitu gani sweet!”

“Nakusubiri, usichelewa damu inachemka, natamani joto la karibu ...” kumbe Boy hakuwa mbali alikuwa maeneo ya Sinza madukani, akashuka kwenye daladala na kuelekea mtaa wa pili alikokuwa akiishia Manka, jumba la kifahari lililojengwa na Alex Ganza, alipofika alifungua mlango na kuingia hadi sebuleni ambako alimkuta Manka amejilaza sofani akiwa mweupe pee! Loh! Macho yakamtoka si kidogo, ilikuwa ni maajabu ambayo hakuwahi kukutana nayo, mtoto alifumba macho sijui alihisi baridi ama vipi, alikuwa amemtega si kidogo.