TAFUTA HAPA
SIMULIZI KUTOKA JIKONI-2
DADA JESCA APAKATWA NA SHEMEJIYE JIKONI – WAFUMANIWA.
Mtunzi; Issa S. Kanguni
Simu iliita Da’Jesca akiwa bado kitandani hajaamka. Ni siku ya jumapili, siku ya mapunziko kwa waatumisi wa nafasi kama yake. Yeye ni katibu muhtasi, pia ni mhazini kwenye shirika moja la kiserikali lenye ofisi zake kwenye jengo la JM Mall lililopo Samora Avenue kakikati ya jiji la Dar es Salaam. Alipepesa macho kisha akageuza kichwa upande kuangalia saa ya ukutani. Inakaribia saa mbili unusu. Mwili aliuhisi mchovu kwani jana alikunywa bia zaidi ya nne wakati kiwango chake cha kawada ni chini ya bia tatu na akalala saa nane wakati kiwango chake cha kawaida ni si zaidi ya saa sita. Alikuwa akimsubiri mumewe ambaye alitarajiwa kurejea toka safari jioni ya jana. Aliangalia tamthiliya TBC na baadaye Bongo Movie.
Baada ya muito wa tatu alinyoosha mkono na kuichukua simu kwenye stuli kando ya kitanda. Alihisi ni mume wake, lakini alipoangalia jina la mpigaji, alitabasamu. Alijikohoza kusafisha koo. Akapokea.
‘Halloo’ sauti ilitoka ya mkwaruzo ikapenya kwenye kinasa sauti cha simu yake, TECNO Y3.
‘Halloo, habari za asubuhi’ sauti ya kiume ilimjibu. Si ya mumewe.
‘Nzuri tu, kumbe shem, za kwako?’ alijifanya kushangaa.
‘Mi nipo poa shemeji. Ina maana hukunifahamu? Namba yangu umefuta nini?’
‘Hata sijaifuta, nimei-save kwenye simu nyingine si unajua tena enzi zetu hizi, watu tunamiliki simu zaidi ya moja hata kama moja ingelitosha kwa matumizi yetu. Ila sauti yako siwezi kuisahau, nimeiweka kichwani na inanisisimua kila ninapoisikia. Mzima wewe?’
‘Ah, umeanza masihara yako. Mi nashukuru Mungu nimeamka salama.’ Alisita kidogo kabla ya kuendelea ‘vipi bro yupo? Naona simpati kwenye simu wakati ratiba yake ilikuwa ni kuingia Dar jana.’
‘Hapana. Bado hajarudi. Jana nilimsubiri sana. Simu yake pia ilikuwa haipatikani.’ Sauti yake mororo ilianza kurudi.
‘Basi anaweza kuingia leo.’
‘Sidhani.’
‘Eee, kati ya leo usiku na kesho alfajiri.’
‘Ok. Mi naendelea kusubiri arudi, aje aingie leo.’
‘Basi baadaye shemeji.’ jamaa akajifanya kuaga.
‘Baadaye’ kabla hajakata simu akakumbuka kitu. ‘By the way shem, kwani leo unaingia kazini?’ alimuuliza huku akijifunua shuka. Akainuka na kushusha miguu yake laini chini, kifua wazi mapaja nje, simu sikioni.
‘Hapana leo siendi kazini. Gari ipo Kurasini kwenye foleni ya kupakia. Ntaenda ofisini kesho kwa maandalizi ya safari jioni.’
‘Ahaa… poa’
‘Kwani ulikuwa unatakaje shemeji’angu? Naweza kwenda kwa ajili yako.’
Da’Jesca alisita kidogo. Anamtamani Denis kimapenzi toka kitambo. Anatamani japo amwone tu akonge roho yake. Jitihada zake za kujaribu kumnasa zilikwisha gonga mwamba siku nyingi. Denis anajua kumkwepa. Anajifanya haoni akitegwa wala hasikii akidokezwa, tangu kipindi kile Da’Jesca akiwa kimada tu wa Tito hadi sasa kawekwa ndani kwa pingu za maisha.
Huku simu ikiwa bado sikioni, hakuna anayeongea, Da’Jesca aliinuka akaenda dirishani na kukunja pazia kwa mkono mmoja kuruhusu mwanga na hewa zaidi. Kijiupepo mwanana cha asubuhi kilimpepea na mwanga wa jua ukaangaza uso. Matiti kifuani pake ungelidhani ni ya msichana aliyevunja ungo mwezi jana.
‘Nilitaka shem kama ungekuwa na nafasi uje unisaidie. Jana nililewa nikavuruga vitu hovyo. TV haiwaki na redio ndo usiseme…’ alimwongopea.
‘sasa kwa tatizo hilo si ni bora ungemwita fundi?’
Da’Jesca alitamani amjibu kwa hasira ‘fundi wa nini we zoba njo unikunje’ lakini badala yake akasema ‘Poa shem, ntamwita fundi.’
‘Idiot’ aliongeza kwa sauti baada ya kukata simu.
Alijinyoosha akapiga miayo kisha akaanza kutandika kitanda na kupanga vitu mle chumbani. Da’Jesca ni msafi na anapenda vitu vyake vikae kwa mpangilio, siku zote.
Mume wake yupo safarini kwa takriban siku tisa sasa, amepeleka shehena ya bidhaa kwenye nchi jirani ya Zambia toka kwenye bandari maarufu katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Kati. Bandari ya Dar es Salaam. Kabla ya safari hii ya Zambia alipeleka mizigo Congo, kabla ya safari ya Congo alikuwa Rwanda na kabla ya safari ya Rwanda alipeleka `nondo na vifaa vingine vya hardware Mwanza ambako alirudi na shehena ya marobota ya pamba na zawadi ya mkufu wa dhahabu wa kiunoni kwa mkewe.
Tangu wafunge ndoa leo ni siku ya mia moja na nne ambapo kati ya siku hizo ni siku 28 tu alizowahi kulala nyumbani Dsm. Tena hizo ni ukichanganya na zile siku anazorudi zaidi ya saa 7 usiku akiwa amechoka kiasi cha na kuondoka kabla ya saa kumi na mbili alfajiri.
Da’Jesca amemmis mume wake. Kimwili. Seriously.
Da’Jesca na mume wake wameanza kujenga nyumba yao kule Boko Chasimba, ila kwa sasa wanaishi kwenye nyumba ya kupanga hapa Sinza. Nyumba ni ndogo ya chumba kimoja, sebule, maliwato, stoo na jiko. Self contained. Kuta zimenakshiwa vizuri kwa rangi ya maziwa ndani, urujuani nje na nyeupe darini. Sakafu ni ya marumaru za kisasa. Ni nyumba nzuri kwa mtu asiye na familia kubwa kama ilivyo Tito. Uzio wake nje ni wa futi tatu tu wenye geti jeusi, bado haujapigwa lipu wala rangi. Nafasi baina ya uzio na nyumba ilitosha kuegesha kama magari mawili hivi madogo. Da’Jesca hana gari bado. Katikati ya uwanja kuna mfenesi mdogo. Unafaa kwa kivuli lakini bado haujaanza kutoa matunda.
Asubuhi hii hali ya hewa ni nzuri kulinganisha na siku mbili tatu zilizopita. Jua linajitahidi kupenyeza miale yake licha ya kuzongwazongwa na vijimawingu mdaa. Miungurumo ya magari kwenye barabara ya Shekilango haikusaidia kumfanya Da’Jesca arudishe mawazo yake kumfikiria mumewe Tito aache kumfikiria Denis.
Alijifunga khanga nyeupe kifuani, akafungua mlango wa chumbani aelekee bafuni. Alitembea kwa mwendo wake wa kawaida tu, ila mwili wake, kifua kilivyomsimama na nyuma kulivyomcheza ungedhani anafanya kusudi. Huyu binti kapata mwili. Ndiyo maana siku zote ninaposimulia kuhusu Da’Jesca huwa najitahidi sana nisivutwe katika kumsifia uzuri na maumbile. Sentensi zangu za kumwelezea ni za juu juu tu. Ni mzuri kuliko ninavyomwelezea. Amependelewa umbo, sura na haiba.
Akiwa bafuni anachukua sheva na kupachika wembe mpya – Gillette Silver Blue. Choo chake ni kisafi cha marumaru nyeupe sakafuni na ukutani. Sehemu ya kuogea ipo chini kwa sentimita kama nane hivi kulinganisha na kwenye sinki la choo. Alitegesha kioo akajisafisha kwapa la kushoto halafu la kulia, kisha akachutama kumalizia sehemu nyingine. Mwanamke usafi bwana.
Robo saa baadaye alitoka bafuni chupi mkononi, keshaoga.
ITAENDELEA…