TAFUTA HAPA

Mpangaji - 1


CHOMBEZO: Mpangaji
Sehemu: 01
Mtunzi: Frank Masai
Simu:

Mnamo mwaka 2008,nilimaliza kidato cha nne katika shule ya Tabora Boys. Baada ya kumaliza shule,nilirudi zangu nyumbani Morogoro kwenye nyumba ya baba na kuanza maisha mengine kama raia wa kawaida.

Nyumba ile ilikuwa kubwa sana, na ilionekana kubwa zaidi baada ya kaka zangu kuondoka na kwenda kuanza maisha ya kujitegemea. Kaka yangu wa kwanza alienda Arusha, wa pili akaenda Dar na wa tatu yeye alienda Dodoma,hiyo yote ni katika saka za maisha.
Shule niliyotoka yaani Tabora Boys, kwa kifupi ilikuwa haina wanawake. Wanawake tulikuwa tunaonana nao Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo tulijumuika nao pamoja katika ukumbi wa chuo cha Uhaziri kilichopo pale pale Tabora. Yaani namaanisha kuwa, kila ilipofika Ijumaa ya mwisho wa mwezi, zile shule zilizokuwa na jinsia moja pale Tabora ,zilikutana na kubadilishana mawazo huku wale wenye wapenzi wakienda mbali zaidi kwa kubadilisha na kukabidhiana viungo vyao vya mwili.

Mimi nilikuwa msanii tu! Yaani sina demu wala nini, tabia yangu ilikuwa ni kuchukua wasanii wenzangu wale wasiokuwa na wanaume. Kwa siku hiyo moja ya Ijumaa, niliweza “kugonga” watoto si chini ya wawili,kila mmoja kwa wakati wake.

Tabia hiyo ilikomaa sana katika mwili wangu,kitu ambacho kilisababisha niwe kila wakati nataka “kula mizigo” . Hivyo pindi hamu ilipokuwa inanikamata sana,nilijifanya naugua ili wanitoe nje ya shule eidha kwa kunipeleka hospitali au kunipa rikizo ya muda mfupi.

Kitendo cha wao kunipa nafasi hiyo, kilinifanya niwe natoroka mahala wanaponiacha na kwenda zangu sehemu zangu maalum kwa ajili ya kujichukulia “mizigo” ya “kugonga”, na pindi nilipokuwa nakosa sana mizigo hiyo, basi nilihamishia majeshi yangu kwa yeyote nitakaye kutana naye lakini wa jinsia ya kike.
Nakumbuka siku hiyo nilishikwa na hamu ya kufanya ule upuuzi kiasi kwamba nilishindwa hata kwenda darasani. Kitendo kile kilifanya yule msimamizi wa wanafunzi pale shuleni kuniona kama naumwa,hivyo aliniongoza hadi hospitali moja ya pale Tabora na nilipofika, ndipo nikajidai naumwa zaidi.

Nilijiregeza kiasi kwamba nilishindwa hata kutembea,hivyo nikaletewa kile kiti cha wagonjwa wasiyojiweza ili kinisaidie kuingia hospitali. Baada ya kuniingiza mle, yule mwalimu akabaki nje kwa ajili ya kusubiri majibu yatakayotoka kwa yule aliyenipokea.
Ile kufunga ule mlango niliyoingilia, nilinyanyuka haraka na kuanza kuongea na yule muuguzi aliyenipokea huku nikimshawishi kwa uongo mwingi ili asinidunge sindano zao,hasa diripu.
“Kaka, unataka hela hutaki?”. Nilinyanyuka na kumtupia swali yule jamaa aliyekuwa anahangaika kunisukuma na kile kiti cha wagonjwa.

Kitendo cha mimi kunyanyuka vile ghafla,kilimfanya kidogo ashtuke na kuhisi kuwa nimechanganyikiwa.

“Wewe si unaumwa wewe? Au ndiyo Malaria inakupanda kichwani?.Aliuliza yule kaka.
“Tulia kaka, skonga kuna ukame sana. Hapa bila kuzuga naumwa basi kule skonga ningebaka wenzangu. We sema, unataka hela au hutaki”.Nilijitetea kidogo na kurudi kwenye mada yangu.

“We unataka ufanye nini? We mwenyewe kwanza ni mwanafunzi,halafu unaniulizia mfanyakazi kama nataka hela. Inakuwaje hiyo?”.Jamaa alikuwa mbishi kuelewa,ila nikamsawazisha.

“Sikiliza Bro, mimi hapa siumwi. Cha msingi, wewe nibandike bandike hayo madiripu halafu muite huyo ticha aje kuniona. Usimruhusu aende kwa daktari,kwani ukifanya hivyo utakosa hela”.Nilimwambia hayo huku nikimwangalia usoni nikisubiri jibu lake.

“Ehee, nakusikiliza dogo. Au ndo umemaliza?”.Yule muuguzi akauliza tena.
“Kwani Bro hujanielewa wapi? Mbona unakuwa na fuvu gumu?”.Nilimuuliza kwa jazba kidogo huku nasukuma kichwa chake kwa kidole cha shahada.

“Dogo sikiliza, hapa tunasaidiana. Mimi nikikuwekea hayo madiripu,nitapataje hiyo hela?”. Jamaa aliniuliza swali hilo.

“Kumbe tatizo ni hilo. Akija we zuga kuwa unanihurumia sana,halafu mwambie bei ya haya madiripu pamoja na hela ya msosi wangu nitakao kula nikiwa hapa. Usimruhusu aende kwa daktari mkuu, maliza hapa hapa. Mwambie wewe utapeleka taarifa zote ofisini”.Nilimaliza na yule muuguzi kwa tabasamu,akachukua maplasta na kuanza kubandika ile mirija mikononi mwangu bila ya zile sindano, wakati huo ilikuwa ni mida ya saa saba mchana.
“Sasa dogo, aking’ang’ania kwenda kufanya malipo ofisini je?”.Yule jamaa muuguzi aliniuliza baada ya kumaliza kunitundikia zile diripu uchwara.

“Lile ticha siyo janja, halijui lolote. Yaani pale skuli kazi yake kusimamia makazi tunayolala na siyo kufundisha. Halafu mimi nina kadi hii ya bima ya afya, hivyo wewe usiwe na wasi. Mimi matibabu yangu ni bure”.

“Ha ha haa, hapo sawa nimekuelewa. Sasa ngoja niende kwa ticha lako”.Jamaa akawa anaondoka kwenda kumuita mwalimu yule niliyekuja naye.
Baada kama ya nusu dakika,waliingia huku mimi nikiwa kama sijielewi pale kitandani.

“Ticha, aisee dogo anaumwa sana”.Nilimsikia jamaa akianza kuongea na ticha wangu.
“Kwa hiyo ni nini kinamsumbua?”.Akauliza ticha.
“Nimecheki mapigo yake ya moyo ndiyo yanaenda kasi sana,hivyo yaonekana ni BP. Ila usiwe na shaka sana. Wewe niachie elfu hamsini za matibabu pamoja na tupesa kidogo kwa ajili ya chakula cha mgonjwa akihamka.

Siwezi kuendelea na matibabu bila kupata msaada wa kifedha ili tununue dawa zake na vitu vingine muhimu kama hizo diripu ambazo anatakiwa atundikiwe tatu”.Jamaa muuguzi alijielezea nia yake,na bila kipingamizi,yule ticha aliingiza mikono yake kwenye mfuko wa suruali na kuibuka na waleti iliyonona kiasi chake.
Wakati huo mimi nilikuwa namuangalia kwa jicho moja la kuiba, na nilishuhudia akitoa noti saba za elfu kumi na kumkabidhi yule jamaa.
“Sasa dokta, fanya harakati huyu mtoto apone. Mimi nitakuja kesho ili nijue ni nini kinaendelea, sawa dokta?Akiamka mpe salaam zangu”.Ticha alimalizana na yule jamaa muuguzi na kuanza kuondoka huku akisindikizwa na yule muuguzi ambaye kwa kumuangalia alikuwa ana ukame sana kifedha,hivyo zile hela kwake ilikuwa kama bahari kutokea jangwani.

“Dogo tumewin. Kweli ili ni bonge la boya. Sasa sikiliza, kanipa elfu sabini, wewe chukua hii thelathini halafu pitia huo mlango kafanye yako.
Huu wa kuingilia mimi naufunga, we ukirudi pitia mlango huo huo halafu njoo ile ofisi yangu kunipa taarifa,mwisho iwe saa kumi na mbili, sawa?”.Yule jamaa muuguzi alinipa maelekezo ya nini cha kufanya baada ya kuhakikisha yule ticha katokomea kabisa pale hospitali. Nilimjibu kwa kuitikia poa huku nazitoa zile diripu na kuanza kutoka nje.

Niligundua kuwa yule jamaa alikuwa ni muuguzi wa zamu ambaye ana cheo kidogo,na katika hospitali ile,wanafunzi walikuwa wana sehemu zao maalum kwa ajili ya kulazwa na siku hiyo kulikuwa hakuna mwanfunzi aliyeletwa zaidi yangu.

Niliingia viwanjani na kuanza kutafuta mwanamke wa kutuliza maumivu yangu huku nikiwa na hamasa kubwa ya ujana wangu ambao sikufahamu kuwa ni maji ya moto.

Kiukweli soko lilikuwa limedoda siku ile, hadi saa kumi na moja na nusu, nilikuwa sijapata goma la kunisuuza maumivu yangu, hivyo niliamua kurudi zangu hospitali na breki ya kwanza ilikuwa ni kuingia kwenye ile wodi na kubandika yale madiripu na kisha kuanza kupiga kelele kana kwamba nilikuwa nimetoka usingizini.
Haikuchukua hata dakika, yule jamaa alikuja huku katabasamu na kuniuliza.
“Vipi dogo, umefanikiwa?”.
“Aaah, huko majanga tu! wamehadimika kama bia ya bingwa”.
“Kwa hiyo, vipi sasa?”.
“Leo usiku nitatoroka, nitajifanya napunga upepo halafu naondoka. Nitarudi baadaye”.
“Hapana dogo,hiyo ya usiku sikuruhusu. Ukipigwa je? We tulia, kesho tutapanga tena”.
“Poa kaka, ila naumia mwenzako”.
“Tulia dogo, vumilia hadi kesho. Sasa hivi naondoka, namuachia maagizo muuguzi mwingine. Toa hayo madiripu halafu jifanye umepata nafuu kidogo”.Jamaa aliongea hayo na kutoka nje ambapo aliniacha mimi nabandua yale maplasta na kisha kukaa kitako.
Baada ya dakika tano,yule jamaa muuguzi aliingia na muuguzi mwingine ambaye nilipomtazama moyo wangu ukawa kama umekufa ganzi. Nikashindwa kuyatoa macho yangu usoni pake na kunifanya nizidi kushikwa namshawasha mwingine wa hali ya juu.
“Habari yako mgonjwa”.Ilikuwa ni sauti tamu na nyororo ikipita masikioni mwangu na kusababisha akili na ubongo wangu kuhama kwa muda na kujenga fikra za kishetani katika mwili wangu.

“Dogo unasalimiwa, mbona umekaza macho? Malaria ndiyo inazidisha kasi nini?”. Aliuliza yule jamaa muuguzi kitu ambacho kilinifanya nitoke katika yale mawazo yangu potofu.
“Hamna Dokta, sema akili yangu inawaza itakuwaje hadi kesho ikiwa hivi hivi. Poa dada, mambo vipi?”.Nilimjibu yule jamaa muuguzi na kumsalimia yule muuguzi aliyeingia naye.
Muuguzi yule alikuwa ni mdogo kimwili na mwenye rangi ya kuvutia sana. Alivalia gauni lake la kiuguzi ambalo kifuani lilimshika vizuri na kusababisha kile kifua chake chenye marimao mawili yaliyokomaa kubetuka kidogo na kusababisha hamsha nyingine katika mwili wangu.

“Poa tu! Hali yako inaendaje?”.Aliuliza tena yule dada.
“Mimi poa na ninamshukuru Dokta kwa kazi nzuri hadi hivi sasa naongea na wewe”.Niliongea maneno ambayo ni msomi pekee angejua nina maana gani. Hiyo shukrani kwa dokta haikuwa kwa ajili ya kunitibu, ila utaijua baadaye napoendelea kukusimulia.
“Haya dogo, mimi nataka kwenda zangu nyumbani sasa hivi. Wewe ukiwa na shida yoyote, muite huyu muuguzi. Anaitwa Nesi Subira, yupo hapa kwa ajili ya field au kwa Kiswahili field ni mafunzo ya vitendo”. Aliongea jamaa yule muuguzi huku mimi nikibaki na maneno machache kichwani mwangu yale ya ‘Wewe ukiwa na shida yoyote, muite huyu muuguzi’.
Nilitabasamu na kumuaga dokta ambaye alianza kutoka nje ya mlango ya wodi ile huku nyuma yake akifuata yule Nesi Subira.
Baada ya wale wauguzi wawili kutoka nikaanza kujiwazia moyoni jinsi ya kumpata Nesi Subira ambaye kwa wakati huo tayari alikuwa kajaa akilini mwangu hasa kwa kile kivazi chake nadhifu na cha kuvutia kilichokua kifupi kiasi.
Ufupi ule wa kile kivazi ulisababisha miguu yake nyororo kama losheni ya cocoa butter kuonekana hadi juu kidogo ya magoti, na ile michirizi nyuma ya miguu yake ndio haswaa ilimuamsha Prince na kusimama dede pale kitandani.
Mawazo ya kumfikiria Nesi Subira yakaniteka akili na kujikuta nikibebwa na usingizi ambao ulikuja kuisha baada ya kusikia sauti ile ile ya Nesi Subira ikiniamsha.
“We kaka, we kaka. Hamka ukapate chakula”.Aliniambia Nesi Subira baada ya kuamka.
“Dada mimi siwezi, yaani hapa tumbo linanivuruga sana. Kwani saa ngapi sasa hivi?”.Nilizuga na kumuuliza swali.
“Sasa hivi saa mbili na nusu, ndiyo muda wa wagonjwa waliyo katika uangalizi kwenda kupata chakula”.Alinia
mbia yule Nesi Subira baada ya kuangalia saa yake mkononi.
“Aaah, mi siendi bwana. Kama vipi kaniletee huku huku. Chukua hela hii hapa”.Nilimwambia yule Nesi huku namkabidhi noti ya shilingi elfu kumi.
“Haya kaka….”
“Niite Prince”.Nilimkata kauli kwa kumtajia jina langu.
“Haya Prince, kwa hiyo chakula gani?”.Aliniuliza.
“Kalete kile unachoona kitanifaa mimi”.Nikamjibu huku namuangalia usoni.Hadi hapo nilikuwa namjibu majibu yangu kisomi zaidi. Kama angeelewa nachomaanisha,s
idhani kama angeuliza swali linalo fuata.
“Ok! Na kinywaji gani?”.
“Hicho niletee chako mwenyewe”.Nikamjibu.
“Changu mwenyewe kivipi?”.Akazidi kunichimba maswali.
“Kwani wewe una kinywaji gani?”.
“Mimi sina kinywaji”.
“Okey! Nitakwambia baadaye. Sasa hivi niletee chochote utakachokiona”.Nikamjibu na baada ya jibu hilo,akatoka kwa ajili ya kwenda kufanya nilichomuagiza.
Huku nyuma mimi nikabaki nawaza na kuwazua jinsi ya kumuingia yule Nesi Subira ambaye ndiyo alifanya hata ile sehemu ya kati ya shuka la hospitali ile kuwa kama pana panda na kushuka.
Baada ya kuwaza sana, niliamua saa nne au saa tano za usiku ule ndiyo nifanye niliyotumwa na shetani.
Baada ya dakika kama kumi na tano,Nesi Subira aliingia na kimfuko cheusi kidogo kilichosheheni chips mayai ndani yake pamoja kuku nusu. Wakati huo mkono wake wa kushoto alikuwa kabebelea maji ya kunywa na soda aina ya fanta.
“Dah! We dada unajua sana. Hivi ulijuaje kuwa napenda fanta?”.Nikamuuliza swali lingine la kisomi huku nikimaanisha fanta ni yeye kutokana na rangi aliyokuwa nayo.
“Mi ndo kinywaji changu hicho”.Alijibu huku anatabasamu.
“Ha ha haaa, na mayai je?”.Swali lingine la kisomi.
“Siyo saana, ila napenda yakiwa yamekaangwa”.Alijibu Nesi.
“Kwa hiyo yakiwa yamechemshwa na yapo tayari kuliwa na wewe, unaweza kuyala?”.Nilizidi kutema mafumbo.
“Mh! Ya kuchemsha mi siyo mpenzi”.Akajibu huku akizidi kutabasamu.
“Kwa hiyo mayai yaliyochemka hata mawili humalizi?”.
“Mawili tu! Hayo fasta,tena naongezea na koka”.
“Aaaah”.Nilihamaki huku nikiwa na furaha baada ya jibu lile.
“Eeee”.Akajibu.
“Basi poa. Nikimaliza nadhani nitalala,au utakuja kupiga stori na mimi?”.
“Mh! Sijui aisee. Ila nitaangalia si wajua vitu vya watu hivi”.Alinijibu wakati huo mimi nilishaanza kutupia kile chakula kinywani mwangu.
“Ok! Poa. Ngoja mimi nile kwanza kwa maana ili tumbo nahisi linanyonga kwa sababu halina kitu”.Nilimjibu yule Nesi na kisha alinikabidhi chenji yangu na kutoka mle wodini.
Sikutaka kumuonesha muda uleule nia yangu, mpango mzima nikaupanga ufanyike saa nne au saa tano kama kutatokea kikwazo kwenye saa nne.
Baada ya kumaliza kula na kunywa, nililala kwa kujiegesha huku akili yangu ikiwa inategea saa nne ifike.
*************
:: Nini kitaendelea?